Tatizo la msingi la CHADEMA ni kudahili wanachama wala rushwa

Panya Buku wa Lumumba naona mnahaha kututoa kwenye kashfa ya Arusha..

Hamchomoki kenge nyie
 
Chadema mlifanya kosa kubwa sana kumsafisha lowasa mbele ya watanzania wanafki ninaowajua mimi..penye unafki kuna uerevu.na sasa mtavuna mlichopanda maana hakuna namna
Tupo Arusha sasa hivi panya nyie....

Mnadhani mtatutoa kwenye reli.....
 
Mkuu umesoma vizuri mada yangu?
Nimeanzia kwa ufupi kwenye historia ya kilichofanywa jana.

Kilichofanyika jana kilikuwa kinafanywa kwa ufanisi enzi zile za chadema asili...

Baadaye wakajitia najisi kwa kupokea majizi(kwa sauti ya lissu)

Wapo tuliopinga hiyo najisi kabla,wakati inafanyika na hadi leo na siku zijazo.

Ili kuondoa najisi hiyo ni shurti panya waondolewe bila kujali ukubwa au udogo wao...na nikiongelea panya namaanisha hata panya buku waliochukuliwa na chadema.

Kwa kufanya hivyo panya wote nchini watakosa mahala pa kukimbilia na watabaki mtaani hasi kifo chao kitapowakuta.

Kama Chadema imeamua kurejea kwenye misingi ile ya zamani basi isichague kupambana na panya wanaofueukuta na kuhama nyumba moja kwenda nyingine bali ipambane na yoyote yule mwenye tabia ya upanya.

Chadema ikifanya hivyo basi CCM na vyama vingine vitafanya hivyo na hatima yake nchi itaondokona na panya.
 
Ni kweli mleta uzi kitendo cha cdm kuwakubali hao wanachama toka ccm ni kosa kubwa la kiufundi kwani walijifunza kosa kwa Shibuda. Ila inaonekana cdm hawakijufunza kwenye kosa lile na sasa ndio wakalirudia zaidi kiasi kwamba kwenye uwanja wa propaganda wamepigwa bao.

Pamoja na udhaifu/kosa hilo la cdm hiyo haihalalishi ccm wawarudishe wanachama wake kwa rushwa. Sasa hapa tunachoona ni ccm inayatoa rushwa kupitia serekali na cdm inayopokea rushwa kupitia madiwani wanaohama. Je katika mazingira haya rais anaweza kusimama hadharani akasema anapambana na rushwa?
 
Mtoa mada uliko vurunda ni kutuambia "bora tubaki na wezi". Kama kweli unauchungu na Nchi hii,unapaswa kukemea na kulaani rushwa kwenye siasa za Tanzania. Majizi yaliyoko ccm yatemwe. Nilidhani utasema hao madiwani wala rushwa watemwe na kufungwa.kumbe na wewe ni walewale.
 

Mkuu, kama wewe ni muumini wa mifumo, utakuwa katika njia sahihi. Lakini kama wewe ni muumini wa watu, utayumbishwa sana. Kama unaona Dr. Slaa pekee ndio rejea ya mafanikio ya CHADEMA, ukumbuke pia wapo walioamini Lipumba ndio rejea ya mafanikio ya CUF. Ukimfuata mtu, ipo siku atabadilika halafu utabaki njia panda. Hebu fikiria waliokuwa waumini wa Lipumba, leo wako katika hali gani kimaamuzi? Anafukuza wabunge wa chama chake!

Ukisimamia mfumo, yeyote anayetaka kuungana nawe wala hutapata shida kumkaribisha. Umpokee lakini atafuata mstari wa mfumo. Kama chama kinakataa wanacchama wapya kwa kisingizio 'walikuwa wala rushwa', basi ina maana itafika mahali unaweza kushindwa kuongeza idadi ya wapiga kura wako. Siasa ni upepo na karata, haina principle maalum. Nani alijua leo Nape ataziponda Bomberdier? Usikariri watu, kariri mfumo!
 
Swali lako hapo chini ni la msingi sana!
Ingawa Hata Rais aweza kuamua kukaa kimya kwa kuwa shutuma kwa CCM ni zile zile ..
alipokuja kwa style ya kuwabadilikia watoa na wala Rushwa tulimbeza na tukaanza kuwatetea mafisadi.

Ndio maana nikaja na swali la msingi je ni kweli Chadema ina taka kuirejea vita hiyo?

Je Chadema ipo tayari kubeba gharama ya vita hiyo?

Moja ya gharama ya vita hiyo kwa Chadema ni kuondoa wote walioingia wakiwa na madoa ya ufisadi wakianza na yule fisadi kuu waliomtaja kwenye famous list of Shame ,kumbuka aliambatana na panya wengi ambao leo hii tunawalalamikia kurudi CCM.
 
njaa kali hata wa ccm wakipewa watapokea
 
Tofauti yangu mimi na wewe ni hapo unapotaka kutuaminisha kuwa siasa ni karata...Ni kosa kubwa alilolifanya mwenyekitu na linaigharimu chadema hadi leo.

Kama unaamini katika Siasa ni karata basi waache CCM wachezi karata zao...yaani waendelee kuhinga wanaohongeka na hakuna haja ya kutoa kilio....
 
... Kama unaamini katika Siasa ni karata basi waache CCM wacheze karata zao...yaani waendelee kuhonga wanaohongeka na hakuna haja ya kutoa kilio....
Wapo waliohongeka na wapo waliocheza dili waonekane wamehongeka, na hawa ndio wanaofanya mjadala huu uwe moto. Hao wanaoweza kuhongeka kiukweli wapo pande zote Sema tu hajapatikana mtu wa CHADEMA kuwahonga madiwani wa CCM, lakini nakwambia matazamio ya madiwani wengi yamekuwa tofauti maana macho yamekuwa mengi na hakuna kujigawia zabuni, na wengi wanajuta kugombea udiwani kwani haulipi chochote zaidi ya hasara. Sasa akipatikana mtu wa kumuhonga diwani aachie ngazi kwa milioni 20, wengi wataachia tena yawezekana CCM wakawa wengi wao. Kuhongeka ni tabia (zilizochangia msukumo wa kugombea), na wala si chama
 
Wanadahili wala rushwa ili wawaumbue watoa rushwa
 

Kwahiyo unataka kusema rais ameona bora aendelee na rushwa kwani chama chake kimezoeleka kwa hilo na kwa kuwa cdm ipo na watuhumiwa wa rushwa na kinawatetea? Utetezi dhaifu.

Mimi sio kiongozi wala mwanachama wa cdm bali ni shabiki wake wa kutupwa, ila nijuavyo chama chochote kina mfumo wake wa nidhamu hivyo sijui ni hatua gani cdm kinawachukulia wanachama wenye tuhuma mbalimbali. Kama cdm wanataka kuirudia au kuiendeleza vita hiyo wanachama na viongozi wake ndio wenye jibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…