Tatizo la kuwa na harufu mbaya kinywani (bad breath) - Chanzo, dawa za kuzuia na ushauri

Tatizo la kuwa na harufu mbaya kinywani (bad breath) - Chanzo, dawa za kuzuia na ushauri

Tatizo lako ni dogo tu kijana.

Jitahidi unapopiga mswaki uwe unasugua ulimi kwa sababu chakula huwa kinaangukia na kuburuzwa hapo wakati wote wa kula,unaposahau kuukosha ulimi na ikawa ni suala la muda mrefu basi mabaki ya chakula yanagandana baadae hutoa harufu.

Sugua ulimi wako kwa mswaki usiokuwa mgumu sana kuepusha michubuko na vidonda ulimini.

Jambo lingine jitahidi kupiga mswaki kila baada ya kula chakula na usiweke kipaumbele sana kupiga mswaki wakati wa kuamka na kulala,bali kipaumbele iwe kila unapokula chakula cha ratiba yako upige mswaki na iwe ndio tabia yako hiyo.

Tatu tafuta dawa inaitwa sensodyne bei ni kuanzia 12000 hii dawa nzuri sana kwa mambo ya kinywani uwe unatumia hiyo kama dawa yako ya maisha japo bei kubwa,kama huwezi tafuta dawa zingine za meno nzuri.

Pia unapopiga mswaki piga juu chini juu chini,na sio ile kushoto kulia kushoto kulia.

Piga katika kila engo.

Vuta picha unapopiga mswaki basi mswaki wako uwe unaishia katika nafasi baina ya jino na jino(hapa ngumu kuelewa,ni kama ile juu chini)
 
Mie sio Dr ila nilimsoma Chris Lukosi alisema uwe unatafuna Tangawizi kila asubuhi pia inasaidia kutibu magonjwa mengine ukiachana na hilo lako.
 
Nilikuwa na hii shida nikiwa sekondari ila shida yangu nikajua ipo sehemu gani.

1. Kama una tabia ya kutafuna vinyama ndani ya kinywa acha, mimi baada ya kuacha niliona mabadiliko makubwa...
Tatizo lako ni dogo tu kijana.

Jitahidi unapopiga mswaki uwe unasugua ulimi kwa sababu chakula huwa kinaangukia na kuburuzwa hapo wakati wote wa kula,unaposahau kuukosha ulimi na ikawa ni suala la muda mrefu basi mabaki ya chakula yanagandana baadae hutoa harufu...
Nashkuru sana ndugu zangu kwa ushauri mlionipa hakika nitaufanyia kazi.
 
Ngoja na mimi nikupe eperience yangu.

Mkuu harufu mbaya itaondoka kwako ukijitahidi usafi wa kinywa chako.

Mi nakushauri unapopiga nswaki zingatia haya:

1. Usitumie mswaki wako zaidi ya miezi2.

2. Sugua vizuri meno yako pande zote za kinywa pamoja na ulimi wako.

3. Weka dawa ya meno mara mbili na ya kutosha pia hapa namaanisha kuwa unaweka dawa mara ya kwanza unasugua meno yako vizuri na ulimi kisha unatema na kusukutua,kisha unaweka dawa tena unasugua tena meno na ulimi vizuri ila povu da dawa usiteme liache kwa muda hata wa dk5 mpaka 8 huku kama unalisukutua ndani baada ya hapo ndo uliteme na kupitisha mswaki kisha usukutue na maji.

4. Sababu ww una tatizo waweza piga ht mara tatu kwa awamu moja ya usafi wa kinywa.

5. Kama una meno yenye matobo usiruhusu mabaki ya vyakula hayakai kwa muda mrefu baada ya kula so piga mswaki kila mara baada ya kula ili kuyaondoa mabaki kinywani.

NB: Hapa tumechangia tukiassume tatizo linasababishwa na kinywa ila niliwahi kusikia kuna wwngine tatizo huwa linatoka ktk njia ya chakula yaani kuanzia hapo kwa msosi tunapomezea kwenda ndani huko so km utaona njia zote za kusafisha kinywa zimedunda basi nenda hospitali waeleze wakucheck na hilo pia.

Pole sana mkuu naimagine unayopitia kwenye mahusiano yako na dada zetu walivyo na nyodo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja na mm nikupe eperience yangu.

Mkuu harufu mbaya itaondoka kwako ukijitahidi usafi wa kinywa chako.

Mi nakushauri unapopiga nswaki zingatia haya:

1.Usitumie mswaki wako zaidi ya miezi2...
Asante sana kwa ushauri mzuri ulionipatia Mungu azidi kukubariki.
 
Pole sana kw hiyo hali.

Kwanza hakikisha unaenda kusafisha kinywa walau mara mbili kwa mwaka(Kuna tabaka huwa linaganda kati ya meno ambayo yanakuwa ni malimbikizo ya vyakula mwisho huganda na kuwa vigumu,hivi huchangia sana harufu mbaya mdomoni hivyo inatakiwa vikasafishwe.yaan kati ya jino na jino ibaki fizi tu.unaweza angalia hapa meno ya mbele kwa ndani uone kama hizo calculi hazipo.

Pili hakikisha baada ya kula unafanya flossing,tafuta flossing thread zinapatikana pharmacy ukishamaliza kula unapitisha uzi huu kati ya meno kwa kinywa kizima.

Lakini pia tumia miswaki mizuri na uhakikishe unapiga mswaki kila kona ya kinywa chako bila kusahau ulimi.

Kila la kheri.

NB kusafisha kinywa kwa dentist ni muhimu mno kama hatua ya kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana kw hiyo hali.
Kwanza hakikisha unaenda kusafisha kinywa walau mara mbili kwa mwaka(Kuna tabaka huwa linaganda kati ya meno ambayo yanakuwa ni malimbikizo ya vyakula mwisho huganda na kuwa vigumu,hivi huchangia sana harufu mbaya mdomoni hivyo inatakiwa vikasafishwe.yaan kati ya jino na jino ibaki fizi tu...
👏👏👏
 
Pole sana kw hiyo hali.
Kwanza hakikisha unaenda kusafisha kinywa walau mara mbili kwa mwaka(Kuna tabaka huwa linaganda kati ya meno ambayo yanakuwa ni malimbikizo ya vyakula mwisho huganda na kuwa vigumu,hivi huchangia sana harufu mbaya mdomoni hivyo inatakiwa vikasafishwe.yaan kati ya jino na jino ibaki fizi tu.unaweza angalia hapa meno ya mbele kwa ndani uone kama hizo calculi hazipo...
Hiyo flossing thread ni bei gani ndugu?
 
Shukrani sana ndugu

Wanangu wa A town inakuaje??
Mkuu wala usipate shida ww ukishakuwa sawa nitafute km nilivyokuambia, na baada ya kutumia dawa ntakayokupatia naomba usisahau kurudisha mrejesho hapa, unajua ckuwa nafahamu km upo serious kiasi hiki, ww pambana ukishapata iyo hela ya dawa niliyokuambia basi nitafute, nishawasaidia wengi wenye tatizo km lako na wamenishukuru, so usiwe na wasi wasi ndugu tatizo lako limekwisha, japo ukipona usisahau kurudisha mrejesho hapa hapa kwenye huu uzi.
 
Sawa kaka
 
Sawa kaka
Yah wala usije kupoteza tena pesa yako, watu wamepoteza sn pesa kwa hili tatizo na bado liko pale pale, kuna jamaa yeye ni kutoka mwanza aliweka uzi humu tangu mwaka 2013 km ckosei, nimekuja kumtibu mwaka jana mwishoni.
 
[emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Una kisukari? , Pressure?, Ana vidonda vya tumbo?
Hivyo pia hupelekea kutoa harufu mbaya 0762291006

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivyo vingine sina ila ninadhani nina vidonda vya tumbo maana hizi dalili ninazo;

*Kiungulia
*tumbo Kujaa gesi
*Kutopata choo vizuri
*Maumivu ya mgongo, n.k

Kwahiyo vidonda vya tumbo navyo ni chanzo cha tatizo??
 
Nenda hospitali ukacheki km ni vidonda vya tumbo, km unavyo pia utancheki kuna dawa ya asili naijua ni kiboko ya vidonda vya tumbo ila wanauza bei ya juu kidogo 40,000 ukimaliza hyo uko poa, but narudia tena hata ukipona hvyo vidonda bado tatizo lako la harufu litabaki palepale labda lipungue tu, ili kulimaliza hilo tatizo ni muhimu kuniona pia.
 
Asante sana mkuu, kuhusu kukuona ondoa shaka.
 
Back
Top Bottom