Tatizo la Simba ni kocha au wachezaji?

Tatizo la Simba ni kocha au wachezaji?

Mzee Ngonyani

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2022
Posts
1,049
Reaction score
2,242
Mimi nikiwa kama mpenzi na shabiki wa Simba sports club sifurahishwi na mwenendo wa timu pamoja na matokeo mazuri ya uwanjani. Timu haiko vizuri hatuna beki ukuta unavujisha na upande wa ushambuliaji ni butu.
Wapenzi wa mpira wa miguu karibuni nanyi mseme chochote maana mwenzenu nina wasiwasi hasa mashindano ya kimataifa.Tutatoboa kweli?
 
Me naona vyote,

Kocha mpira anaofundisha sio na wachezaji wanacheza kifaza sanaaa HAWAJITUMI na jawana ARI/UCHU wa mafanikio
 
Timu si inaongoza ligi.
Ipo super Cup.
Ipo championship

Halafu siku hizi si mnacheza direct football,iaminini timu yenu.
 
Naona aina ya mfumo wa kocha ni kutaka matokeo tu hata Timu zenye mafanikio huko CAF ni hizo Wydady au Esperance hawaeleweki ila kwenye matokeo wao ndio wanapita Mamelodi wana mpira wa kuvutia ila pana hatua matokeo ndio yanahitajika inatakiwa uchezwe mpira wa Matokeo hata hawa Al Ahly mpira wao sio wa pasi nyingi ni kupata matokeo ndio maana umewaona wamekuja daslm muda mrefu ili kupata matokeo na si aina ya kucheza Mpira wenye udhamini wa fedha nyingi una vitu vingi sana ili kufanikiwa wacha niishie hapa kidogo...
 
Timu si inaongoza ligi.
Ipo super Cup.
Ipo championship

Halafu siku hizi si mnacheza direct football,iaminini timu yenu.

Papatu papatu tutafika kweli. Kocha anaomba muda uishe rejea mechi na singida
 
Utopolo kwenye Kivuli cha simba sie simba tupo busy na Africa super league
 
Mimi nikiwa kama mpenzi na shabiki wa Simba sports club sifurahishwi na mwenendo wa timu pamoja na matokeo mazuri ya uwanjani. Timu haiko vizuri hatuna beki ukuta unavujisha na upande wa ushambuliaji ni butu.
Wapenzi wa mpira wa miguu karibuni nanyi mseme chochote maana mwenzenu nina wasiwasi hasa mashindano ya kimataifa.Tutatoboa kweli?
Ikiendeleza mtindo huo mpaka ikachukua kombe la super cup bado utaendelea kutokuwa na fulaha? Sisi tunataka ushindi kwa mtindo wowote wa uchezaji ndugu.
 
WEWE NI MAALUKI

TIMU INAONGOZA LIGI
IKO SUPER CUP
IKO MAKUNDI AFRIKA
HIYO HIYO TIMU IMEMFUNGA YANGA NGAO YA JAMII.

UNATAKA NINI ZAIDI??

UCHEZE VZR BILA CHOCHOTE UMEKUWA ASENO?
 
Back
Top Bottom