Kuna hili tatizo la mdomo kusogea pembeni ambalo humpata mtu akiwa na umri mkubwa kubisa.
Kuna watu wawili ambao nawafahamu vizuri tu wamewahi kukutwa na hiya hali, kimtaa hakuna jibu nimeweza kulipata zaidi ya kuwa wamerogwa/wametupiwa majini. Wakuu naombeni majawabu kwenye hili.
Kwa kukazia: huyo mmoja kati ya wawili ni mdada alikuwa mzuri balaa tumepotezana kama miezi mitatu hivi kuja kumwona nimemshangaa.
Hiyo hali ya mdomo kusogea pembeni (kitaalamu huitwa Facial nerve paralysis/Bell's Palsy) husababishwa na matatizo ya mishipa ya fahamu ya uso/mdomo (facial nerve) ambayo husimamia na kuendesha utendaji kazi wa misuli ya uso/mdomo.
Mishipa ya fahamu ya uso (facial nerve) ziko za aina mbili: ya upande wa kushoto na wa kulia.
Uimara wa mishipa hizo zote (kushoto na kulia) ndiyo hufanya uso/mdomo wako kuwa katika nafasi na muonekano wake wa kawaida.
Kutokana na hitilafu, kuharibika au maambukizi katika mishipa hiyo ya fahamu ya uso (facial nerve paralysis) misuli inayosimamiwa na kuendeshwa na mishipa hiyo huwa midhaifu/hushindwa kufanya kazi yake hivyo mdomo/uso kusogea pembeni/upande mmoja.
Kukiwa na athari (hitilafu, uharibifu, maambukizi, kupooza) kwenye mshipa wa fahamu wa uso/mdomo (facial nerve) ya upande mfano wa kushoto basi misuli ya upande huo huwa midhaifu au hushindwa kufanya kazi na huvutwa na misuli ya upande wa kulia ambayo iko imara, hivyo mdomo huhamia/husogelea upande wa kulia. Vivyo hivyo kama mshipa wa upande wa kulia ukiwa na hitilafu mdomo huelekea kushoto.
Pia jicho la upande husika haliwezi kufumbwa kisawasawa, yaani mtu akifumba macho jicho moja hubaki wazi.
Hali hii (facial nerve paralysis/Bell's Palsy) husababishwa na vitu mbalimbali mfano:
-maambukizi ya aina fulani ambayo hushambulia mishipa hiyo ya fahamu: bacteria, virusi kama HSV nk
-Ajali au kuumia uso ambapo mishipa hiyo huweza kukatika
-maambukizi kwenye masikio (otitis media)
-uvimbe kwenye masikio, uso au ubongo ambao hugandamiza mishipa hiyo ya fahamu ya uso
-kiharusi (stroke)
-kisukari nk
Kwa hiyo hivyo ndivyo hali hiyo inavyotokea.