Tatizo la kushindwa kumuangalia mtu usoni mkiwa mnaongea

Tatizo la kushindwa kumuangalia mtu usoni mkiwa mnaongea

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Hili ni tatizo la kisaikolojia ambalo nimegundua watu Wengi tunalo.

Mtu mnaonge yeye anaangalia chini. Ni uwoga na kukosa kujiamini. Ni vizuri tukaangalia wapi tunafeli.

Mimi binafsi watu walionizidi umri siwezi kuwakazia macho usoni ila watoto nawaangalia na wananielewa.
 
Hili ni tatizo la kisaikolojia ambalo nimegundua watu Wengi tunalo.

Mtu mnaonge yeye anaangalia chini.
Ukiwa na tabia kama hii nchi za Ulaya nk hutaaminika. Just jitahidi sana ubadilike. Hata ukienda kwenye interview yoyote unatakiwa uwaangalie machoni unaozungumza nao.

Usipifanya hivyo unaweza kufeli hata kama una sifa zinazotakiwa. Mara nyingi watu wanaoshindwa kuangalia wengine machoni wakati wa mzungumzo kuna jambo wanaficha au wanasema uongo.
 
Hoja nimeikubali hii.
Wakati mwingine hoja siyo kutokujiamini, bali sababu inaweza kuwa pia mila na desturi; ambapo kuangalia sana mtu usoni inaweza tafsiriwa kama ukosefu wa adabu.
Basi itakuwa mila mbovu sana. Mbona kabila langu ukiongea bila kumuangalia mtu machoni unadhani kuwa mtu mbaya. Hata sehemu waliyostaarabika ukifanya hivyo utaonekana hauko sawa. Ndiyo maana hata customer care workers wanatakiwa kumuangalia mteja machoni wakati wanazungumza.
 
Kwa mtu ambaye umezoeana naye kila siku unaonanan naye kama oficini au mitaani kumuangalia machoni inakuwa ni rahisi, tatizo ni pale ambapo uliyekutana naye ni mtu ambaye hamujazoeana naye mfano mgeni wako au jamaa tu mumekutana naye sehemu na kuanza kupiga naye story.
 
Kwa mtu ambaye umezoeana naye kila siku unaonanan naye kama oficini au mitaani kumuangalia machoni inakuwa ni rahisi,tatizo ni pale ambapo uliyekutana naye ni mtu ambaye hamujazoeana naye mfano mgeni wako au jamaa tu mumekutana naye sehemu na kuanza kupiga naye story.
Kumbe hili ni tatizo la wengi? Ohoo my God. Badilikeni. Mimi ukiwa mgeni ndiyo kwaaanza naona kuna umuhimu wa kuangaliana machoni wakati wa mazungumzo.
 
Nilikua na tatizo hili zamani, lkn nimeondokana nalo sahiz ukiongea na mm sipepesi macho pembeni.!
 
Basi itakuwa mila mbovu sana. Mbona kabila langu ukiongea bila kumuangalia mtu machoni unadhani kuwa mtu mbaya. Hata sehemu waliyostaarabika ukifanya hivyo utaonekana hauko sawa. Ndiyo maana hata customer care workers wanatakiwa kumuangalia mteja machoni wakati wanazungumza.
Ndio maana likawa ni kabila lako na sio kabila la mwingine.
 
Ukiwa na tabia kama hii nchi za Ulaya nk hutaaminika. Just jitahidi sana ubadilike. Hata ukienda kwenye interview yoyote unatakiwa uwaangalie machoni unaozungumza nao.

Usipifanya hivyo unaweza kufeli hata kama una sifa zinazotakiwa. Mara nyingi watu wanaoshindwa kuangalia wengine machoni wakati wa mzungumzo kuna jambo wanaficha au wanasema uongo
Classic one...
 
Sio
Hili ni tatizo la kisaikolojia ambalo nimegundua watu Wengi tunalo.

Mtu mnaonge yeye anaangalia chini.Ni uwoga na kukosa kujiamini. Ni vizuri tukaangalia wapi tunafeli.

Mimi binafsi watu walionizidi umri siwezi kuwakazia macho usoni ila watoto nawaangalia na wananielewa.
Sio mila na tamaduni zetu hizo! Tunaiga utamaduni wa nje huo!
Tunatazamana machoni bila kupepesa macho tunapogombana huku na mvua ya mate ikinyesha, sio wakati tupo kwenye maongezi na watu waliotuzidi umri au hadhi!
 
ndege JOHN una matatizo sana we kijana😁😁kuna thread yako unaongelea kutoweza kutongoza mpaka upige kilaji leo tena hapaa daah .
Hiyo inatokana na kutojiamini mkuu jifunze kuongea na watu bila kitu chochote kichwani utajenga kujiamini sana sana.
 
Hili ni tatizo la kisaikolojia ambalo nimegundua watu Wengi tunalo.

Mtu mnaonge yeye anaangalia chini.Ni uwoga na kukosa kujiamini. Ni vizuri tukaangalia wapi tunafeli.

Mimi binafsi watu walionizidi umri siwezi kuwakazia macho usoni ila watoto nawaangalia na wananielewa.
Mmh
 
Kwa kipindi hiki cha covid-19 ni mbinu ya kujikinga na mvua za rasharasha toka kwa waongeaji staili ya kabudi na si tatizo la kisaikolojia wala uoga.
Kwa watu wa aina ya uliyemtaja inaeleweka, si tu hutamwangalia, bali utakaa mbali.
 
Binafsi huo upuuzi siwezi..mm hata nikitongoza demu huwa nawaangalia machoni hadi anajikuta ananikubalia kwa hofu ya kuangaliwa hadi kipele dadeq..
 
Ndio maana likawa ni kabila lako na sio kabila la mwingine.
Ndiyo. Lakini sehemu na jamii nyingi, kuangalia mtu machoni wakati wa mazungumzo ndiyo tabia inayokubalika. Hujasikia watu wengi tu wanasema fulani huenda ni mwizi au mchawi kwani hathubutu kuangalia mtu machoni? Mambo yako hivi: 1. Unapoongea na mtu mtizame machoni. 2. Usimdokolee mtu macho kama ham-interact. (hii tabia wanayo sana wanaume wa Bongo kwa wanawake. Ukiwa majuu ukifanya hivyo utaonekana kama mwanga na mtu anaweza kukutukana)
 
Back
Top Bottom