Tatizo la Ng'ombe kujaa gesi tumboni

Gemini Are Forever

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2019
Posts
1,508
Reaction score
2,619
Wanajamvi, Salaam!

Nina ng'ombe wangu amejaa sana gesi tumboni yaani tumbo limetuna vibaya mno leo ni siku ya nne.

Msaada wenu wataalamu na wazoefu wa mifugo. Shida hiyo husababishwa na nini? Ni ugonjwa au? Nini suluhisho la kutatua hilo?

Karibuni.
 
Ushauri namba 1:
Ita daktari amshughulikie, usije ukampoteza.
Kutoka hapo ongea na daktari kiundani zaidi huku ukisubiri majibu yawafugaji wa jf

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulikuwa huna sababu ya kumjibu kama huna jibu. Kwani hajui kuna madaktari wa mifugo na hospitali za mifugo? ameamua kutumia njia hii ambayo kuna mtu labda ni daktari wa mifugo analifahamu tatizo hili na kumsaidia fasta, au akawepo mfugaji mwandamizi ambaye tatizohili hukabiliana nalo mara kwa mara kwa njia rahisi za kienyeji ama za kihospitali.
 
Philipo D. Ruzige said:
Ita daktari amshughulikie
Nipo mbali sana na madaktari na ndio maana nimekuja hapa JF kupata msaada wa haraka kwa wazoef wa humu jukwaani.
 
Mkuu watu husema ukimpa maji ukichanganya na magadi kama hakuna weka majivu kidogo hutoa gesi...
Sijui ukweli wake...

Tafuta namba za wataalam humu kuna nyuzi nyingi..

Pole na kila la heri!

Everyday is Saturday.......................... 😎
 
Bambushka said:
Mkuu watu husema ukimpa maji ukichanganya na magadi kama hakuna weka majivu kidogo hutoa gesi...
Sijui ukweli wake..

Tafuta namba za wataalamu humu kuna nyuzi nyingi.

Pole na kila la kheri.!
Asante kwa maoni ndugu, ntajaribu kufanya hvyo.
 
Chanzo ni nini mkuu au haufahamu chanzo ?
Wanachungia kwenye nyasi za aina gani?

Dawa.
1. kama tatizo ni kuvimbewa chukua tumbaku loweka kiasi kwenye maji kisha mnyweshe. Kama tatizo ni kuvimbewa litaisha ndani ya masaa matatu tu.

2. Kama uko maeneo ya mbugani tafuta mimea fulani wasukuma wanaita " MALEWE GA MBULI" loweka kiasi mnyweshe hiyo hali itaisha tu baada ya muda mfupi.

3. Wakati mwingine tatizo kama hili hutokea Ng'ombe aking'atwa na nyoka hasa Swila na hii jaribu kumchunguza vizuri kama hana sehemu inayoashiria uvimbe. Sumu ya swila huua taratibu kwa ngombe ila huchukua muda mrefu hata mwezi akiwa amejaa tumbo baadae ataanza kuoza sehemu aliyoshambuliwa.

4. kuna wakati mwingine majani fulani au wadudu fulani kwenye majani husababisha Ng'ombe kujaa tumbo japo ni hali ambayo baadae huwa inaisha.

5. Mwaka 2003 niliwahi kuona kisa kimoja cha ngombe kujaa tumbo kwa muda wa mwezi mzima baadae alikufa nilipomchuna nikagundua mwili mzima ulikuwa umejaa maji nilitumia dawa zaidi ya 3 za Oxtetracyclin lakini hazikutibu.

Ni hayo tu pole sana mkuu inaumiza sana kupoteza mfugo wako kwa ugonjwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
PTER said:
Chanzo ni nini mkuu? Au hufahamu chanzo? Wanachungia kwenye nyasi za aina gani?
Sijui chanzo mkuu na kuhusu majani hakuna majani maalumu kwa kweli coz wanachungwa kw uchunguji wa kiasili (wa masafa marefu kidogo).

Hii ni case ya pili kwa ng'ombe kupata tatizo kama hili. Miezi miwili iliyopita nilimpoteza ng'ombe wa mkubwa wa laki 5 kwa tatizo hili hili ambapo aliugua nikamchoma sindano za Oxytetracycline lakin hakupona, alikaa kam wiki 3 na ilikuwa anapata shda kutoa haja.. Baadae akaja kufa.
 
Ukitaka kuondoa iyo gesi mtoboe kwa juu upande wa kushoto wa tumbo then iyo gesi ita be released japo inahitaji uzoefu kidogo au pia unaweza tumia stomach tube kuingiza mdomoni Hadi tumboni,ila kiufupi tafuta mtalamu wa mifugo ng'ombe atakwenda na maji huyo pia epuka kuchunga ovyo kwenye magugu kwani huleta bloating kwa mifugo pia angalia chakula unacholisha

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Ukupaswa kumchoma OTC,iyo Ni bloating unataka kutoa ushuzi kwa sindano hii akili ya wapi mfugaji wewe.TUMIA MADAKITARI WA MIFUGO WACHA UBISHI!!!

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Hyperkid said:
Ukitaka kuondoa hiyo gesi tumboni mtoboe kwa juu upande wa kushoto

Asante sana kwa ushauri mkuu ila nitatoboa kwa kutumia nini?
 
Vinapatikana wap mkuu?
Kwenye maduka makubwa ya dawa na vifaa tiba kwa wanyama,nanikushauri hilo zoezi SI lakufanya wewe utaweza kumuuwa endapo utakosea,you have to know anatomy of ruminant animal ndipo utoboe kwani unaweza kukosea na usitoboe tumbo husika Kisha kutoboa other delicate organs na bada ya kutoboa puliza wound spry Kama alamycin or OTC kwenye kidonda

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Kwani kinyesi chake kiko vipi,uharo,au kigumu harufu yake jee ya kawaida au tofauti? ,Kama nkigumu mbadala wakukilainisha chukua SABUNI ya kipande tengeneza povu na weka kwenye kinyeo usiogope ingiza mkono kabisa Kisha pakaza SABUNI ya kipande iliyorojeka apoapo ushuzi utamtoka na gesi kupungua

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Mkuu hyperkid asante sana kwa ufafanuzi..

Kinyesi chake kilikuwa uharo kiasi kwa siku za kwanza ila baadae alikoma kabisa kutoa na kinyesi kilikuwa na harufu tofauti.
Mkuu labda nizudi kukuliza maswali kidogo juu ya icho kinyesi je kilikua na uteute,na damu damu na je vip kuhusu upumuaji wake ukitizama mbavu anapumua kwa nguvu Hadi kuona kupanda na kushuka kwa mbavu? Apa nakuliza ili niweze kujua Ni gonjwa gani hasa linamesumbua ndipo nikwambie dawa gani ununue

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Pia nikuombe Kama unaweza kupima joto nakunipa kwa kesho,apa unachukua clinical thermometer unainyiza kwenye kinyeo (rectum)nakusubiri kwa dakika2 Kisha kuchomoa nakusoma Apo Kama joto lake litakua 40C-41C ,na naweza sema ana SALMONELLOSIS dawa yake Ni sulfonamide au sulfadiazine pia sulfamethoxazole zinasaidia ayo Ni majina ya kitabibu majina ya trade Ni BAYTRIL

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Wakati nasoma Olevel ndipo kwa mara ywanza nilishuhudia mnyama anatundikiwa drip..

Ng'ombe wa mkuu wa shule alijaa gesi siku2 baada ya kutoka kuzaa basi alizidiwa mpaka hatua ya kushindwa kujigeuza akamlalia ndama wake mpaka akafa basi aliitwa dr wa mifugo maana alikuwa ni ng'ombe wa kisasa Fresian,alipofika akamtundikia drip kisha akamuingiza kifaa flani hv km bisibisi kisha akakifungua ule mshikio wake wa juu bomba likabaki tumboni basi ikaanza kutoka gesi yote kisha baada ya kumaliza akachomoa ule mrija wa kile kifaa akasema hapahitaji kushonwa panajiziba penyewe.Ng'ombe akapona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…