Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Rejea mada tajwa hapo juu.

Nina mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 10 sasa lakini bado anakojoa kitandani, nafikiria kwa umri huu ni mkubwa mtu kukojoa kitandani.

Tafadhali wakuu naomba mnisaidie nini chakufanya, kuna tiba ya tatizo hilo?
Mugabe dawa ya huyu dogo ni rahisi mno

Issue yake ni unconscious activity ukitumia nguvu utafeli.

Mwambie alale kitandani kwake hasa usiku mfano saa nne au tano baada ya hapo mwambie ajikojolee kama kawaida yake akiwa yupo macho, msisitize ajikojolee kwa sababu ile adha ya kujilowanisha, joto la mkojo na aibu ndio vitakuwa vinamkurupusha awapo katika usingizi kila akitaka kujikojolea kwa kuwa taarifa hizo zitakuwa tayari saved katika medulla oblangata Kumbuka hii ni unconscious activity controlled by medulla.
 
Hajawahi kuwaona vikojozi, kwenye familia yetu (hadi watoto wa bro) mtoto akishaacha kunyonya na kukojoa kitandani kunaisha inabaki ile ya mara moja moja. Ila kuna mtoto wa dada yangu hadi ana miaka 12 bado analimwaga
Mimi Kaka yangu niliyemfwata ameacha kukojoa akiwa form 4.

Wengine wote mara baada ya kuacha kunyonya tuliacha kukojoa.

Yeye sasa alikuwa kikojozi.

Mzee alimpiga sana lakini wapi..tena alikuwa anaumwaga kitanda chote hadi mnamuonea huruma.

Ikawa kila siku lazima afue,aoge,aanike godoro.

Kuna dawa ilikuja kumsaidia,now yaani ni msafi huyoo acha.
 
Hawa wanaobeza utafikiri wao ndo walezi wazuri alafu matoto yao yanavuta bangi pumbav.....toa suruhisho sio maneno ya kwenye kanga....umejuaje kama hamchapi kama ni ugonjwa je? au matatizo ya akili???.... Africans sisi ni kuhukumu na kulaumu ndo tunachoweza...
 
Wengi wanaobeza bado hawana familia
Na kama wanazo basi wana watoto wadogo ambao hata miaka 5 hawajafika.
Hii hali bado hawajaiexperience kwenye familia zao.
 
Rejea mada tajwa hapo juu.

Nina mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 10 sasa lakini bado anakojoa kitandani, nafikiria kwa umri huu ni mkubwa mtu kukojoa kitandani.

Tafadhali wakuu naomba mnisaidie nini chakufanya, kuna tiba ya tatizo hilo?
Hakikisha anakojoa kabla ya kulala. Muamshe usiku akakojoe mara mbili au mara tatu. Hakuna dawa nyingine. Usipofanya hivyo ataendelea kukojoa hadi mtu mzima. Usiwasikilize wanaosema unamlea vibaya.
 
Wana JF msiwe mnaandika ili kujifurahisha eti ni uzembe mzazi/wazazi hell no! Kukojoa kwa mtoto haina uhusiano na malezi wala sio makusudi ya mtoto ni out of control situation ambayo inasababishwa na either mtoto kuwa na usingizi mzito sana, kibofu kidogo kinachoshindwa kuhimili kuzuia mkojo, unywaji wa vimiminika vingi kabla ya kulala na kushindwa kuamka. Na matatizo mengine ya kiafya.

Kwa baadhi ya watoto hali hii huisha baada ya kufikisha miaka sita na wengine huendelea hadi miaka 15.

Namna ya kuzuia zipo nyingi ningemshauri mleta mada aingie kwenye google atazikuta nyingi ila katika hizo njia hakuna kumchapa mtoto, Kumkemea, Kumfokea, kumdhalilisha kwa wenzake kama comments nyingi za "wataalam" zinavyoashiria hapa.

Kila la kheri katika siku yetu wakulima wenzangu.
 
 
Ushauri murua kabisa na akikosa dawa hiyo amtafutie nyingine inaitwa Amitiplline
 
Rejea mada tajwa hapo juu.

Nina mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 10 sasa lakini bado anakojoa kitandani, nafikiria kwa umri huu ni mkubwa mtu kukojoa kitandani.

Tafadhali wakuu naomba mnisaidie nini chakufanya, kuna tiba ya tatizo hilo?
Akifikisha birth-urinating-day ya miaka 11 nialike

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rejea mada tajwa hapo juu.

Nina mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 10 sasa lakini bado anakojoa kitandani, nafikiria kwa umri huu ni mkubwa mtu kukojoa kitandani.

Tafadhali wakuu naomba mnisaidie nini chakufanya, kuna tiba ya tatizo hilo?
Mfuatilie kwa karibu. Asinywe maji karibu na muda wa kulala, muamshe, saa 1 tangu baada ya kulala, na kila baada ya masaa 3 mpaka kuche. Utampa mazoea ya yeye mwenyewe kujiamsha.
 
Sema tunakuwaga na akili sana aisee tuliokojoa masafa marefu.Mimi nilikoma nilipofika form 1.
Hili tatizo mtu asipojua anaweza sema ni maksudi lakini muhusika unakuwa huna control nalo kabisa hata upewe kipigo cha mbwa koko.
Nina mtoto wa father yetu mkubwa yuko form v saizi lakini bado analimwaga.
Hatar sana.
 
Wee Mzee binti wa miaka 6 anawezaje kufanya zoezi hili?

Hizi Dawa zako balaa.
 
Mawasiliano si ndio hii thread? au tayari unataka kugeuza fursa!

Sema Dawa hapa wanufaike wengi, ingekuwa watu wote kama wewe JF ingepoteza maana na wala isingekuwa na msaada kwa watu.
Kila mtu ana taratibu zake mkuu, so nafanya kile ninachoona ni sawa kwa upande wangu, mtu akiona anageuzwa fursa au anataka kutapeliwa, simply anakaa tu kimya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…