Tatizo la Maji: Mto Ruvu hauna maji au ni matengenezo ya DAWASA?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Ni vema tukaelezwa Ukweli ili tujipangie Siku za kuoga

Tatizo ni nini hasa?

Ni matengenezo ya Pump za Dawasa au Mto Ruvu hauna Maji?!

Msema Ukweli ni mpenzi wa Mungu wa mbinguni!
 
Nakumbuka mwaka jana maji yalivyopungua mheshimiwa alituambia tunakata Sana miti. Mwaka huu mkuu wa mkoa alituambia CCM haijaleta ukame. Mwakani majira kama haya tutaambiwa tunaoga sana.
 
Kuna mafundi/ vifaa/ cranes na magari kibao ya dawasa, sehemu kama tatu kwenye barabara ya bagamoyo....huenda ndio maji yamepungua ila kuna kitu wanaficha kwa kisingizio cha ukame.
 
Tatizo ni watu wachache wa akili za kiwango na aina yako ndio wanahusika kusimamia wengine wengi kupata maji.
 
Mvua Hakuna

Wakulima wanakesha usiku kuchepusha maji

Wengine wanawaza kuuza maji Yaani ni tafran
 
Mbona na mwanza hakuna maji au nako ni mto Ruvu na dawasa[emoji706]
 
Nakumbuka mwaka jana maji yalivyopungua mheshimiwa alituambia tunakata Sana miti..mwaka huu mkuu wa mkoa alituambia CCM haijaleta ukame.mwakani majira kama haya tutaambiwa tunaoga sana
Mbona umesahau lile sakata tulielezwa Mchina alikuwa anamwagilia sana mashamba yake na alisimamishwa hizo shughuli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…