Tatizo la msingi la CHADEMA ni kudahili wanachama wala rushwa

meningitis

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Posts
8,425
Reaction score
4,768
Tulipokuwa tunapinga lowassa asipokelewe CHADEMA kimagumashi kama ilivyofanyika tuliona mbali sana.

Tulichokuwa tunakipinga ni kurasimisha usanii ,ulaghai na ulaji rushwa.

Labda kwa wale waliokuwa hawajabalehe katika siasa hasa kuanzia 2010 ni vyema wakatambua kuwa hapo kabla CHADEMA chini ya Dr Slaa kama katibu walianzisha harakati za kimkakati za kusaka wanachama kutoka kwenye jamii ya wasio wanachama wa vyama vingine vya siasa.

mkakati huu ulikuwa mzuri na ulijengwa na hoja kuu ya kwamba CCM ni mafisadi na wala rushwa.

mkakati huu uliifanya CHADEMA kupendwa na kuungwa mkono na wengi mimi nikiwemo.

Mwaka 2015 baada ya gia ya angani kuwekwa tulishuhudia mafisadi ya CCM yakihamia CHADEMA na kupewa nafasi za kugombea uongozi katika level mbalimbali kuanzia Urais hadi uenyekiti wa kitongoji.

Hakukuwa na scrutiny yoyote zaidi ya kuhongana na uongozi wa CHADEMA kushindwa kusimamia principles za chama.

Matokeo yake wezi,wahalifu,mafisadi na wala rushwa wote waliofurushwa CCM wakavaa joho jeupe lenye kola nyekundu na kugeuzwa kuwa wagombea huku wafia chama mithili ya Dr Slaa wakidhihakiwa na kuitwa wasaliti waliopewa rushwa na CCM.

Leo hii wezi,wala rushwa na wahalifu waliokuwa CCM wanapoamua kurudi walipotoka Ndio kina Nassari na lema wanakuja kutulilia tena ...This is pathetic!!

Mlifungia majini kwenye chupa sasa yanatoka mnaturudia sisi wananchi??

Poleni sana na mmechelewa ni bora tubaki na chama chenye mafisadi na waadilifu ambacho kikiamua kinaweza kuwashughulikia mafisadi.

Leo hii Mnyeti na Gambo wakihamia CHADEMA tutaambiwa wamekiri na waneingoka...wakiondoka tena mtasema wamehongwa ...huo mchezo wenu wa kitoto umefika mwisho ...pambaneni na hali yenu.

Haitasaidia kutulalamikia na kutuobesha bongo movies za 2008...mnachotakiwa kukifanya ni kusafisha panya wote mliowakaribisha chumbani mkianza na panya buku !

Mada hii ni kwa ajili ya CHADEMA asili
 
Je Chadema ina dhamira ya kweli ya kurudi kwenye misingi hasa ile ya kupambana na ufisadi?
 
Tulipokuwa tunapinga lowassa asipokelewe CHADEMA kimagumashi kama ilivyofanyika tuliona mbali sana.

Tulichokuwa tunakipinga ni kurasimisha usanii ,ulaghai na ulaji rushwa.
Unahalalisha rushwa kwa kujificha kwa kina slaa.
Labda kwa wale waliokuwa hawajabalehe katika siasa hasa kuanzia 2010 ni vyema wakatambua kuwa hapo kabla CHADEMA chini ya Dr Slaa kama katibu walianzisha harakati za kimkakati za kusaka wanachama kutoka kwenye jamii ya wasio wanachama wa vyama vingine vya siasa.

mkakati huu ulikuwa mzuri na ulijengwa na hoja kuu ya kwamba CCM ni mafisadi na wala rushwa.

mkakati huu uliifanya CHADEMA kupendwa na kuungwa mkono na wengi mimi nikiwemo.

Mwaka 2015 baada ya gia ya angani kuwekwa tulishuhudia mafisadi ya CCM yakihamia CHADEMA na kupewa nafasi za kugombea uongozi katika level mbalimbali kuanzia Urais hadi uenyekiti wa kitongoji.

Hakukuwa na scrutiny yoyote zaidi ya kuhongana na uongozi wa CHADEMA kushindwa kusimamia principles za chama.

Matokeo yake wezi,wahalifu,mafisadi na wala rushwa wote waliofurushwa CCM wakavaa joho jeupe lenye kola nyekundu na kugeuzwa kuwa wagombea huku wafia chama mithili ya Dr Slaa wakidhihakiwa na kuitwa wasaliti waliopewa rushwa na CCM.

Leo hii wezi,wala rushwa na wahalifu waliokuwa CCM wanapoamua kurudi walipotoka Ndio kina Nassari na lema wanakuja kutulilia tena ...This is pathetic!!

Mlifungia majini kwenye chupa sasa yanatoka mnaturudia sisi wananchi??

Poleni sana na mmechelewa ni bora tubaki na chama chenye mafisadi na waadilifu ambacho kikiamua kinaweza kuwashughulikia mafisadi.

Leo hii Mnyeti na Gambo wakihamia CHADEMA tutaambiwa wamekiri na waneingoka...wakiondoka tena mtasema wamehongwa ...huo mchezo wenu wa kitoto umefika mwisho ...pambaneni na hali yenu.

Haitasaidia kutulalamikia na kutuobesha bongo movies za 2008...mnachotakiwa kukifanya ni kusafisha panya wote mliowakaribisha chumbani mkianza na panya buku !

Mada hii ni kwa ajili ya CHADEMA asili[/QUOTE
Mmnyeti mwenyewe keshakir kuwa alitoa rushwa wewe naona unawashwa washwa
Je si kweli kwamba mh raisi alibariki kutolewa kwa bl 6 kuratibu mipango hii nchi nzima?
Je si kweli kwamba huu ni mwendelezo wa kukihujumu chama mnachoita kilaiku kimekufa.
Je si kweli kwamba raisi alipokuwa arusha alienda monduli kuzima uasi wa wanajeshi waliomgomea kuchanganya shughuli yao na siasa za kina gambo?
Je sio kweli kwamba mh. Raisi haungwi mkono jeshini na ndo maana akawaita kina mahita ili kuweka mambo sawa?
 
Mleta mada endelea kujijibu mwenyewe
teh teh. Mkuu unategemea mwanamke aliyetolewa kwa mume na kuolewa na mwingine,siku mwingine akiolewa kwa style yake atamlaumu nani zaidi ya mume. Eti mke wa mtu anadai mumewe hajui mapenzi, kwa hiyo alipokutana na huyo akajua ndie anajua.Jiulize alijuaje kabla ya kuzini?.Ila ukiwa na kijiji chenye nusu watu km huyo mwanamke unategemea uzinzi ukawa haramu? CCM hawajui uimara wa chadema ni kwa vile ccm imewasaidia kuchuja wadhaifu wote na kuondoka nao.Mwishowe ccm inakuwa inapimwa kwa wingi wa vilaza.
 
1. Matokeo yake wezi,wahalifu,mafisadi na wala rushwa wote waliofurushwa CCM wakavaa joho jeupe lenye kola nyekundu na kugeuzwa kuwa wagombea huku wafia chama mithili ya Dr Slaa wakidhihakiwa na kuitwa wasaliti waliopewa rushwa na CCM.

Mkuu Menigitis, hapo umekiri wazi kuwa wezi, wahalifu, mafisadi na wala rushwa wako CCM; sasa sijui ni kwa nini usiunganishe nguvu tupambane nao? Kujua ugonjwa au tatizo ni 50% ya tiba.

2. Leo hii wezi,wala rushwa na wahalifu waliokuwa CCM wanapoamua kurudi walipotoka Ndio kina Nassari na lema wanakuja kutulilia tena ...This is pathetic!!

Sijaelewa vizuri tatizo lako kwa walichofanya jana akina Joshua Nassari ni lipi hapo.

Je una maana kwa vile wale madiwani waliohongwa na CCM na kuachia nafasi zao wangeachwa kimya kimya bila chanzo cha matukio yale kuchunguzwa? Au je ulitaka baada ya uchunguzi kukamilika akina Nassari wakae kimya tu kwa vile wala rushwa wamerejea zizini kwao (CCM)?

3. Mada hii ni kwa ajili ya CHADEMA asili
Pia sijawahi kusikia kusajiliwa au kuwepo kwa hicho chama.

Vipi hapo unalenga kujenga au kubomoa mkuu?

Bila shaka CHADEMA kina madhaifu mengi, vyama vya upinzani vina madhaifu mengi tu LAKINI ukijumlisha udhaifu wote wa vyama vyote vya upinzani haufiki 10% ya udhaifu wa CCM. Udhaifu wa CCM ni mkubwa na ndio sababu ya udumavu uliopo Tanzania iwe ni kiuchumi, kisiasa, kielimu, kiafya nk nk
 
Je Chadema ina dhamira ya kweli ya kurudi kwenye misingi hasa ile ya kupambana na ufisadi?

Naiamini sana CHADEMA,yawezekana viongozi walidhani kwa njia hiyo ni sahihi,tunajifunza na makosa,hope wamejifunza tunaenda mbele.

Pili aliyemleta Lowassa si Mbowe bali ni Dr.Slaa,nenda kasikilize ile hotuba yake aliyoitoa mara ya kwanza aliposema sababu za kuondoka.ALikubali kwamba yeye ndiye aliyemleta Lowassa,amemeleta mgeni halafu akamkimbia mgeni hivyo hata Dr.Slaa si wa kumwamini pia.
 
Chadema mlifanya kosa kubwa sana kumsafisha lowasa mbele ya watanzania wanafki ninaowajua mimi..penye unafki kuna uerevu.na sasa mtavuna mlichopanda maana hakuna namna
 
teh teh. Mkuu unategemea mwanamke aliyetolewa kwa mume na kuolewa na mwingine,siku mwingine akiolewa kwa style yake atamlaumu nani zaidi ya mume. Eti mke wa mtu anadai mumewe hajui mapenzi, kwa hiyo alipokutana na huyo akajua ndie anajua.Jiulize alijuaje kabla ya kuzini?.Ila ukiwa na kijiji chenye nusu watu km huyo mwanamke unategemea uzinzi ukawa haramu? CCM hawajui uimara wa chadema ni kwa vile ccm imewasaidia kuchuja wadhaifu wote na kuondoka nao.Mwishowe ccm inakuwa inapimwa kwa wingi wa vilaza.
Wewe ndio panya wenywe waliongia ingia chadema wakiwa na panya buku?
 
Uzi ushadoda tupia kavideo kama Nasari kuchangamsha uzi
 
Chadema mlifanya kosa kubwa sana kumsafisha lowasa mbele ya watanzania wanafki ninaowajua mimi..penye unafki kuna uerevu.na sasa mtavuna mlichopanda maana hakuna namna
Ni km walivyosema wenzio kuwa ni kosa kubwa sana barca kumsajili suarez baada ya world cup. Lowasa kapunguza sana chadema kuvamiwa na wasiojulikana kipindi kizima cha uchaguzi. CCM hawakuwa tayari kupangua timu yao ya mazombi. Endeleeni kurudiarudia ujinga km kasuku.
 
Chadema mlifanya kosa kubwa sana kumsafisha lowasa mbele ya watanzania wanafki ninaowajua mimi..penye unafki kuna uerevu.na sasa mtavuna mlichopanda maana hakuna namna
Kuliko kitila mkumbo, Lipumba,Dr Slaa etc?
 
Back
Top Bottom