Tatizo la macho kuwasha

Tatizo la macho kuwasha

Joined
May 8, 2014
Posts
73
Reaction score
10
Habari wanaJF,

Kwa muda mrefu nimekuwa nikisumbuliwa na macho huwa macho yananiwasha sana ambapo kwa sasa hali imekuwa mbaya najua walioko humu jukwaani wanaweza kunipa ushauri niende hospitali kupima au kuna dawa mbadala. Pia endapo nitatumia miwani huwa inauzwaje?

Ahsanteni.
 
Hiyo ni aleji ndugu haina dawa, tafuta tu ni kitu gani kinachokusababishia aleji hiyo ukiepuke.Hilo tatizo liliwahi kunisumbua sana miaka fulani likaja kuisha lenyewe baada ya kubadilisha mazingira.
 
mimi mwenyewe kila nikinywa pombe macho yanawasha mpaka masikio na ninapiga chafya sana ila nisipokunywa nakua safi kabisa
 
dawa ya asili.chemsha majani ya chai yapoe kisha unawe uso.kula kisamvu kwa wingi yaan kula kibakuli kila siku.
 
Tumia levokabastinhydrochloride eyedrops na kula certizin 10mg tablets zitakusaidia kupunguza muwasho wa macho.Lakini kama alivyosema mdau hapo juu huo ni uzio ni vyema ukijua chanzo cha uzio na kuepuka!
 
Tumia levokabastinhydrochloride eyedrops na kula certizin 10mg tablets zitakusaidia kupunguza muwasho wa macho.Lakini kama alivyosema mdau hapo juu huo ni uzio ni vyema ukijua chanzo cha uzio na kuepuka!

Mzio not uzio
 
nenda kcmc kamwone optometrist atakusaidia,bt iyo inaweza kua allergic conjuctivitis
 
kitu gani kingine cha tofauti umekigundua kwenye macho yako.. je yanavimba, yana badirika rangi, unapata shida ktk kuona..?
 
Huo ni ugonjwa wa RED EYES zipo dawa madukani
 
ooohh angalia mazingira unayokaa .hasa sehemu unayolala..mara nyingi inakuwa kama shuka au blanket unalotumia linakuwa na ukungu ndo unasababisha hvo.au vumbi la chumbani kwako...lakin vilevile huenda unalala karibu na kabati la nguo lenye nguo zilizokaa humo muda mrefu zinzkuwa na ukungu mzito sana ..so nahisi ndo inasababisha kuwashwa macho... lakini vilevile angalia aina ya manukato unayotumia..baadhi ya bodrsprays au perfume huenda ndio zinakuletea hali hyo
 
kitu gani kingine cha tofauti umekigundua kwenye macho yako.. je yanavimba, yana badirika rangi, unapata shida ktk kuona..?



Mkuu sipati shida kwenye kuona ila huwa yakiwasha yanavimba na nikiangali mwanga kama tv au simu yanatoa machozi.
 
Write your reply...
ulipona?
maana na mke wangu ashaanza hili tatizo
 
Back
Top Bottom