Tatizo la kuunguruma kwa tumbo

Tatizo la kuunguruma kwa tumbo

umbwa

Member
Joined
Sep 9, 2013
Posts
25
Reaction score
1
wapendwa wanajukwaa mi nina tatizo ambalo nina imani wengi wetu pia linawasumbua na kuwakera. Tatizo lenyewe ni tumbo kutoa sauti inayokera . Wengi husema ni kwa sababu ya njaa lakini mimi hunitokea hata kama nimeshiba. Siumii ila inanikera kwani inanipunguzia kujiamini .naomba kujua inasababishwa na nini ?na njia za kutibu?
 
punguza kula na jamba inapobidi usijibane

sasa utajamba kwenye kikao au darasani? Unajua sio kila wakati unakuwa katika position ya kutoa hiyo gas.... Yan sijui nifanyeje?
 
ha ha ha hii ndio dawa? maana hata mimi hapa sasa hivi linanguruma sana na sijala chochote
Hahaha, wewe sasa inabidi uende haja kubwa hicho ni chakula cha jana. Indication kwamba process is done so toilet ndio inahitajika
 
Yawezekana hizo ni dalili za vidonda vya tumbo,kuna wakati hiyo gesi haina harufu sio?
 
yan gesi inakuwa nyingi na haina harufu mbaya kama ushuzi wa sikuzote......
 
yah.... Thanks ila huko net lugha inakuwa complex sana ndo maana natafuta mtaalamu mswahili mwenzangu
nimesoma hiyo link kwanza jaribu kutokula vyakula vya mafuta{ila sina uhakika}ila kuna mmoja ame comment kuwa,solution ni kula taratibu na usijaze chakula mdomoni na ukitafune mpaka kisagike vya kutosha,na usinye maji katikati ya mlo isipokuwa maji ya uvuguvugu{mmh hii ngumu}.unapokula haraka haraka na bila kutafuna vizuri na bila chakula kusagika vya kutosha,inasababisha chakula tumboni kifanye kazi ya ziada kwenye mfumo wa kusaga chakula ulichokula.maybe hiyo ndio hali ya kusababisha mngurumo wa tumbo.sijui kama ni kweli maybe ma dokta humu watasaidia
 
Back
Top Bottom