Tatizo la kupoteza kumbukumbu

Tatizo la kupoteza kumbukumbu

SHIGOTTO

Senior Member
Joined
Sep 4, 2018
Posts
156
Reaction score
282
Nawasalimu na kuwatakia afya njema, naomba kujuzwa mzee wangu mwenye umri wa miaka 83 amepata hali ya kupoteza kumbukumbu hii haijitokezi mara kwa mara, anasahau mambo yanayotokea muda huu kama vile kukumbuka mtu aliyekuja na kuondoka baada ya kumsalimia lakini vile vya zamani vyote anavikumbuka vizuri sana mfano majina ya rafiki zake,shule aliyosoma, ofisi aliyofanya kazi na vinginevyo.

Kwa vile hali hii ndo kwanza inaanza ningependa kujuwa kama kuna msaada wowote wa kukabiliana nayo kabla hali haijawa mbaya zaidi, naomba niwakilishe.
 
Hiyo ni dementia (kupoteza kumbukumbu) na ni kawaida sana kwa wazee wengi sana katika miaka hii.

Jaribu sana kumfanya awe active (wanasema inasaidia sana kuchemsha ubongo) na kujitahidi kusoma hata magazeti alimradi asikae 'idle'.

Hapo sasa ndiyo kazi ya ulezi wa mzazi inapoanza kwa uhakika na unatakiwa wewe na familia muwe na moyo ili kumsaidia mzee katika hii hatua ngumu kidogo na hapo ndiyo unapoambiwa pepo yako iko miguuni kwa wazazi wako.

Wa kwangu alipoteza memory ikafikia hatujui hata sisi watoto wake, kwa kweli ilikuwa inasikitisha sana. Hata kwenda msalani ilikuwa mpaka umkisie kama mtoto vile.
 
shukrani sana najitahid kadri Mungu anavyonijalia maana mimi ni mtoto pekee kwa baba na mama nashukuru kwa ushauri ndugu yangu
All the best, Mungu akupe nguvu za kuwahudumia wazazi wako. Utapata amani sana siku watayoondoka na kuelewa kwamba ulijitahidi kuwapa maisha bora katika siku zao za mwisho hapa ulimwenguni.
 
Uzee unaweza kuchangia pakubwa lkn hakikisha manjano hasa ile mbichi isikosekane kwenye chakla chake kuanzia chai na ...
 
Back
Top Bottom