Tatizo la kumbukumbu iliyopitiliza

Mkuu inaoneka una ujuzi na haya mambo,asilimia 95 ya mambo ulivyosema juu ya maisha yangu ni kweli.
Diet-hapa hua sili wala kunywa kila ambacho macho yanatamani
Sleep-Hii hua nazingatia sana kuanza saa 6 hadi 8
Medication-mara nyingi natumia herbs tu, za hospital mara chache
Genetics-Hapa ndio sina uhakika ila wazazi wanatunza sana document maana hata cheti cha clinic ninacho walinipa
Cognitive training-Hapa nahisi kukariri zile lyrics za nyimbo tangu nikiwa mdogo nahisi ilinisaidia, pia nilikua mchoraji sana
 
Huna kazi au miradi ya kukuweka busy.

TAFUTA HELA. Nikuibie siri ,hao jamaa zako sio kama hawakukumbuki ila wanakukataa kwa sababu umechacha.
 
Chai
 
Unaweza kutukumbusha siku yako ya mwisho kunyonyeshwa ilikuwaje?

Tupe experience yako kidogo mkuu
 
Mkuu hakuna kitu kimenifurahisha kama kupata mtu ambaye tuna experience maisha ya aina moja.

ulichokiandika ni asilimia 90% mimi pia napitia.

Nakumbuka utoto wangu kwa asilimia kubwa sana

matukio mengi ya yaliyowahi kutokea uko nyuma harufu,ata nyimbo mfano

just a dream -nelly
nakumbuka mara ya kwanza nilisikiliZa wapi nilihisi nini

kadharika nachukia hii hali kuna watu waliongea vizuri au vibaya kuhusu mimi mpaka leo nakumbuka

mfano:kuna mama aliniambiaga uyu mtoto atakuja kuwa na akili sana
nikiwa darasa la 3.

kuna jamaa yangu zangu waliwahi niokoa nikiwa nataka kuendelea mtoni,nikiwa darasa la 2,cha ajabu wao walishasahau

naikumbuka picha ya kwanza iliyokaa kichwani mwangu kuhusu dar,nakumbuka mwalimu wa chekechea alivyokuwa ananitreat

nakumbuka baadhi ya tabia zangu mbaya na njema za utoto

hizo ni za miaka mingi iliyopita

kuhusu mpenzi nakumbuka harufu za wanawake wote nimewahi kula nao

ndio maana baada ya kugundua harufu za wanawake nimewahi kulala nao zinanisumbua niliacha kujihusisha na ngono mpaka ndoa.

na mengi naweza kushare hapa ila tu nilichokuja kujua

mimi naumizwa zaidi na maneno kuliko kitu Chochote

nidhurumiwe,niachwe,nikose kazi sihumi kabisa.


lakini ukisema jambo baya au jema sikusahau kabisa najitahidi kuwa mr I don't care lakini nashindwa nimekaa na vitu vingi kifuani nashindwa nivitolee wapi inaumiza sana
 
Daah mimi mechi ya kwanza kuangalia kwenye TV ilikua Cameroon vs Argentina WC 1990 lakini nakumbuka wachezaji karibu wote hadi sub zao pamoja na matukio ya rafu aliyofanyiwa Armando Maradona....Makanaki kiungo muhimu alitolewa na kadi nyekundu..
 
Mkuu nashukuru umeeleza kile ambacho unakipitia,naona tunafanana, tena bora umeingia deep hasa kwa mademu, mimi niliamua mengine nisiandike kiundani ila kiukweli kukumbuka vitu vingi sana wakati mwingine kunaleta huzuni kama utaamua kuzingatia.
Na kama kilikuwa kizuri basi kitaendelea kunipa furaha kila ninapokumbuka
Kiukweli nilishagundua kusahau siwezi kwahio hua naamua kuishughulisha akili kwa kusoma vitabu, makala au kuangalia movie tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…