Tatizo la Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu na kuwashwa sehemu za siri kwa wanaume na wanawake- Fahamu chanzo, Dalili na Matibabu yake

Mimi huo ugonjwa ulinipata toka 2016 nikaapuzia kuutibia mpaka mwaka huu 2019 ulipozidi ndo nikaona nitafute tiba nikaenda pharmacy nikamwelezea doctor akanipa iyo dawa ukioga unapaka sijamaliza at week nishapona kabisa
 
Mi nina (fangasi) mabaka mwili mzima hasa mgongoni, nilitumia dawa za mahospitalini za kunywa na kupaka, nikatumia vitunguu hadi maji ya break, yakawa yanapotea baada ya muda yanarudi

sasa yanarudi tena sijui tatizo nini
Tatzo la huu ugonjwa huwa unajirudiarudia sijui Kwann hata Kama ulipona ukawa fresh kabsa
 
Nenda hospitali kiongozi kwa wataalam wa magonjwa ya ngozi, niliwahi kuwa na tatizo hilo sio kiwango chako.
Umechelewa sana kushughulikia tatizo, ila usafi pia muhimu lazima uoge mara mbili kwa siku na uhakikishe sehemu zenye tatizo unakausha vizuri kwa taulo safi, sio taulo miezi haujafua tatizo halitoisha
 
mkuu wai hospital . Pia nakushauri usi google izo dalili .. ku google dalili za ugonjwa ni njia ya kujiaminisha muda kufa umefika
 
Dawa ya izo fangasi ni usafi mkuu ,kama mtangulizi mmoja amesema hapo juu tupa boxer zote anza upya
.jitahidi muda wote pawe pakavu sehemu za siri ,ukihisi jasho ingia wash room kausha na kitambaa au tissue paper then endelea na mizunguko..vaa boxer ndani 12 hours, jitahidi uwe na kitaulo kidogo kisafi kwa ajili ya kukausha sehemu za pumbu ,then lete mrejesho
 
Nunua dawa ya Iodine tincture. Vaa gloves, paka na pamba sehemu zenye muwasho. Ila kabla ya kulipaka pumbu, hakikisha unalipaka with a thin layer of lotion then iodine inafuata. Ukilipaka Iodine hivi hivi, cha moto utakiona.
 
Shukran
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…