Tatizo la kushindwa kumuangalia mtu usoni mkiwa mnaongea

Tatizo la kushindwa kumuangalia mtu usoni mkiwa mnaongea

Binafsi napenda sana kutazamana na mtu usoni, ni rahisi sana kutambua pale mtu anapokua anasema uongo kwa wale tunaojua kumsoma mtu machoni ..

Sent from my itel W5002 using JamiiForums mobile app
 
Hili jambo wakati mwingine mimi ninalo .
Naweza kuongea na mtu alafu katikati ya mazungumzo nakuwa sipendi kumuangalia sana usoni.

Huwa naweza kukuangalia usoni ila kwa muda mchache sana sio muda wote.

Mara nyingi nikiongea na mtu huwa najikuta namuangalia KWENYE PAJI LA USO.

Harakaharaka utasema namuangalia kumbe naangalia pale katikati ya macho mawili kwa juu kidogo

Sijui sababu hasa ni ipi inayonifanya niwe hivi.

Lakini hiyo haiathiri uwezo wangu wa kuongea.

Kwa mtu niliyemzoea kama mke wangu namuangalia saanaa na ndugu wengine
 
Mi kuna Sura nyingine sitaki kuzitazama usoni wakati tunaongea sababu naweza angua kicheko katikati ya mazungumzo. Weee kuna Sura zinatisha. Full comedy.
 
Mimi hata uwe nani naangea kwa kukuangalia usoni, ukiongea nakuangalia usoni...
 
Nadhani hii inatokana na kutokujiamini na aibu.Kwenye mawasiliano kuna kitu kinaitwa "body language"na macho ni part mojawapo. Kama mtu hasemi ukweli utamjua kupitia hilo,ana simanzi/furaha utajua pia,ana tamani /vutiwa au anadharau utajua.

Katika maongezi ni muhimu kutazamana machoni inatoa kithibitisho kwamba upande wa pili upo pamoja nawe,unakufatilia/sikiliza na kukuelewa.Isiwe kama kukodoleana macho ila macho yanakutana at certain times 👀
 
Basi itakuwa mila mbovu sana. Mbona kabila langu ukiongea bila kumuangalia mtu machoni unadhani kuwa mtu mbaya. Hata sehemu waliyostaarabika ukifanya hivyo utaonekana hauko sawa. Ndiyo maana hata customer care workers wanatakiwa kumuangalia mteja machoni wakati wanazungumza.
Watu wa Asia huwa hawamwangalii mtu usoni anayemzidi umri au cheo nazani ni mila na desturi ata sisi kwa kabila letu binti kukuangalia usoni ni utovu wa nidhani na wanaweza kumuhisi ameshakuwa kulumbembe.
 
Mil

Mila mbovu ni tafsiri yako
 
inategemeana na aina yamtu

Sitarajii umkute MTU shule IPO kipato chake pia kipo harafu eti aangalie chini mnavoongea

Wengine niumasikini unawapoza kwamba akitazama chini sana utamuona wamana

Kuna msemo niliupataga iringa enzi nasoma tosamaganga

#Imbwa ndavila panyi ye nyisi(isiyorasmi kwawasiojua kihehe,nihivi MBWA mtazama chini ndo mwizi....unaweza pishana nae anaingia jikoni ukirudi unakuta kalamba mpaka chungu
 
Watu wa Asia huwa hawamwangalii mtu usoni anayemzidi umri au cheo nazani ni mila na desturi ata sisi kwa kabila letu binti kukuangalia usoni ni utovu wa nidhani na wanaweza kumuhisi ameshakuwa kulumbembe.
Kweli kabisa binti au kijana mdogo kumkazia macho mtu mzima ni utovu wa nidhamu, ingawaje inategemea uhusiano binafsi na huyo mtu na aina ya mazungumzo.......hata wazungu hawapendi hii tabia ya kumkazia mtu macho, inaweza kuchukuliwa kama sign ya intimidation....kwa marafiki na watu mliozoeana mnaweza kutazamana machoni au wapenzi kwa ajili ya kupata attention au mahaba kwa mwenzako....
 
Nadhani hii inatokana na kutokujiamini na aibu.Kwenye mawasiliano kuna kitu kinaitwa "body language"na macho ni part mojawapo. Kama mtu hasemi ukweli utamjua kupitia hilo,ana simanzi/furaha utajua pia,ana tamani /vutiwa au anadharau utajua.

Katika maongezi ni muhimu kutazamana machoni inatoa kithibitisho kwamba upande wa pili upo pamoja nawe,unakufatilia/sikiliza na kukuelewa.Isiwe kama kukodoleana macho ila macho yanakutana at certain times 👀
Nitapenda unifundishe hilo, vipi siye ambao tunapenda kusikiliza na kuelewa kutumia masikio na ubongo zaidi kuliko macho. Watu mnaopenda kukazia macho watu mnaoongea nao mtakuwa na hulka ya kutowaamini wengine au mna hisia kali za kudanganywa au kusalitiwa....au tuseme mnapenda attention sana hasa mademu.
 
Wakati mwingine hoja siyo kutokujiamini, bali sababu inaweza kuwa pia mila na desturi; ambapo kuangalia sana mtu usoni inaweza tafsiriwa kama ukosefu wa adabu.
Which in actual sense it's not true hence no need to bother. Always keep an eye contact.
 
Back
Top Bottom