Uchaguzi 2020 Tatizo la sera za Rais Magufuli ni kutogusia maendeleo ya watu kwenye kampeni zake

Maendeleo ya vitu bila ya maendeleo ya watu hayo sio maendeleo ya kweli. Nilijiandaa sana kusikia sera za maendeleo ya watu mfano namna ya kuwapa bima wananchi zaidi ya milioni 50, issue za food security na kadhalika. Ila ninachokisikia ni midege na ma-SGR tu. Ndiyo maana kampeni za sasa hazina mvuto
 
Maendeleo ya watu yanakuwaje? Fafanua kwa undani
 
Hivi mtu anashindwa kupata hata chai ya asubuhi, anadandia malori kwenda kijijini kwake eti aje kupanda flyover sijui ndege. Labda zile ndege za sabasaba.
 
Unazungumziaje maendeleo ya watu wakati hujaweka viwezeshi vya hao watu kupata maendeleo? Huwezi kuwa na viwanda vikubwa vinavyoajiri watu wengi bila kuwekeza kwenye umeme wa uhakika. Huwezi kuwaambia wananchi walime mazao ya biashara wakati hujawekeza katika miundombinu ya kuwafikia wananchi. Huwezi kutaka wananchi wafanye kazi wakati hujawekeza kwenye huduma ya afya. Huwezi kuhubiri afya njema wakati hujawekeza kwenye maji safi. Usitegemee maendeleo ya watu katika sehemu ambayo mtu akitaka kwenda eneo jingine lenye umbali wa kilomita 300 anatumia siku mbili hadi tatu. Usitegemee maaendeleo ya watu katika eneo ambalo watu wanalima nyanya lakini zinatumia siku tano hadi kufika sokoni. Huwezi kutegemea maendeleo ya watu katika eneo ambalo mtoto anatembea umbali wa kilomita 30 kuikuta shule. Huwezi kutegemea maendeleo ya watu katika serikali ambayo zaidi ya asilimia 20 ya wafanyakazi wanatumia vyeti vya kufoji.
 
Uwanjani tulienda kuangalia tamasha la mziki wala hatujaenda kumsikiliza yeye!!
 

sio tatizo la magufuli ni tatizo la wajinga ambao hawajui uwekezaji huanza kwanza! haiwezekani ufanye kazi sehem ambapo hapafanyiwa uwekezaji kuanzia kujenga ofisi
 
Kuzidi ya lisu?
Watu wa chadema kila kukicha mnateseka na mwazo hata mkiwa kwenye majukwaa mnatoa povu la moshi wa kumi mpaka mapafu yenu yatajaa ukungu.

Mpaka uchaguzi uishe mtakuwa wateja wa mahospitali yaliyo jengwa na jembe.
Umeandika nn sio lazima ujibu kila kitu unapoteza haina yako humu au ndio mnafundishwa huko ccm maana nasikia hata baba yenu anasema anataka kazi ya kufagia kwa vyumba vya malaika. Jifunzeni kutoa hoja za kufikirika
 
Umeandika nn sio lazima ujibu kila kitu unapoteza haina yako humu au ndio mnafundishwa huko ccm maana nasikia hata baba yenu anasema anataka kazi ya kufagia kwa vyumba vya malaika. Jifunzeni kutoa hoja za kufikirika
Punguzeni hasira kwenye mikutano hao ni watu sio ng'ombe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…