Tatizo la kuwa na harufu mbaya kinywani (bad breath) - Chanzo, dawa za kuzuia na ushauri

Tatizo la kuwa na harufu mbaya kinywani (bad breath) - Chanzo, dawa za kuzuia na ushauri

Hakuna dawa, ni kuoga, kubadili nguo, kupiga mswaki hata mara3 kwa siku,
 
Natumai mu wazima wa afya wana jf. Mimi nina rafiki yangu ana tatizo la kunuka kinywa hata na mwili hasa kwa mwili pale anapofanya kazi ndogo tu je ni aina gani ya dawa anapaswa kutumia?
Mwambie huyo Rafiki yako ale kipande cha Tangawizi mbichi kila siku asubuhi na usiku kwa muda wa siku 30 atakuwa amepona huyo kunuka mdomo. chanzo.Herbalist Dr.MziziMkavu
 
Jamani tuwe makini kwa Mambo ya msingi hasa maradhi mtu kaomba msaada kwa anae jua Tiba ya kunuka mdomo , matokeo mtu analeta utani ,malipo hapa hapa utazaa mtoto nae ananuka mdomo au mpenzi wako ,Sasa sijui utabadili Id yao uombe msaada , maana hamna jinsi utajibiwa kikauzu hivi hivi tena watanukuu ulichoandika mkuu!
 
1.COLGATE MAXFRESH TRASPARENT TUBE
2.MBEGU ZA MLONGE +CHUMVI MAWE
 
Kuna dawa ya meno inaitwa CLOSE UP made in Kenya zipo za aina mbili Kijani na Nyekundu mimi natumia nyekundu ina nifaa sana nimehangaika sana na tatizo hilo naona hiyo dawa omekuwa mkombozi wangu. Kwa sasa siwezi brush meno yangu pasipo dawa hiyo ntafanya lolote niipate.
Niliwahi kutumia hata zile za forever bright zinazouzwa kuanzia 15000 na kuendelea, Colget, Aha, Angola, whitedent, na zingine nyingi hazikunisaidia. Nikaenda hospitali mara nyingi nikawa naoshwa mdomo napewa vidonge na kuambiwa ninunue Mouth wash navyo havikunisaidia siku moja nilipomweleza tatizo langu dereva wetu kazni kwetu akanambia Boss kuna dawa ya meno inaitwa CLOSE UP from that day namsile kama kawa. May Almighty bless that driver.
 
Kama hutojali huyo rafiki yako akijaribu kutumia hiyo dawa naomba unipatie feedback Mkuu.
 
Saizi nasmile kama kawa jaribu Close Up
hivi mtu usipoambiwa na mtu mwingine, wewe kama wewe uligunduaje kuwa mdomo unanuka? ile harufu unaweza kuihisi wewe mwenyewe?

Nauliza tu nipate kufahamu
 
hivi mtu usipoambiwa na mtu mwingine, wewe kama wewe uligunduaje kuwa mdomo unanuka? ile harufu unaweza kuihisi wewe mwenyewe?

Nauliza tu nipate kufahamu
Hili swali lako linalenga kupata taarifa gani?
 
Habarini za kazi,

Mimi ni kijana nina umri wa miaka 31 kwa sasa, ninatatizo linalonisumbua sana hadi nakosa raha kabisa, nilienda pharmacy nikapewa dawa ya kusukutua na nyingine kama mafuta naweka mdomoni inakaa wa mda kama dakika mbili, nili itumia kwa mda lakini tatizo bado liko pale pale, yaani napata shida sana.

Naomba msaada wenu jamani.
 
acha kuzama chumvini mkuu, pia acha sigara kama unatumia, na pombe, weka utaratibu wa kusafisha kinywa mara kwa mara, hasa kabla ya kulala
 
Back
Top Bottom