Tatizo la Majina ya Kiislam Katika Viya ya Maji Maji 1905 - 1907

Tatizo la Majina ya Kiislam Katika Viya ya Maji Maji 1905 - 1907

TATIZO LA MAJINA YA KIISLAM KATIKA HISTORIA YA VITA VYA MAJI MAJI

Ukisoma historia ya Vita Vya Maji Maji utakutana na jina Mkomanile.

Linaandikwa jina moja tu, ''Mkomanile.''

Kwa nini liandikwe jina moja tu?

Huyu ndiye mwanamke pekee katika majina karibu 67 ya mashujaa wa Vita Vya Maji Maji aliyenyongwa na kuzikwa katika kaburi la halaiki Mahenge Songea.

Huyu mwanamke jina lake ni Khadija Mkomanile.
Kwa nini jina la Khadija halikuandikwa?

Tuseme hawakulijua?

Ukisoma historia ya Maji Maji utasoma jina Chinyalanyala jina moja tu.

Kwa nini liandikwe jina moja tu?

Jina lake ni Omar Chinyalanyala.
Inawezekana kuwa jina la Omar hawakuifahamu?

Ukisoma historia ya Vita Vya Maji maji utasoma jina la Songea Mbano.

Hapa unasoma majina mawili jina moja halikutajwa.

Kwa nini jina lake la kwanza halikuandikwa lifahamike?
Huyu jina lake lake la kwanza ni Abdulraufu.

Hili jina Abdulraufu hawakulijua?
Kuna ''Kazembe'' lakini jina lakini la kwanza halipo.

Haya yanashangaza sana.

Kipande hicho hapo chini kinatoka katika kitabu cha Abdul Sykes:

''Kuelewa hali ya Uislam wakati ule, unahitaji kusoma barua iliyoandikwa na Chifu Songea bin Ruuf wakati alipokuwa akikusanya nguvu za raia wake dhidi ya majeshi ya Wajerumani na huku akijaribu kupata ushirika wa machifu wengine katika sehemu za kusini ya Tanganyika na ng'ambo ya Mto Ruvuma katika Msumbiji.

Barua hii aliyoandikiwa Sheikh, Sultan Mataka bin Hamin Massaninga anaandika (barua hii ipo katika herufi za Kiarabu):

Sultan Songea bin Ruuf anasema:

''Kwa Sheikh Sultan Mataka bin Hamin Massaninga.
Asalaam Aleikum,

Ninakuletea barua kupitia Kazembe.

Tumepata amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa Wazungu lazima waondoke nchini.

Tupo katika kupigananao hapa.

Naamini tumeshapatana muda mrefu, (kwa hiyo) niletee wanao, ili tufanye ushirikiano.

Nilitaka kukuletea mifugo kama zawadi, lakini sipo katika hali ya kuweza kufanya hivyo, kwa kuwa vita ambavyo Mwenyezi Mungu amevitaka vinaendelea.

Niletee watumiaji bunduki mia moja, na niunge mkono katika kulivamia Boma (Songea).

Ninakuletea chupa ya Mtume Muhammad, ambayo ndani yake ipo nguvu ya kuwashinda Wazungu.

Usiwe na shaka nayo, ina uwezo mkubwa.

Tutakapoliteka Boma (Songea), tutakwenda kwenye vituo katika Nyasa pamoja, mimi na wewe.

Hivi sasa tusahau ugomvi wetu wa zamani.

Chupa hii, na dawa, imeletwa na Chinyalanyala mwenyewe, kiongozi wa vita.

Ameleta vilevile kombe, na anakupa salamu nyingi.

Endapo watu wako watakuja, Chinyalanyala mwenyewe atafika na atakupa vitu vingi vilivyo vitukufu.

Hassan bin Ismail anakusalimu.
Salam nyingi,

Sultan Songea bin Ruuf.''

Msikilize Mwalimu Hussein Bashir mwandishi wa vitabu kadhaa vya historia akizungumza:

Hata Uislamu ni dini ya kigeni Africa.
 
Uislam na uganga ni vitu viwili tafauti,Waganga wanaweza kuwa Waislam lakini Uislam sio Uganga na ndio maana utaona hakuna utowaji wa mashetani(mapepo) kwenye misikiti..

Tunashuhudia kila siku utowaji wa mapepo na majini kwenye Makanisa lakini mambo hayo hatuyaoni kwenye Misikiti
Lakini mapepo na majini ni ndugu wa waislam. Je unaweza mfukuza nduguyako?
 
Lakini mapepo na majini ni ndugu wa waislam. Je unaweza mfukuza nduguyako?
Hamna kitu kama hicho katika uislam,mapepo,waislam wanawaita mashetani na majini ni adui mkubwa wa Uislam..

Muislam anatakiwa amlaani shetani kabla ya kufanya kitu chochote kile,kwa kusema "audhu bilahi minal sheitan rajim"..

Propaganda za kuutia ubaya Uislam ndio iliyokifanya wewe uandike hayo..

Je katika dini yako kuna sehemu yoyote inayokufundisha wewe kumlaani Shetani?
 
Wewe uliyatoa wapi hayo majina mengine ambayo unafikiri ndio makamilifu na sahihi??
 
Hayo majina ya Kiarabu yanaongeza nini katika historia Yetu au yanasaidia nini katika maisha yako? Ila bado hujachelewa unaweza ukaandika vitabu vyako vya historia kwa muktadha unaoupenda wewe. Kiukweli hizi dini zimetujaza ujinga wa kutweza asili yetu na kutukuza vya wageni.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Mini...
Majina kama majina hayana maana yoyote mpaka ujue historia za wenye majina hayo.

Nakuwekea majina na historia ya wenye hayo majina.

Kleist Abdallah Sykes, Mzee bin Sudi, Suleiman Majisu, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Ibrahim Hamisi, Rawson Watts, Cecil Matola na Raikes Kusi.

Hawa ni waasisi wa African Association 1929.

Hii ndiyo historia ya hao wenye majina hayo.

AA ikawa TAA na ikawa TANU 1954.

Abdulwahid Kleist Sykes, Hamza Mwapachu, Sheikh Hassan bin Ameir (Mufti wa Tanganyika), Sheikh Said Chaurembo, Vedasto Kyaruzi, John Rupia na Steven Mhando.

Hawa walikuwa wajumbe wa TAA Political Subcommittee 1950.

Hii ndiyo historia yao.

Mkutano wa kwanza wa TANU August, 1954 ulihudhuriwa na hao hapo chini:

Julius Nyerere, Denis Phombeah, John Rupia, Frederick Njiliwa, Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mohamed Mtamila, Rajabu Diwani, Schneider Abdillah Plantan, Marsha Bilali, Rashid Ally Meli, Iddi Faiz Mafongo, Iddi Tulio, na wengineo watu hawakuzidi 20.

Hii ndiyo historia ya wenye majina hayo.

Angalia picha hiyo hapo chini ya Baraza la Wazee wa TANU mwaka wa 1954 na majina ya wajumbe wake:

1661618815992.jpeg


Nadhani umeelewa maana ya majina katika historia na ikiwa itakuwapo njama ya kufuta majina haya kwa namna yeyote ile historia itakuwa imevurugwa.
 
Back
Top Bottom