Tatizo la machinga: Sasa Serikali imeanza kuamka toka usingizi wa ganzi

Tatizo la machinga: Sasa Serikali imeanza kuamka toka usingizi wa ganzi

Toka Serikali ya Awamu ya Tano ilipoanza kuwatukuza "wanyonge" kundi ambalo wamachinga wakaingizwa, ganzi iliingiwa kisawaswa katika vyombo karibia vyote vya dola.

Rsis wa wakati huo alirudia rudia kuwa yeye yupo pale kwa ajili ya wanyonge, hivyo wasibugudhiwe mijini.

Matokeo ya miaka mitano ya hii anarchism kutoka kwa wanyonge hao, yameonekana miji yote nchini.

Ikawa biashara ya machinga ni popote alipo binadamu.
Migahawa, nyanya na kabichi, nguo, viatu, vyombo vya ndani vyote vikavamia barabarani.

Barabara zikawa zinagombewa na machinga, bidaboda, wapita njia kwa miguu na magari.

Hapo hakuna tena sheria za traffic au vibali vya biashara au sheria za afya.

Vyote vilikula ganzi aliyoinjikwa na Magufuli.
Wanyonge wasibugudhiwe.

Matokeo yake mji kama DSM , uchafu, kinyesi, takataka na hata magonjwa ya matumbo yameongezeka.
Ajali ndio usiseme, boda boda wanajiendea wapendavyo.

Sasa baada ya ajali dhahiri ya Kariakoo na moto wa soko la Kariakoo, taratibu ganzi imeanza kuiachia serikali.

Sasa serikali inagundua kuwa kuna Roadway Ordinance Act, kuna Road Traffic Act, kuna sheria za Mipango Miji na Afya.
Na serikali vile vile wameanza kukumbushwa juu ya Sheria za Biashara.

Wasi wasi wangu ni kama ganzi iliyopigwa na Mwendazake kwa vyombo vya dola itatoka kikamilifu ili miji ijiendedhe kistaarabu kama Awamu zilizotangulia au hilo ganzi kuwendelea karibu na uchaguzi.
JamiiForums754916659.jpg
 
Kama Arusha ile barabara ya kuelekea Krokoni kutokea mataa yote ilikua imechukuliwa na machinga nyanya zinatandikwa hadi barabarani
 
Ukweli yule angeweza kuishi muda mrefu naona Tz sifa kubwa ingikuwa umaskini na unyonge ukionekana unakaa nyumba nzuri na unavihela basi wewe utakuwa FISADI au sio MZALENDO kwahiyo lazima wakutupe LUPANGO utakaa humu hadi ufe.
 
Ukweli yule angeweza kuishi muda mrefu naona Tz sifa kubwa ingikuwa umaskini na unyonge ukionekana unakaa nyumba nzuri na unavihela basi wewe utakuwa FISADI au sio MZALENDO kwahiyo lazima wakutupe LUPANGO utakaa humu hadi ufe.
Ukweli lazima usemwe, waliwaita watu wanyonge si kuwassidia bali kuwatumia kisiasa.
 
Back
Top Bottom