Tatizo la mtoto kutopenda kunyonya.

Tatizo la mtoto kutopenda kunyonya.

KANYAGWANDA

Member
Joined
Apr 16, 2023
Posts
21
Reaction score
56
Wakuu habari zenu.
Naomba ushauri.Mtoto wangu wa KIUME wa miezi minne anachangamoto ya kunyonya kwa shida sana.Mchana akiwa na njaa atalia sana akipewa ziwa ndo analia zaidi.Akiwekwa mgongoni baada ya muda akashushwa ananyoa kidogo then anapotezea.

Usiku akiamka toka usingizini ananyonya vizuri tu issue ni hiyo mchana yaan ni vita na mama yake.

Naomba ushauri wenu wataalamu.
 
Pole sana kwa changamoto unayopitia na mtoto wako. Kutonyonya vizuri mchana kunaweza kusababishwa na mambo kadhaa, kama vile usumbufu wa mazingira (kelele, mwanga mwingi), uchovu, au hata kipindi cha ukuaji (growth spurt) ambapo wanabadilika kitabia.
Jaribu haya:
✅ Tafuta mazingira tulivu – Punguza kelele na mwanga mwingi wakati wa kunyonyesha mchana.
✅ Mshike kwa njia tofauti – Wakati mwingine kubadilisha pozi la kunyonyesha husaidia.
✅ Mpatie muda – Usimlazimishe, badala yake jaribu mara kwa mara bila shinikizo.
✅ Mwangalie afya yake – Ikiwa anaendelea kukataa, hakikisha hana maambukizi ya masikio, mafua, au tatizo lingine la kiafya.
✅ Endelea kumpa usiku – Kwa kuwa usiku ananyonya vizuri, basi bado anapata maziwa anayohitaji
 
Asante sana kwa ushauri mkuu.
Nitajihidi kufanya hivyo.Sioni shida yeyote ya kiafya aliyonayo.Hapo kwenye makelele nadhani upo sahihi zaidi maan akiwa ananyonya akasikia kelele yeyote anashituka na kunyonya kunaishia hapo.
 
kama ishu ni kelele basi wakati wa kunyonya zima TV,Sabufa au feni na muache kuongea kwa sauti kwa muda..au labda joto linamsumbua kiasi anakosa raha
 
Yes hii njia nimeitumia naona imezaa matunda mkuu.Asante sana
 
Back
Top Bottom