Mapensho star
JF-Expert Member
- Jun 30, 2016
- 3,052
- 4,104
Kwa miaka mitano tangia uingie madarakani wapo wananchi wengi waliokuunga mkono wakakubali kufunga mikanda wakasahau yale yote uliyowaahidi ili mambo ya msingi yafanyike wakitegemea mambo yatakuwa mazuri mbeleni
Ni kweli umefanya mengi Mheshimiwa kama watangulizi wako ambayo walishayafanya anajenga reli ya kisasa,unajenga bwawa,umeboresha miundombinu mingine kama flyover na barabara
Sasa umefika muda wa kampeni wananchi wamejitokeza wengi walikuwa wanategemea kusikia maendeleo yanayowagusa watu
Ni kweli miundombinu ni muhimu lakini maendeleo ya watu ni muhimu pia kwa hili Mheshimiwa kuna kila dalili watu itabidi waendelee kukaza mikanda kwa kipindi kingine cha miaka mitano ili miradi ikamilike