Tatizo la kutosikia vizuri na body balance

Tatizo la kutosikia vizuri na body balance

iddy eba

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2015
Posts
573
Reaction score
1,171
Wakuu mimi ni kijana(19 years now) nina tatizo la kutosikia vizuri na body balance(nimesoma science kidogo naelewa masikio ndio yanayo control body balance) hili tatizo limenianza mda sana tangu nipo mdogo wa miaka kama 9 hivi sasa limekuwa kubwa kiasi kwamba nahitaji attention kubwa sana kuongea na mtu na mara nyingi nikitembea huwa siendi sawa(napepesuka mda mwingine hadi kudondoka).

Hospital nimeenda mara y kwanza muhimbili mwaka 2009 na mama nilichunguzwa nikaambiwa nahitaji hearing device na kwa kuwa gharama ilikuwa kubwa bi mkubwa alishindwa kumudu, by 2012 baba akafanikiwa kuipata hiyo hearing device ambapo niliitumia ila ikawa nikivaa sana masikio yanazidi kuuma, hii ilipelekea kwenda tena Hospital mara hii ikiwa ni CCBRT hapo tukaambiwa twende ekenwa(Hospital flani hivi ipo magomeni) tulivyofika pale na kupimwa solution ilikuwa kutumia kwanza dawa flani hivi zinaitwa neorouns(kama sijakosea) kwa miezi mitatu mfululizo then nikimaliza niendelee kutumia hearing device.

Hii haikuniletea nafuu yoyote mpaka namaliza form four na kwenda likizo ifakara kwa babu, nikiwa huko baada ya miezi kadhaa masikio yakawa ya nauma sana, nikapelekwa Hospital na babu (st Francis Hospital ifakara) baada ya kunichunguza wakaniandikia barua ya rufaa kwenda muhimbili surgery department.. Baada ya Kurudi dar na kwenda muhimbili mzee akanambia gharama ni kubwa sana kwa sasa na yeye hana pesa.

Natumai kuna madaktari humu mnipe japo ushauri wa nini cha kufanya maana nimeshindwa kwenda chuo sababu ya masikio na naona kadri siku zinavyokwenda ndivyo yanavyozidi kupoteza uwezo wake.

Natumai mtanisaidia kwa hili Doctors

USHAURI NA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU
Pole sana mkuu,

Mkuu mi nakushauri nenda chuo kasome hata medical lab, mbona watu wenye shida kama yako wapo wengi tu,

Mimi niliwahi kuugua kama wewe na nilipita kote huko ulikopita , tena zaidi mpaka mwananyamala na sinza hospital, Bugando.

Hiyo dawa uliyoitaja niliwahi kupewa na profesor wilyoma pale Bugando ilinisaidia kwa muda japo haikumaliza tatizo,

Now nipo fresh japo asilimia ndogo sana imebaki niwe perfect na mtu hawezi kunijua,
Mpaka nimwambie, kiufupi nsha pona

Kwa hapa dar es salaam usipokuwa makini macho yatafuata, utaanza kuona ukungu,

KILICHONISAIDIA
1.Acha kula vyakula vya m gengeni na viwandani kama vile soda, juice, bia , blue band n.k
Tumia maji tu ya kunywa kama mbadala

2.Kula matunda kwa wingi

3.Fanya mazoezi, anza kwa kuruka kamba nyumbani kidogo kidogo then anza mazoezu ya kutembea na kukimbia (epuka kulala lala ovyo)

3.Jisomee biblia au insppiration books (muhimu).

Mkuu
Ushapona tayari.

NB: Fuata ushauri niliokupa epuka tiba za hawa jamaa wanaojiita wataalam wa asili , huko kote nimepita sikupona mpaka nikaamua kuoka,

Mungu ni mwema now siha y angu ni njema kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app

in short tuko wengi, hata mimi since 2007 sikio la kulia limeziba kabisa, haliumi nmeenda muhimbili wakanikatazaga tu nisile kisamvu na mihongo na kelele.

kwakweli nimepitia mengi sana kuhusu sikio mpaka sina hamu hapa nilipo...nmeamua kukubali hali yangu tu. Siwezagi kulala sehemu za kelele au kama tunaongea na cm uko kwenye kelele nazisikia kelele badala ya wewe.. yani nahitaji utulivu wa akili kiasi kwamba ikitokea mikelele navurugika
 
Pole sana mkuu aisee

Sent from my Apple iPhone 5s using JamiiForums Auto-reply Mobile app
 
Hata mimi nina hiyo shida kwa zaidi ya miaka 10 sasa,nilitibiwa Muhimbili kwa madawa haikuwezekana at last nikaambiwa nitumie hearing aids,nimezitumia lakini zina adha zake ukikaa nazo muda mrefu zikiwa ON masikio yanakuwa hayasikii kabisa,nimeachana nazo ninaishi ninavyojua mwenyewe.

Kifupi masikio naona hayana tiba,ila ni kumuomba Mungu,hakuna linaloshindikana kwake ,nina matumaini kuwa siku moja masikio yangu yatasikia tena,niko kwenye maombi na sitarudi nyuma kwa hilo,mpaka nimepokea muujiza wangu.
 
Hyo hearing sioni kama inasaidia kwa kwely, maana wengi tuliozitumia tuishia kuachana nazo
 
Pole sana mkuu,

Mkuu mi nakushauri nenda chuo kasome hata medical lab, mbona watu wenye shida kama yako wapo wengi tu,

Mimi niliwahi kuugua kama wewe na nilipita kote huko ulikopita , tena zaidi mpaka mwananyamala na sinza hospital, Bugando.

Hiyo dawa uliyoitaja niliwahi kupewa na profesor wilyoma pale Bugando ilinisaidia kwa muda japo haikumaliza tatizo,

Now nipo fresh japo asilimia ndogo sana imebaki niwe perfect na mtu hawezi kunijua,
Mpaka nimwambie, kiufupi nsha pona

Kwa hapa dar es salaam usipokuwa makini macho yatafuata, utaanza kuona ukungu,

KILICHONISAIDIA
1.Acha kula vyakula vya m gengeni na viwandani kama vile soda, juice, bia , blue band n.k
Tumia maji tu ya kunywa kama mbadala

2.Kula matunda kwa wingi

3.Fanya mazoezi, anza kwa kuruka kamba nyumbani kidogo kidogo then anza mazoezu ya kutembea na kukimbia (epuka kulala lala ovyo)

3.Jisomee biblia au insppiration books (muhimu).

Mkuu
Ushapona tayari.

NB: Fuata ushauri niliokupa epuka tiba za hawa jamaa wanaojiita wataalam wa asili , huko kote nimepita sikupona mpaka nikaamua kuoka,

Mungu ni mwema now siha y angu ni njema kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana kaka mkubwa LUCKDUBE . Ni kweli macho yameanza kuzingua siku za karibuni, nitajaribu kufata ushauri wako
 
The mind has a power to create and heal the diseases. If you want to heal your body then, just change your mind and thoughts. The conventional doctors wound but the mind heals.
 
Back
Top Bottom