Tatizo la Kukosa Hedhi (Amenorrhea)

Tatizo la Kukosa Hedhi (Amenorrhea)

Shukrani..tatzo linasababishwa na nin? Mana hosptal wanasema ni kawaida.
Mkuu Chocs kama wanavyosema huko hospitali ni Mabadiliko ya mwili wa Mwanamke inatokea kwa kila Mwanamke hii lakini sio kwa wote baadhi yao huwa ndio hivyo sio maradhi.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu KAUMZA Pole sana kwa shemeji yetu hatoki hedhi dawa nitakupa za Tiba Mbadala jaribu mojawapo wa dawa zangu hizo 5 kwa kutumia kwa muda wa siku 3 kisha uje hapa unipe Feedback.

DAWA ZA KUTEREMSHA HEDHI.

Ikiwa hedhi imezuilika kwa kufikia umri wa kumaliza au ni kwasababu ya mimba, inafahamika lakini ikiwa si kwasababu mbili hizo basi hufanyiwa dawa na kuirudisha hedhi.

1. Kunywa chai ya mdalasini.

2. Mvuje ukinywewa pamoja na pilipilimanga huteremsha hedhi iliyo fungwa katika uzai au mapito yake.

3. Manemane ukiponda na ukinywa siku tatu asubuhi kabla ya kula chakula

4. Kitunguu Saumu na maganda yake huteremsha hedhi

5. Kunywa maji yaliyochemshwa na Zaatari.

Chanzo.MziziMkavu Mtaalam wa Sayansi za Kiafrika Tiba za Asili.
 
  • Swali kwa Madaktari (linatokana na hii thread): "Je mwanamke asipopata kwa muda mrefu siku zake kuna madhara yeyote kiafya kwake?." Kama ilivyo kwa mpendwa wa mleta mada.
Aksante
 
  • Swali kwa Madaktari (linatokana na hii thread): "Je mwanamke asipopata kwa muda mrefu siku zake kuna madhara yeyote kiafya kwake?." Kama ilivyo kwa mpendwa wa mleta mada.
Aksante

Kukosa Hedhi (Amenorrhea)

amenorrhea.jpg


Tatizo la kukosa hedhi ni jambo ambalo linawakumba wanawake wengi waliovunja ungo. Aidha suala hili limekuwa likiwaletea usumbufu mwingi wa kisaikolojia wanawake wengi waliowahi kukumbana nalo.


Tatizo la kukosa hedhi au amenorrhea linaweza kutokea awali kabisa (primary) au baadaye kabisa maishani (secondary).


Primary amenorrhea ni hali ya kukosa hedhi inayoweza kumtokea msichana aliye katika umri wa kuvunja ungo na ambayo huweza kuendana na hali ya kukosa mabadiliko ya kubalehe kama vile kuota matiti au nywele za kinena; au msichana anaweza kuwa na mabadiliko ya kubalehe lakini asipate hedhi.


Secondary amenorrhea ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke ambaye si mjamzito, hanyonyeshi, na ambaye hajavuka umri wa kukosa hedhi (menopause) na wala hatumii njia za uzazi wa mpango kama vile sindano au vidonge, na ambaye hapo awali alikuwa akipata hedhi kama kawaida lakini akasimama kwa miezi mitatu au zaidi.


Mwanamke hupataje hedhi?


Ili mwanamke aweze kuwa na mzunguko ulio sahihi wa hedhi, ni lazima matezi yake ya hypothalamus na pituitary pamoja na kiwanda cha kutengeneza mayai ya kike (ovaries) na mji wa mimba (uterus) vifanye kazi zake sawasawa.


Hypothalamus huchochea tezi la pituitary kuzalisha hormone chochezi ya follicle au follicle-stimulating hormone (FSH) pamoja na homoni ya luteinizing (LH). Hizi FSH na LH kwa pamoja huchochea ovaries kuzalisha homoni za estrogen pamoja na progesterone. Kazi za estrogen na progesterone ni kusababisha mabadiliko katika ukuta wa uterus yaani endometrium ikiwepo kupata hedhi. Ili damu ya hedhi iweze kutoka nje, njia ya uzazi ya mwanamke haina budi kuwa huru yaani isiyo na matatizo yeyote yale.


Amenorrhea husababishwa na nini?


Visababishi vya amenorrhea vyaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu, vile vinavyohusisha matatizo katika mfumo wa homoni, vile vinavyohusisha matatizo ya kimaumbile katika njia ya uzazi ya mwanamke na vile vinavyohusisha mabadiliko katika mwili wa mwanamke.


Matatizo katika mfumo wa homoni: Matatizo katika mfumo wa homoni yanaweza kuwa katika tezi za hypothalamus, pituitary au ovary.

Matatizo katika Hypothalamus: Matatizo katika hypothalamus yanayoweza kusababisha mwanamke kukosa hedhi ni pamoja na

Uvimbe katika ubongo karibu na tezi ya pituitary

Ukosefu au upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwa via vya uzazi. Ugonjwa huu

hujulikana kama Kallmann syndrome
Lishe duni na utapia mlo

Uzito mdogo kuliko kawaida (kukonda kwa kupitiliza)

Matatizo katika tezi ya Pituitary: Vyanzo vinavyohusisha tezi ya pituitary ni pamoja na
Kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin katika damu au kwa kitaalamu Prolactinemia. Prolactin

ni homoni inayochochea uzalishaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha. Hali ya kuwa na prolactin nyingi katika damu inaweza kutokea iwapo kuna uvimbe unaoitwa (prolactinoma) katika tezi ya pituitary.

Kuwepo kwa uvimbe mwingine wowote katika tezi ya pituitary.

Pituitary kushindwa kufanya kazi baada ya seli zake kufa, hususani iwapo mama alipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.

Kuharibika kwa tezi ya pituitary baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili.
Kuwa na historia ya kupata tiba ya mionzi inayohusisha tezi ya pituitary.

Matatizo katika ovary: Vyanzo vinavyohusisha matatizo katika viwanda vya kuzalisha mayai ya kike yaani ovaries ni pamoja na

Kutozalishwa kabisa kwa mayai (Anovulation)

Kuwepo kwa kiwango kingi cha homoni za kiume katika damu (Hyperandrogenemia)

Ovary kuwa na vifukovifuko (Polycystic ovarian syndrome) na kushindwa kufanya kazi zake vizuri. Haya ni matatizo ya homoni ambayo huwapata baadhi ya wanawake walio katika umri wa kuzaa

Kufa na kushindwa kufanya kazi kwa ovary kabla ya muda wake
Ugonjwa wa kuzaliwa unaoitwa Turner syndrome ambao humbatana na kukosekana kwa ovary au ovary kuwa changa kuliko kawaida, msichana kushindwa kuvunja ungo na msichana kuwa na kimo kifupi kuliko kawaida.

Ugonjwa huu hutokana na matatizo ya kijenitikia (genetic disease)
Ukosefu wa kimaumbile wa ovary ambao hutokea wakati wa ukuaji

Kufa kwa ovary baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili
Historia ya kuwahi kupata tiba ya mionzi au madawa yanaathiri ovary

Ugonjwa wa kurithi wa Galactosemia unaoambatana na kuwa na kiwango cha juu cha sukari aina ya galactose katika damu

Matatizo ya kimaumbile katika njia ya uzazi: Matatizo ya kimaumbile katika njia ya mfumo wa uzazi wa mwanamke yanayoweza kusababisha ukosefu wa hedhi ni pamoja na

Mwanamke/msichana kuzaliwa bila kuwa na uke, shingo ya uzazi au mji wa mimba (uterus)
Kuta za uterus zinazotazamana kujishikiza pamoja

Utando unaozunguka uke (hymen) kuziba kabisa na kukosekana kwa tundu la kupitishia damu ya hedhi (imperforate hymen)

Kuwepo kwa utando unaokatiza katika uke unaozuia damu ya hedhi kushindwa kutoka
Mabadiliko katika mwili wa mwanamke: Mambo yanayoweza kuathiri mwili wa mwanamke na kumfanya ashindwe kupata hedhi ni pamoja na

Kula kiasi kidogo sana cha chakula kuliko kawaida au kula kupita kiasi
Unene uliopitiliza au kupungua uzito/kukonda isivyo kawaida
Uwepo wa magonjwa sugu kama kifua kikuu
Utapiamlo
Msongo wa mawazo
Matumizi ya madawa ya kulevya

Matumizi ya baadhi ya madawa hususani baadhi ya dawa za kutibu magonjwa ya akili
Kuwa na hofu iliyopitiliza
Kufanya mazoezi ya mwili kupita kiasi

Dalili za Amenorrhea ni zipi?


Kukosa hedhi siyo ugonjwa bali ni dalili ya kuwepo kwa tatizo au ugonjwa fulani katika mwili. Kulingana na ugonjwa unaosababisha tatizo hili, kukosa hedhi kunaweza kuambatana pia na


Matiti kutoa maziwa wakati mwanamke si mjamzito na wala hanyonyeshi, maumivu ya kichwa na matatizo katika kuona vitu ambavyo kwa pamoja vinaweza kuashiria uwepo wa uvimbe katika ubongo

Mwanamke kuwa na nywele na vinyweleo vingi mwilini na kuota ndevu kama mwanaume hali inayoashiria kuwepo kwa wingi kwa homoni za kiume za androgen

Ukavu katika uke, kutoka jasho sana wakati wa usiku, au mabadiliko katika kupata usingizi vinaweza kuashiria matatizo katika ovary
Kuongezeka uzito kupita kiasi au kupungua kwa uzito isivyo kawaida
Mwanamke kuwa na mhemko kuliko kawaida yaweza kuashiria kuwepo kwa matatizo ya kiakili na kisaikolojia
Uchunguzi na vipimo


Msichana yeyote aliyefikia umri wa kubalehe na kuvunja ungo na ambaye bado hajaanza kupata mabadiliko yeyote ya kubalehe katika mwili wake hana budi kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Aidha msichana aliyefikia umri wa miaka 16 na ambaye bado hajaanza kupata hedhi anatakiwa pia kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi.


Kwa wanawake waliokuwa wakipata hedhi kama kawaida lakini ghafla wakaacha kupata kwa muda wa miezi mitatu mfululizo au zaidi nao pia hawana budi kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi wa tatizo hili.


Vipimo vifuatavyo vinaweza kufanywa kuchunguza sababu za kukosa hedhi kwa mwanamke:


Kupima damu kwa ajili ya kuchunguza kiwango cha homoni za FSH, LH, TSH na prolactin ambazo uzalishwaji wake unachochewa na tezi ya pituitary, na pia kupima kiwango cha homoni ya estrogen inayozalishwa na ovary.

Kipimo cha ultrasound ya nyonga kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa matatizo katika njia ya uzazi na pia kuchunguza hali ya ovary.

CT scan au MRI ya kichwa kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa matatizo kwenye tezi ya pituitary au hypothalamus.

Vipimo vya kufahamu ufanyaji kazi wa tezi ya thyroid

Kupima damu ili kufahamu kiwango cha homoni ya prolactin katika damu
Kuchunguza uterus kwa kutumia aina ya X-ray inayoitwa Hysterosalpingogram na kipimo kingine kiitwacho Hysteroscopy ambacho huchunguza chumba cha uterus.
Matibabu ya kukosa hedhi


Matibabu ya kukosa hedhi yanaweza kufanyika nyumbani bila kuhitaji dawa, ingawa pia, kutegemeana na chanzo cha tatizo, yanaweza kuhitaji dawa na hata upasuaji wakati mwingine.

Matibabu yasiyohitaji dawa


Baadhi ya wanawake wanaopata tatizo la kukosa hedhi kwa sababu ya kujinyima kula (wanaofanya dieting) na hivyo kupata upungufu wa virutubisho mwilini, wanashauriwa kula lishe bora.

Baadhi ya wanawake wanaopata tatizo hili la kukosa hedhi kwa sababu ya kuongezeka uzito kupitiliza, wanashauriwa kuwa makini katika aina ya vyakula wanavyokula ili kuwa na uzito unaotakiwa.

Wanawake wanaokosa hedhi kwa sababu ya kufanya mazoezi ya mwili kupita kiasi wanashauriwa kujiwekea kiasi katika ufanyaji wao wa mazoezi.

Iwapo kukosa hedhi kumesababishwa na msongo wa mawazo, ni jambo jema kutafuta njia za kushughulikia matatizo hayo na kuyatatua ili kuondoa msongo wa mawazo

Inashauriwa kutokuvuta sigara na kuacha kunywa kunywa pombe.

Matibabu yanayohitaji dawa: Matibabu ya kukosa hedhi hutegemea chanzo cha tatizo. Matibabu huelekezwa katika kutibu chanzo, na iwapo chanzo cha tatizo ni matatizo ya kimaumbile, upasuaji unaweza kufanyika. Kwa

wanawake wenye matatizo ya kuwa na kiwango kingi cha prolactin, daktari anaweza kushauri matumizi ya dawa aina ya bromocriptine au pergolide. Kwa wanawake wenye upungufu wa homoni ya estrogen au wale

wenye matatizo katika ovary zao, dawa zenye kurejesha homoni hiyo zaweza pia kutumika. Wakati mwingine dawa za uzazi wa mpango zaweza kutumika kurejesha mzunguko wa hedhi na pia kusaidia kuongeza kiwango cha homoni ya estrogen mwilini.

Upasuaji: Upasuaji unaweza kufanywa iwapo kuna

Uvimbe katika ubongo unaoathiri tezi ya pituitary na hypothalamus

Matatizo katika njia ya uzazi ya mwanamke

Je kukosa hedhi kunaweza kusababisha nisipate mtoto?


Ikumbukwe kuwa, kukosa hedhi si ugonjwa bali ni dalili ya kuwepo tatizo hivyo basi iwapo tatizo hilo lina uhusiano na kutunga mimba na kupata mtoto, uwezekano wa kupata mtoto utakuwa mdogo ikiwa tatizo hilo

halitashughulikiwa. Matatizo kwenye tezi za pituitary, hypothalamus pamoja na ovary ambayo yana uhusiano

mkubwa na kukosa hedhi, husababisha pia tatizo la ugumba. Iwapo matatizo hayo yatashughulikiwa ipasavyo, uwezekano wa kupata kupata hedhi na hatimaye kupata mimba huwa mkubwa.Kukosa Hedhi (Amenorrhea)

Chanzo.https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/325245-kukosa-hedhi-amenorrhea.html
 
Je anatumia dawa zozote za uzazi wa mpango?
Mh hio PRIMOLUTE ni dawa inayotumiwa wa watu wanaopata hedhi isiyo na mpangilio(unregular mensturation)/mapungufu ya progesterone hormone na watu wanaodhamiria kusogeza siku za hedhi..Na hio dosage si sahihi vilevile haitakiwi kutumiwa kwa muda mrefu maximum ni siku 14.
Hio CLOMID ni dawa ya kusaidia upate OVULATION(OVULATORY DYSFUNCTION IN WOMEN DESIRING PREGNANCY) inaweza kutumika incase of secondary amenorrhea na matumizi yake ni 50 mg daily for 5 days(from the 5.day of menstrual cycle if the pasient has menstruation).
Since amejaribu hizo dawa mbili bila mafanikio anatakiwa apatiwe GONADOTROPINE-(follitropin alpha/follitropin beta/urofollitropin)..
 
Wakati ule nazaa ilikuwa nikijifungua nakaa miezi kama 24 kabla ya kuanza kupata siku tena. but was long time ago.
 
Habari zenu wakuu. mimi ni mama ninaye nyonyesha mtoto wa miezi kumi sasa. nilianza kupata cku zangu mtoto alipokuwa na miezi miwili ila nimeshangaa ghafla mwezi huu cjapata cku zangu na si mjamzito.Niliugua typhoid mpaka sasa nipo kwenye dozi ya typhoid inaweza kuwa sababu? asanteni
 
Ni kawaida kwa mama anayenyonyesha kutokupa hedhi, au kupata mwezi huu mwezi mwingine usione kabisa.so ni hali ya kawaida mamy
 
asanteni ndugu zangu Qute cherry na Dinazarde kwa majibu nilipata wasiwasi nikahisi labda nitakuwa na tatizo.asanteni sana
 
asanteni ndugu zangu Qute cherry na Dinazarde kwa majibu nilipata wasiwasi nikahisi labda nitakuwa na tatizo.asanteni sana

Ndio hivyo na huwezi beba mimba mpaka utakapoachishaa kumnyonyesha mtoto,ukimuachisha utaingia mwezini kama kawaaida
 
Habari zenu wapendwa wa jukwaa la elimu ya afya. kama kichwa kinavoeleza, mke wangu nimeanza ishi nae takribani mwaka sasaa, ila anashindwa kupata hedhi yake karibu mwezi wa 8 sasaaa. tulienda hospital akapewa dawa za kuregulate mzunguko wake wa hedhi, hiyo ilimuwezesha kupata hedhi mara moja tuuu na ilikuwa Februaly but mpaka sasa hajapata tena. nipeni ushauri, tatizo ni nini na suluhisho laweza kuwa nini. kuanzia miaka miwili kurudi nyuma alikuwa anapata hedhi japo sometimes alikuwa anaruka mwezi mmoja.
 
Rudini tena Hospital then akafanyiwe ultrasound angaliwe vizuri kizazi chake na mfumo mzima wa mfuko wake wa uzazi
 
Kabla ya kwenda hospital na kupata hizo dawa ka kuregulate hedhi yake. tulianzia kwa Dr. akaangaliwa kwa Ultrasound yes ikaonekana kuna kiuvimbe, ktk mfumo wa uzazi, yule dr. akasema twende ktk chumba cha magonjwa ya akina mama, alipofika huko dr. wa magonjwa ya akina mama akasema huo uvimbe sio tatizo, and some time huisha wenyewe, ndipo akatupa hizo dawa za kuregulate mzunguko wake
 
habari jf doctor.
Nina miaka 27.Awali nilikuwa siijui tarehe yangu ya kubleed kutokana na kitokuwa na constant date.lakn naona tatizo limeendelea kwa kukosa kabisa kuona siku zangu huu ni mwezi wa nne sasa.sijawai kutumia kitu chochote kuhusu uzazi wa mpango.nahitaji mtoto ila siku sizioni naombeni msaada wa ushauri .na nini sababu ya hayo .
 
habari jf doctor.
Nina miaka 27.Awali nilikuwa siijui tarehe yangu ya kubleed kutokana na kitokuwa na constant date.lakn naona tatizo limeendelea kwa kukosa kabisa kuona siku zangu huu ni mwezi wa nne sasa.sijawai kutumia kitu chochote kuhusu uzazi wa mpango.nahitaji mtoto ila siku sizioni naombeni msaada wa ushauri .na nini sababu ya hayo .

Sijajua we we ni muumini wa upande UPI ila wakati mwingine haya mambo ni Spiritual pia.
 
Back
Top Bottom