Tatizo la saratani ya ini

Poleni sana.

Kama imethibitika ana saratani ya ini, cha muhimu ni kujua stage ya saratani yenyewe.

Ila hakuna dawa ya uhakika 100% kiwa atapona. Japo zipo zinazoonyesha matumaini kidogo kwa wale wagonjwa waliopo katika hatua za awali za saratani.

Kama saratani imefika stage ya mwisho, basi anapaswa kutafuta dawa za kumpunguzia maumivu tu huku akisubiri siku yake. Huo ni ukweli ambao familia mnapaswa kukubaliana nao.

Afya ya mpendwa wenu ni muhimu sana pamoja na uhai wake, ila kuna mahali mkifika hampaswi kutumia gharama kubwa ambazo hazitozaa matunda.

Mungu akawe mfariji wenu.
 
Hepatitis B(Homa ya Ini) ni Ugonjwa wa ngono inatakiwa mtu upate chanjo mara mbili kabla ya kuupata ndo hautaupata Teena.... Chanjo yake niliambiwa ni 30k Moja ya hospital za hapa mjin dar
 
Hepatitis B(Homa ya Ini) ni Ugonjwa wa ngono inatakiwa mtu upate chanjo mara mbili kabla ya kuupata ndo hautaupata Teena.... Chanjo yake niliambiwa ni 30k Moja ya hospital za hapa mjin dar
Homa ya ini ni kisababishi kikubwa sana cha saratani ya ini. Unaweza kupata chanjo ya Hepatitis B na bado ukapata saratani ya ini, Hepatitis C ikiwa sababu mojawapo.

Ijapokuwa, ukipata chanjo ya Hepatitis B unapunguza chances za kupata saratani ya ini.
 
Mpelekeni hapo Ocean hospital, watawashauri cha kufanya; kwa sababu mnapigania uhai, mnaweza kwenda kwenye maombezi na njia zingine mbadala.​
 
Chanzo kikubwa ni pombe kali, bila kula; nilimpoteza mdogo wangu kwa hilo tatizo.
 
Mkuu kuhusu tiba ya Chemotherapy sio nzuri na haiponyeshi kabisa hiyo Chemotherapy. kuna dawa za asili zinazoweza kutibu Saratani ya ini na akapona kabisa anitafute mimi kwa wakati wake ili nipate kumtibia amradhi yake apate kupona.
 
Zitaje majina hizo dawa. Ili tuzigoogle sifa zake

Sio mambo ya utapeli wa waganga wa kienyeji.

Kuna wagonjwa kibao ocean road wanahangaika.

Na mpaka wazungu wanahitaji hizo dawa.

TFDA wanazitambua hizo dawa ?
 
Mkuu sorry sana mimi ndugu yangu imanuel alifarik kwa hepatitis alichelewa ika develope cancer.hakuwa anakunywa pombe kama mimi..swali ni je hiyo jamaa wako anakunywa?
hnywi ni mwisilamu safi
 
hali ya mgonjwa sio mbaya, ametumia miti shamba na imeonyesha dalili nzuri., mwanzoni alikuwa inaonyesha maji kuongezeka kwenye ini na ukubwa wa ini kuongezeka, kwa sasa ini linapungua maji ndiyo bado , mbali na maumivu hana dalili yoyote
 
Mkuu kuhusu tiba ya Chemotherapy sio nzuri na haiponyeshi kabisa hiyo Chemotherapy. kuna dawa za asili zinazoweza kutibu Saratani ya ini na akapona kabisa anitafute mimi kwa wakati wake ili nipate kumtibia amradhi yake apate kupona.
Sasa kazi imeanza wazee wa fursa wameanza mgonjwa kaa chonjo madaktari wameanza kujtokeza .
 
Mwambie akazane tu kula vyakula vya kusaidia ini kuwa imara, aongeze ulaji wa vyakula vinavyoongeza kiwango cha madini ya chuma mwilini, afanye mazoezi ili kuongeza kiwango cha oxygen mwilini na ikibidi akanunue mtungi mdogo wa oxygen awe anatumia pale anapojisikia vibaya sana.

Aachane na pombe kabisa na vyakula vya wiwandani, anywe sana maji aachane na stress hata za mapenzi. Mwisho kabisa aachane na chemotherapy asiende. Kama atatakiwa kufanyiwa upasuaji wa kuta uvimbe sawa akafanya but baada ya hapo aachane na chemotherapy maana huwa inaamsha changamoto zaidi ambazo siwezi kuzielezea hapa maana zimekaa kitaalamu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…