Tatizo la kuahirisha mambo

Tatizo la kuahirisha mambo

Habari wana jf

Niende kwenye point nimekuwa na tatizo la kuahirisha vitu nivipangavyo... sio kwamba siwezi ila ukifika muda tu najikuta tu labda nafanya kitu then nasema nikimaliza nitafanya. Nitaendelea hivyo hivyo mishoni nasema kesho. Kesho inafika narudia nilicho fanya leo. Hili ni tatizo toka utotoni na huenda ningekua nimefanya makubwa mengi nisingekua na hii tabia...

Nimejaribu sana kuishinda ila utakuta nafanikisha kwa miezi kadhaa tu baada ya hapo narudi kwenye cycle hii hii. Nimeangalia videos mbalimbali YouTube kushinda procrastination ila nitazitumia kwa muda tu alafu hali inarudi kama mwanzo. Kwa mwenye tatizo kama langu jua haupo peke yako.

Mwenye uzoefu na njia thabiti ya kushinda hii kitu naomba msaada.

Kijana akishajigundua kuwa yeye ni kichaa tayari amepona.

Wewe ni kichaa aliyejitambua
 
Wachana na mambo ya Internet mkuu.
Suala lako liko kiroho zaidi. Wacha kuhangaika,hili ni suala la kiroho zaidi.
Nilikuwa hivyo,nilikutana na mtu akanipa mwanga.
Akanambia kama unaendaga kwa waganga wanakulia pesa zako bure tuu kama unaendaga.
Namshukuru Mungu,hali kwa sasa sio mbaya sana japo mwenyewe najifelisha.
 
Habari wana jf

Niende kwenye point nimekuwa na tatizo la kuahirisha vitu nivipangavyo... sio kwamba siwezi ila ukifika muda tu najikuta tu labda nafanya kitu then nasema nikimaliza nitafanya. Nitaendelea hivyo hivyo mishoni nasema kesho. Kesho inafika narudia nilicho fanya leo. Hili ni tatizo toka utotoni na huenda ningekua nimefanya makubwa mengi nisingekua na hii tabia...

Nimejaribu sana kuishinda ila utakuta nafanikisha kwa miezi kadhaa tu baada ya hapo narudi kwenye cycle hii hii. Nimeangalia videos mbalimbali YouTube kushinda procrastination ila nitazitumia kwa muda tu alafu hali inarudi kama mwanzo. Kwa mwenye tatizo kama langu jua haupo peke yako.

Mwenye uzoefu na njia thabiti ya kushinda hii kitu naomba msaada.

Kuna mmoja aliniambia kuwa, alivyoanza kulipa ada za shule kila kitu kilikuwa sawa. Kwenye dili alifika kwa wakati. Kila jambo aliliboresha bila ya kusukumwa na mtu.
 
Wachana na mambo ya Internet mkuu.
Suala lako liko kiroho zaidi. Wacha kuhangaika,hili ni suala la kiroho zaidi.
Nilikuwa hivyo,nilikutana na mtu akanipa mwanga.
Akanambia kama unaendaga kwa waganga wanakulia pesa zako bure tuu kama unaendaga.
Namshukuru Mungu,hali kwa sasa sio mbaya sana japo mwenyewe najifelisha.
Nilitaka kujua tatizo la kiroho zaidi na ulilishindaje?
 
Jaribu kuinstall application ya reminder kwenye simu yako.

Kuhairisha hufuatana na usahaulifu na kupuuza vitu.

Njia nyingine ni uwe na notebook unaandika " to -do list ", ukikamilisha unaweka vema njia nzuri ni pangilia task zako kutoka nyepesi kwenda ngumu (simple to complex).
 
Sometimes Kuna mambo labda yanatokea unaona siyo ya muhimu sana kufanya, hivyo unakuta labda unaghairi ghairi hivyo ukilifanya litakusaidia Kwa namna Fulani na usipofanya haikupungizii kitu lakini naamini kama lingekuwa ni jambo la lazima ungelifanya tu, lakini kama unaghairi Kwa mambo ya msingi kabisa basi Kuna shida mahali na hiyo shida inaweza kuwa ni hofu ya kushindwa jambo, kutokujiamini kwenye kufanya mambo Fulani Fulani, kujifelisha kabla ya kuanza labda kwasababu ya overthinking...suluhisho la Hilo nadhani ni mentality tu, hivyo nashauri uwe positive na usahau yote uliyoghairi halafu pata muda wa kupangilia vyote unavyotaka kufanya kwenye kijidaftari chako then weka nadhiri halafu Fanya moja kati ya mengi unavyotaka kufanya, utaona unaanza kuizoea ile Hali ya kufanya jambo.

Tatizo ninaloliona ambalo wengi huwakumba na hili ni kutokuwa na malengo yaliyopangika yani ile Hali ya kupanga mipango ya kimaisha Kwa kuanza na hicho na kumaliza na hicho na kutenga muda wa kuboresha malengo yako, yaani lazima uwe na malengo ya muda mrefu na mfupi Sasa shida inakuja Kuna vitu vinaingia hapa kati ambavyo unataka pia uvifanye ambapo kimsingi havipo kwenye malengo yako makubwa na uliyoanza nayo hivyo kughairi kwingi hutokea pia.Jaribu kuwa mwenyewe tafakari maisha yako ww mwenyewe usichanganye ishu za maisha yako na mitazamo ya wengine, usikubali mitazamo yako unayoiamini iingiliwe na mitazamo ya wengine kiasi ambacho huvuruga dhana nzima ya kuboresha mtazamo wako.
Nakushauri pia uwe interdependent, kuwa proactive siyo mchezo ujue!.
 
Jaribu kuinstall application ya reminder kwenye simu yako.

Kuhairisha hufuatana na usahaulifu na kupuuza vitu.

Njia nyingine ni uwe na notebook unaandika " to -do list ", ukimalisha unaweka vema njia nzuri ni pangilia task zako kutoka nyepesi kwenda ngumu (simple to complex).
Asante sana, nitafanyia kazi.
 
Sometimes Kuna mambo labda yanatokea unaona siyo ya muhimu sana kufanya, hivyo unakuta labda unaghairi ghairi hivyo ukilifanya litakusaidia Kwa namna Fulani na usipofanya haikupungizii kitu lakini naamini kama lingekuwa ni jambo la lazima ungelifanya tu, lakini kama unaghairi Kwa mambo ya msingi kabisa basi Kuna shida mahali na hiyo shida inaweza kuwa ni hofu ya kushindwa jambo, kutokujiamini kwenye kufanya mambo Fulani Fulani, kujifelisha kabla ya kuanza labda kwasababu ya overthinking...suluhisho la Hilo nadhani ni mentality tu, hivyo nashauri uwe positive na usahau yote uliyoghairi halafu pata muda wa kupangilia vyote unavyotaka kufanya kwenye kijidaftari chako then weka nadhiri halafu Fanya moja kati ya mengi unavyotaka kufanya, utaona unaanza kuizoea ile Hali ya kufanya jambo.

Tatizo ninaloliona ambalo wengi huwakumba na hili ni kutokuwa na malengo yaliyopangika yani ile Hali ya kupanga mipango ya kimaisha Kwa kuanza na hicho na kumaliza na hicho na kutenga muda wa kuboresha malengo yako, yaani lazima uwe na malengo ya muda mrefu na mfupi Sasa shida inakuja Kuna vitu vinaingia hapa kati ambavyo unataka pia uvifanye ambapo kimsingi havipo kwenye malengo yako makubwa na uliyoanza nayo hivyo kughairi kwingi hutokea pia.Jaribu kuwa mwenyewe tafakari maisha yako ww mwenyewe usichanganye ishu za maisha yako na mitazamo ya wengine, usikubali mitazamo yako unayoiamini iingiliwe na mitazamo ya wengine kiasi ambacho huvuruga dhana nzima ya kuboresha mtazamo wako.
Nakushauri pia uwe interdependent, kuwa proactive siyo mchezo ujue!.
Nashukuru sana mkuu, hasa swala la over thinking huwa linanikumba sana, nahisi swala la kupangilia vitu ni la muhimu sana, pia kuwa na clarity kipi kiwe na priority. Kingine pia kuwa na mipango mingi, mpk unachanganykiwa uanze na lipi uache lipi! Nahisi hii njia yako yakupa kipaumbele jambo moja la muhimu kwanza ni wazo zuri ntalifanyia kazi.
 
Habari wanaJF,

Niende kwenye point, nimekuwa na tatizo la kuahirisha vitu nivipangavyo. Siyo kwamba siwezi ila ukifika muda tu najikuta tu labda nafanya kitu then nasema nikimaliza nitafanya. Nitaendelea hivyo hivyo mwishoni nasema kesho. Kesho inafika narudia nilichofanya leo. Hili ni tatizo toka utotoni na huenda ningekuwa nimefanya makubwa mengi nisingekuwa na hii tabia.

Nimejaribu sana kuishinda ila utakuta nafanikisha kwa miezi kadhaa tu baada ya hapo narudi kwenye cycle hii hii. Nimeangalia videos mbalimbali YouTube kushinda procrastination ila nitazitumia kwa muda tu halafu hali inarudi kama mwanzo. Kwa mwenye tatizo kama langu jua haupo peke yako.

Mwenye uzoefu na njia thabiti ya kushinda hii kitu naomba msaada.
Hilo ndo tatizo la kuchelewesha mambo badala ya kuchukua maamuzi haraka uwezavyo. Kumbuka "procrastination is thief of time".
 
Nilitaka kujua tatizo la kiroho zaidi na ulilishindaje?
Nilianza kuhisi kuna itilafu mahali baada ya kuona vingi nikianzisha simalizi au vinafeli.
Mf;Kidato cha pili nilibahatika kupata ufadhili wa masomo,mambo yakavurugikaa.
Nilipata binti wa kiarabu,akaanza kunilipia chuo. Mwaka wa mwisho mambo yakavurugika kabisaa.
Nikapata mwanamke wa kizungu, mambo yakavurugikaaa.
Biashara nyingi nikianzisha zunakufaa
Miaka zaidi ya 10 si mchezo, ila Mungu huwa anawakati wake. Nikakutana na mtu akanipa mwanga na naiona tofauti.
Sitakiwi kunywa pombe,bali natakiwa kuwaasa watu wasinywe pombe hovyo.
Sitakiwi kugegeda hovyo wanawake.
Natakiwa kusaidia haswa jamii flani
Natakiwa kusali sana.
Tangu nimeanza kiukweli naiona tofauti ktk maisha yangu.
Kipato nakiona
Afya inaridhisha.
Biashara inapepea
Maono napata
Napata usingizi mzuri
Kiroho sio mbaya,nguvu ipo.
Ila nimejisahau sana, nakula sana mchemsho so nimenenepa sana na naonekana ninapesa hivyo inaniletea matatizo kwa ndugu na jamii😅😅😁
 
Duuh lifestyle ndo ilikua tatizo naona.
 
Habari wanaJF,

Niende kwenye point, nimekuwa na tatizo la kuahirisha vitu nivipangavyo. Siyo kwamba siwezi ila ukifika muda tu najikuta tu labda nafanya kitu then nasema nikimaliza nitafanya. Nitaendelea hivyo hivyo mwishoni nasema kesho. Kesho inafika narudia nilichofanya leo. Hili ni tatizo toka utotoni na huenda ningekuwa nimefanya makubwa mengi nisingekuwa na hii tabia.

Nimejaribu sana kuishinda ila utakuta nafanikisha kwa miezi kadhaa tu baada ya hapo narudi kwenye cycle hii hii. Nimeangalia videos mbalimbali YouTube kushinda procrastination ila nitazitumia kwa muda tu halafu hali inarudi kama mwanzo. Kwa mwenye tatizo kama langu jua haupo peke yako.

Mwenye uzoefu na njia thabiti ya kushinda hii kitu naomba msaada.
Bro nahisi kuna vitu vidogo vidogo sana vinavyoshika haramu in your plans,viache hivyo you will thank me
 
Back
Top Bottom