A
Anonymous
Guest
Yahusu: Tatizo la Maji Machafu Dodoma - Area D, Mtaa wa Mganga/Mtawa
Habari,
Tunapenda kuwasilisha malalamiko kuhusu hali mbaya ya maji machafu yaliyotapakaa barabarani katika eneo la Dodoma - Area D, hasa mtaa wa Mganga/Mtawa karibu na zilipokuwa ofisi za Pembejeo.
Kwa sasa, kinyesi kimeenea barabarani, hali inayosababisha hofu kubwa ya magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, kuharisha, na hata kuongeza hatari ya maambukizi ya COVID-19.
Kwa zaidi ya miezi mitatu sasa, hakuna hatua yoyote dhahiri iliyoonekana kuchukuliwa na DUWASA ili kutatua tatizo hili. Mwanzo barabara zote zilikuwa na lami then tunaona mkandarasi aliyeteuliwa na DUWASA akifanya kazi ya kuweka miundombinu ya maji taka, lakini aliharibu barabara (hajatoa kifusi alichochimba kuweka miundombinu yake - matokeo ni maji kutuama kila mvua ikinyesha, Chamber zote ni mbovu pia zinakusanya maji kwenye mashimo yanayotokana na kifusi hicho kilichobaki) na miundombinu hiyo haifanyi kazi ipasavyo.
Matokeo yake ni kwamba kila siku maji machafu na kinyesi hutapakaa barabarani, jambo linaloathiri usalama wa kiafya wa wakazi wa eneo hili. Tunaambatanisha picha na video kuthibitisha ukubwa wa tatizo.
Tunatoa wito wa haraka kwa DUWASA na mamlaka husika kuchukua hatua stahiki ili kurekebisha miundombinu hiyo na kuhakikisha tatizo hili linatatuliwa mara moja.
Tunaamini kuwa hatua za dharura zitaepusha mlipuko wa magonjwa na kurejesha hali ya usafi katika eneo letu.
Tafadhali tunaomba uwajibikaji na suluhisho la kudumu kwa changamoto hii.
Wakazi wa Area D, Mganga/Mtawa
Coordinates: 6°10'00"S 35°45'39"
Or 6°10'00.0"S 35°45'39.0"E · -6.166667, 35.760833