Tatizo la kuumwa kichwa sana

Tatizo la kuumwa kichwa sana

Redrose20

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
213
Reaction score
35
Salam kwenu wana jf.

Jamani mimi nina tatizo la kuumwa kichwa sana nimekua mtu wa kutembea na kiboksi cha panadol,nimepiga xray ya kichwa lakini sina tatizo ila naumwa sana sana kichwa.

Kama kuna dawa naomba mnijulishe..

Ushauri tafadhali.
 
Kinauma wkt wte tu,nimeshapima macho nimepewa miwan lkn kwa ss naona km hainisaidii..nateseka sn
 
Salam kwenu wana jf.jaman mm nina tatizo la kuumwa kichwa sn nimekua mtu wa kutembea na kiboksi cha panadol,nimepiga xray ya kichwa lkn sina ttz ila naumwa sn sn kichwa..km kuna dawa naomba mnijulishe..ushaur tafadhal.
Una tatizo kama la mke wangu.Na mimi ninatafta dawa ya hili tatizo
 
Una tatizo kama la mke wangu.Na mimi ninatafta dawa ya hili tatizo
Kichwa cha mkeo kinaumaje?Anaweza kuwa na migrene!!Chunguza kinauma wakati gani mfano kukiwa na mwanga mkali,au akila spicy food au stress?.Ajaribu kuepuka factors zinazosababisha kichwa kuanza kuuma .Anaweza kutumia pia Imigran/sumatriptan tablets.
 
Salam kwenu wana jf.jaman mm nina tatizo la kuumwa kichwa sn nimekua mtu wa kutembea na kiboksi cha panadol,nimepiga xray ya kichwa lkn sina ttz ila naumwa sn sn kichwa..km kuna dawa naomba mnijulishe..ushaur tafadhal.

Usitumie sana panadol utaharibu figo zako.tafuta mafuta ya samli kisha mwagia usawa wa juu wa kichwa chako (ifike kwenye ngozi kama una nywele nyingi) utulie kama nusu saa fanya hivyo asubuhi na jioni siku 5 tatizo litaisha.
 
je,unapata choo vizuri? jioni unapataga baridi? kama kuna tatizo kati ya hizo ni pm.nitakuelekeza sehemu ukachukue tiba mbadala.hivi navyo husababisha.
 
Usitumie sana panadol utaharibu figo zako.tafuta mafuta ya samli kisha mwagia usawa wa juu wa kichwa chako (ifike kwenye ngozi kama una nywele nyingi) utulie kama nusu saa fanya hivyo asubuhi na jioni siku 5 tatizo litaisha.

nani kakwambia panadol inaharibu figo?
 
Salam kwenu wana jf.jaman mm nina tatizo la kuumwa kichwa sn nimekua mtu wa kutembea na kiboksi cha panadol,nimepiga xray ya kichwa lkn sina ttz ila naumwa sn sn kichwa..km kuna dawa naomba mnijulishe..ushaur tafadhal.

Tafuta mafuta ya mzaituni halafu changanya na mafuta ya ndimu na mafuta ya kitungu saumu halafu unapaka utosini,matokeo uni PM!
 
Salam kwenu wana jf.jaman mm nina tatizo la kuumwa kichwa sn nimekua mtu wa kutembea na kiboksi cha panadol,nimepiga xray ya kichwa lkn sina ttz ila naumwa sn sn kichwa..km kuna dawa naomba mnijulishe..ushaur tafadhal.

Mke wangu baada ya kupata ujauzito ndo ugonjwa wake. Juan hapana, jioni siku nyingine balaa, baris sometime na Mapigo ya moyo kwenda kasi.

Alipimwa akakutwa na malaria moja wkt huo alikuwa amesha meza metacafrine. Dr. Alimwambia metacafrine kwa mimba changa ilikatazwa.
 
Mke Wangu naye baada ya kujifungua kwanjia ya operation akaanza kupata hilo tatizo kinaumwa hasa saa za asubuhi sana
Alipokwenda kairuki akafanyia xray hawakugundua chochote ila walimshauri inawezekana anamawazo na mikazo huenda ndiyo inayopelekea hali hiyo.
 
Dah..jamani mimi pia naumwa na kichwa hatari..mpaka naweka barafu kwenye mfuke naweka kwenye paji la uso....
 
Asanten sn kwa ushaur wenu,nitayafanyia kaz yote.b bleced!
 
Wana JF,

Ahsanteni sana kwa moyo wenu na muda-mtakapoweza kunisaidia.

mimi kwa ghafla nilianza kuumwa kichwa kama 1 month,nikatibiwa hospitali za mkoani ikashindikana.
Wkasema wameshindwa.

Kinauma upande wa kisogoni na mbele ya uso juu ya macho, lakini nilikuwa nakunywa dawa na kuweka kitambaa cha maji baridi.

siku 4 zilizopita hali ikawa mbaya nikaja kwa emergency flight-DAR.

Nimefanyiwa MRI/kichwa lakini majibu yako sawa-sina tatizo.

Kwa hiyo naanza kufuatailia kujua wapi naweza kupata dr./specialist wa kuniokoa,jana kimeniuma usiku wote.

Kinauma upande wa mbele,muda wote najiokoa kwa kulia tu.Nimepewa pain killers lakini zikiisha bado tatizo liko pale pale.

Naomba niokoe, gharama si tatizo nina uwezo wa popote ,ili mradi nijue nakwenda wapi au kwa Dr.yupi au specialist yupi ambaye ni mzuri kwa Matatizo ya kichwa hapa DAR.

Ahsante.

RE
 
pole mkuu kama madaktari hawaoni tatizo hapo nihatari..
hebu jaribu kutibu KIPANDAUSO.

halafu Dar umetibiwa hospital gani?
 
Back
Top Bottom