Tatizo la maji limetatuliwa, la umeme litakwisha karibuni na miradi mingine yote inakamilishwa. Watanzania tuunge mkono juhudi za serikali yetu

Tatizo la maji limetatuliwa, la umeme litakwisha karibuni na miradi mingine yote inakamilishwa. Watanzania tuunge mkono juhudi za serikali yetu

Tuanze utaratibu wa kuhifadhi maji kuanzia ngazi ya familia. Pia idara za maji zianze utaratibu wa kuchimba mabwawa ya kuhifadhi maji ya mvua. Hii itasaidia wakati wa ukame
 
..tatizo la UKOSEFU WA AJIRA mtalitatua kwa kiwango gani?
 
Tuanze utaratibu wa kuhifadhi maji kuanzia ngazi ya familia. Pia idara za maji zianze utaratibu wa kuchimba mabwawa ya kuhifadhi maji ya mvua. Hii itasaidia wakati wa ukame
Ni muhimu saana maramojatu katika hilo, pia kuanzia ngazi ya familia kuhakikisha tunapanda miti na kusaidia kuzuia uhalibifu wa vyanzo vya maji
 
..tatizo la UKOSEFU WA AJIRA mtalitatua kwa kiwango gani?
JokaKuu Mimi sio msemaji wa Serikali, lakini naziona jitihada za Serikali katika kuifungua Tanzania ili kupata wawekezaji wengi ili kuweza kutanua wigo wa ajira, miaka ya nyuma sekta binafs ilikuwa ina ajiri watu wengi sana, lakini hapa katikati kumekuwa tofauti, naona jitihada za Serikali kuhakikisha sekta binafsi inainuka tena.
 
Serikali ya awamu ya sita haijawahi kupumzika katika kutatua kero za Watanzania, tatizo la maji lililokuwa limetokea hivi karibuni hasa kwa Wakazi wa Dar Es Salaamu limetatuliwa kwa asilimia 100, tatizo la mgao wa umeme liko mwishoni kuwa historia, kila kitu kinahitaji muda na fedha.

Watanzania tuendelee kuunga mkono Serikali ya awamu ya Sita, miradi yote ya maendeleo iiliyopangwa kutekelezwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imeanza kutekelezwa, fedha zimeshapelekwa, miradi iliyokuwa imeanza kutekelezwa miaka ya nyuma hakuna mradi hata mmoja uliosimama.

Ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara za mwendo kasi, madaraja, vivuko, SGR, JNHPP, Ujenzi wa madarasa, ujenzi wa mabweni, ujenzi wa nyumba za Watumishi, Ujenzi wa majengo ya kiutawala, miradi ya kilimo etc.

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, iko kwa ajili ya Watanzania na ni ukweli usio pingika awamu hii hali ya Demokrasia ni ya juu kabisa, ndio maana kila mtu yuko huru kutoa maoni na akasikilizwa. Tatizo la vijana wengi wanaamini kutukana na kukosoa tu ndio kutoa maoni.

Tuipende Tanzania yetu, tuunge mkono juhudi za Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Mungu ibariki Tanzania.
Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Serikali haina uwezo wa kutatua hayo nayoyasema . Ni Mungu tu atunusuru na hii hari.
 
Seriakli ilikua haijui nini cha kufanya...

Ashukuriwe Mungu aliyeshusha na kuleta mvua...
 
Mkuu Nangu Nyau unachosema ndio Serikali ya awamu ya sita sasa inachokifanya ili hapo baadaye kusiwe na shida kama hizi, Serikali imeendelea kuwekeza mabilion ya fedha ili kutafuta chanzo mbadala na tofauti tofauti cha umeme, ndio maana unaona JNHPP inaendelea, kuna miradi ya gesi, jua , upepo inakuja, kikubwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali, uwekezaji mkubwa kama huo ni ngumu kukamilisha kwa miaka miwili ambapo Serikali ya awamu hii imekuwa madarakani

Serikali ya awamu hii ni mali ya CCM kama zilivyokuwa serikali nyingine zilizopita.
Kufail kwa awamu zilizopita na sasa ni failure ya CCM kama chama tawala.

Ugomvi wetu ni pale tunapoona Taifa letu kila siku toka uhuru linahangaika na vitu very basic ambavyo vilipaswa kufanyika nyuma huko lakini baadala yake kila awamu ikija inahangaika navyo wakati huu muda tulipaswa kufanya mambo mengine na kwenda mbele kwa speed zaidi.

Tunachokiona wengi wetu ni viongozi kukosa commitment na kujikita zaidi kwenye ufisadi aka "Dili" huku mifumo nayo ikijikita kuajili vijana "kamlete" wengi wao wakiwa incompetency matokeo yake tunashuhudia total failure kila mahala na speed ya kobe kuelekea maendeleo.

CCM ikubali kujikabidhi kwa wananchi ili iwe mali ya watu wote na kila mtu kupitia CCM aweze kupenya na kuwa kiongozi sio kujuana na hela.... Hapa utapata cream ya vijana na watu competent na commited wanaoweza kufanya kazi kwa bidii, uzalendo nk na Taifa kwenda mbele.
CCM ikubali sasa nyakati zimebadirika na kuruhusu Serikali ibaki kuwa serikali na mifumo yake ikijiongoza na system ibaki kuwa controller na kufanya check and balance kila mahala nyeti.
CCM ikubali kuruhusu mfumo wa vyama vingi kuwa free na watu kuvitumia hivyo vyama kuleta upinzani dhidi yake ili mwisho wa siku Taifa liweze kuongozwa na vyama tofauti vyenye watu tofauti wenye maono tofauti.

KAZI YETU SIO KUIUNGA MKONO SERIKALI, KUISIFIA NK, HAPANA, KAZI YETU NI KUHAKIKISHA SERIKALI INAFANYA KAZI YAKE KWA KUIAMBIA TENA KWA UKALI MAANA SISI RAIA TUNAFANYA KAZI KWA BIDII, TUNALIPA KODI NK, TUNAPOONA MCHEZO MCHEZO KWENYE JASHO NA KODI ZETU LAZIMA TUPIGE KELELE.
 
Seriakli ilikua haijui nini cha kufanya...

Ashukuriwe Mungu aliyeshusha na kuleta mvua...
Tuanze na sisi wenyewe.... Sio lazima kila kitu tusubiri serikali. Usafi wa mazingira yeti, ulinzi wa vyanzo by maji na rasilimali nyingine, malezi mema ya watoto wetu na wengine yatasaidia kuhakikisha tunapiga hatua kwenda kwenye maendeleo chanya
 
tatizo la maji lililokuwa limetokea hivi karibuni hasa kwa Wakazi wa Dar Es Salaamu limetatuliwa kwa asilimia 100, tatizo la mgao wa umeme liko mwishoni kuwa historia ........ ...
Tatizo la maji Dar es Salaam halikutatuliwa na serikali bali limetatuliwa na mvua kunyesha. Litaendelea kujirudia hadi Litakapotatuliwa na serikali mwaka 2025 kwa kukamilika kwa ujenzi wa bwawa la kidunda.

Hilo la mgao wa umeme rais kasema litaendelea hadi mwaka 2025 serikali itakapokamilisha ukarabati wa njia za usafirishaji umeme, mitambo ya uzalishaji umeme na kukamilika kwa kituo cha JNHPP. Hizo bla bla zingine za tanesco na wizara yake achana nazo. Fuata alichosema mkuu wa nchi.
 
Kamwe, Serikali ya ccm haijawahi na haitowahi kutatua tatizo la maji hapa Tanzania
 
Mvua isiponyesha tena mwakani tunaendelea nalo !!
 
JokaKuu Mimi sio msemaji wa Serikali, lakini naziona jitihada za Serikali katika kuifungua Tanzania ili kupata wawekezaji wengi ili kuweza kutanua wigo wa ajira, miaka ya nyuma sekta binafs ilikuwa ina ajiri watu wengi sana, lakini hapa katikati kumekuwa tofauti, naona jitihada za Serikali kuhakikisha sekta binafsi inainuka tena.

..mbona unapozungumzia suala la maji baada ya mvua kunyesha unazungumza kwa kujiamini kana kwamba ni msemaji wa serikali?

..kwanini ktk suala la UKOSEFU WA AJIRA unapatwa na ubaridi na kujihami kuwa sio msemaji wa serikali?

..Majibu yako yananipa mashaka kwamba serikali na CCM hawana mikakati yoyote ya kupambana ukosefu wa ajira hapa nchini.
 
Serikali ya awamu ya sita haijawahi kupumzika katika kutatua kero za Watanzania, tatizo la maji lililokuwa limetokea hivi karibuni hasa kwa Wakazi wa Dar Es Salaamu limetatuliwa kwa asilimia 100, tatizo la mgao wa umeme liko mwishoni kuwa historia, kila kitu kinahitaji muda na fedha.

Watanzania tuendelee kuunga mkono Serikali ya awamu ya Sita, miradi yote ya maendeleo iiliyopangwa kutekelezwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imeanza kutekelezwa, fedha zimeshapelekwa, miradi iliyokuwa imeanza kutekelezwa miaka ya nyuma hakuna mradi hata mmoja uliosimama.

Ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara za mwendo kasi, madaraja, vivuko, SGR, JNHPP, Ujenzi wa madarasa, ujenzi wa mabweni, ujenzi wa nyumba za Watumishi, Ujenzi wa majengo ya kiutawala, miradi ya kilimo etc.

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, iko kwa ajili ya Watanzania na ni ukweli usio pingika awamu hii hali ya Demokrasia ni ya juu kabisa, ndio maana kila mtu yuko huru kutoa maoni na akasikilizwa. Tatizo la vijana wengi wanaamini kutukana na kukosoa tu ndio kutoa maoni.

Tuipende Tanzania yetu, tuunge mkono juhudi za Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Mungu ibariki Tanzania.
Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Sio awamu ya 6 ni awamu ya 5 b
 
Tatizo la Maji limetatuliwa na Mvua zilizoanza kunyesha, wacha maneno mengi..
IMG-20221129-WA0013.jpg
 
Back
Top Bottom