Tatizo la miguu kuwaka moto (neuropathy): Ushauri, Kinga na Tiba

Huu ushauri umeshiba ndio maana naipenda jf.pengine ushauri kama huu ili uupate pesa lazima ikutoke

unapendekeza hospitali gani na gani ambapo wataalamu wa hivyo vipimo wanapatikana
Nadhani vipimo hivi naweza kupata hospital ya Rufaa ya Kanda Mbeya
 
Bahati mbaya sana hata Neurologists nchi hii ni wachache tena unakuta hospital kubwa aliyepo ana Bsc.Neurology pekee hata vifaa vya kupimia tu hakuna zaidi ya yeye kukuchomachoma visindano huko unyayoni.

Hizo ni dalili za Peripheral Neuropathy,ukishajua kisababishi (Nerve damage,Vitamin B deficiency,Diabetes, Inheritance au una HIV etc) watakuanzishia matibabu
jitahidi ufike hospital kubwa like MNH walau watafanya hata Nerve conduction Test (NCT)

Hizo dalili zitaendelea kuwa severe kadri muda unavyokwenda, jitahidi ufanye zoezi la hivyo viungo.

Ukiangukia kwa waganga wa kienyeji ndo umepotea mazima.
 
Punguza mawazo mkuu
 
hata mimi nasumbuliwa na hili tatizo. langu linaongezeka na kifua kuuma
 
Bahati mbaya sana hata Neurologists nchi hii ni wachache tena unakuta hospital kubwa aliyepo ana Bsc.Neurology pekee hata vifaa vya kupimia tu hakuna zaidi ya yeye kukuchomachoma visindano huko unyayoni...
HVI! Duuh!
 
Mdogo wangu na dada yangu walipata hli tatizo, yani mdogo wangu ilikuwa analia usiku kucha, ila walikuja kutumia neurobics zikawasaidia na leo wako sawa ila kipindi cha baridi ni mwendo wa kuvaa soksi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…