Tatizo la NHIf ni mpango kazi

Tatizo la NHIf ni mpango kazi

August

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2007
Posts
9,327
Reaction score
5,206
Tatizo la NHIF mpango kazi wao hauendani na mapato yao, na hii ni kwa sababu hakuweka watu sahihi katika kutengeneza, mpango kazi katika shughuli zao za kila siku na mipango yao ya muda mfupi na muda mrefu.

Pili, inaonyesha pia wajumbe wa bodi pia unamapungufu katika kusimamia na kuthibitisha mpango kazi wa NHIF.

Tatizo mojawapo la mpango kazi wa NHIF, ni ule wa kuwakopesha watoa huduma, ili waimarishe miundo mbinu yao, hapa NHIF, wangejenga hiyo miundo mbinu na kuwa ya kwao, iwe ni majengo, X-ray , duka la madawa n.k

Lingine ni kutumia fedha za muda mfupi kwenye miradi ya muda mrefu, hivyo wao wanapotakiwa kulipa madeni ya muda mfupi hiyo hela hawana, na zile walizowekeza, kwenye kuendeleza majengo ya watoa huduma nazo hawanazo kwani hizo walitegemea kuzirejesha kwa kupewa huduma za muda mrefu.

Na lingine kutokuwa na maamuzi katika gharama za huduma na dawa na hii imetokana na kupanga mipango kazi vizuri na kuwa na wajuzi wa kupanga mipango hiyo kabla ya kuingia mikataba na watoa huduma na kuishauri serikali katika kupanga kiwango cha kuchangia kwa mwanachama moja, familia n.k, na jinsi ya kuwaingiza watu wengi zaidi walio katika sekta zisizo rasmi.

Jingine ni kupanga mpango wa madiliko ya matibabu kutoka ya kutochangia hapo Mwanzo kuja mfumo huu, na kuna watu walikuwa wanakaribia kustaafu n.k, hivyo kuwaondoa watu wengi na kuwaacha wanaelea.
 
Back
Top Bottom