Tatizo la kupumua kwenye chumba kidogo

Tatizo la kupumua kwenye chumba kidogo

Rusende

Senior Member
Joined
Jul 27, 2016
Posts
129
Reaction score
110
Wana-jamii wenzangu mimi nina tatizo la kupumua kwenye chumba kidogo, ama kwenye korido ndefu isiokuwa na uingizaji wa hewa fresh kutoka nje.

Aidha, nikipanda lift mara mlango unapofungwa hupata tabu sana ya kupumua, mara kadhaa hushindwa kuendelea na safari yangu ya floor ninayokwenda. Aidha, hupata tabu sana nipandandapo gari ndogo ikifungwa vioo pia hushindwa kupumua vizuri.

Nilipata maelezo kutoka kwa baadhi ya jamaa kuwa tatizo hilo ni upungufu wa hewa ya oksijen ktk mzunguuko wa damu mwilini mwangu.

Naomba ushauri kuhusu tatizo hili kwani nimekua napata shida sana mara inapotokea kupanda usafiri wa gari lililofungwa vioo licha ya kuwa na kiyoyozi ndani.
 
Wanaj jamii wenzangu Mimi Nina tatizo la kupumua kwenye chumba kidogo,ama kwenye corrido ndefu isiokuwa na uingizaji wa hewa fresh kutoka nje, Aidha nikipanda lift mara mlango unapofungwa hupata tabu sana ya kupumua,mara kadhaa hushindwa kuendelea na safari yangu ya floor ninayokwenda.aidha hupata tabu sana nipandandapo gari ndogo ikifungwa vioo pia hushindwa kupumua vizuri.nilipata maelezo kutoka kwa baadhi ya jamaa kuwa tatizo hilo ni upungufu wa hewa ya oksijen ktk mzunguuko wa damu mwilini mwangu.naomba ushauri kuhusu tatizo hili kwani nimekua napata shida sana mara inapotokea kupanda usafiri wa gari lililofungwa vioo licha ya kuwa na kiyoyozi ndani.
Una hofu ya enclosed space inayosababisha panic attack hivyo kushindwa kupumua vyema. Mawazo yangu nisiye mtaalamu wa udaktari
 
Naona tatizo lako na langu ni sawa kwa yote
Niliposoma nikasema huu uzi niliandika lini? Maana ni mimi kabisa
Claustrophobia kitaalamu
Nafikiri nikifungwa jela nakufa kabisa
Siwezi kupanda daladala na gari lazima nifungue kioo
 
Sahihi kabisa, mara nyingine ina bidi ujaribu kupotezea ama kwa kuchart kwa simu,vip hukupata kushauriwa lolote kuhusu changamoto hii?
 
Sahihi kabisa, mara nyingine ina bidi ujaribu kupotezea ama kwa kuchart kwa simu,vip hukupata kushauriwa lolote kuhusu changamoto hii?
Mkuu haina tiba ni woga tu huo
Nimekaa nao zaidi ya miaka 40
 
Pole Sana mkuu ....
Nilijua kupumua kumbe kupumua.....

na Imani utapata Tiba na tatizo litakwisha.
 
Pole sana fanya meditation ya pumzi ninzuri mno kwani hufungua kabisa kifua.
Hukufanya mfumo wa upumuaji kua mzuri sana.
Kwanini ni meditation??
Kwasababu hii meditation nitiba yamatatizo makubwa makubwa ya mwili na kiroho.
Sio jambo la mchezo nikitu cha ajabu sana mno.
Meditation yapumzi fanya ×2 kwasiku ndani yawiki mojatuu basi utapata matokea bora sana na afya yako itaiiimarika sana.
POLE SANA.
Baada yakua sawa usiache ndio itakua moja la zoezi lako hadi maisha yako.
 
Mkuu,We are the Inner,samahani sana,nilipata changamoto kidogo ya hand set yangu,ulinishauri kufanya meditation kuhusu tatizo langu la upumuaji kwenye enclosed space,naomba ufafanuzi kuhusu zoezi hilo la meditation mkuu.
 
Back
Top Bottom