kwa ujumla ni kwamba klabu zote zinaendeshwa na watu mbumbu sana na wapiga dili tu.japokuwa wanajifanya wanajua hawajui chochote. hasan dalali na kadguda walifanya kazi kubwa sana na ya mfano walipoiacha klub ikaangukia mwa wahuni tu.Ukiondoa Klabu ya Azam, ambayo uendeshaji wake upo kisasa, klabu zingine zote kubwa hapa Tanzania plus TFF zinaendeshwa kihuni, kienyeji na kiujanja ujanja tu. Hazina vision wala mission, zipo zipo tu. Simba na Yanga, zote ni pasua kichwa. Zinaingiza pesa nyingi sana lakini zina mifumo mibovu balaa ya kutumia pesa.
Viongozi hawa waliopo ni wabovu. Haya matokeo ya leo utasikia kocha anafukuzwa. Wakati maandalizi yenyewe hayakuwepo.
Mkurugenzi wa ufundi simba ni nani (Technical director)
Nani mwalimu wa utimamu wa mwili kwenye timu?
Nani mkurugenzi wa masuala ya itifaki katika timu? An?yetambua wachezaji wanakula nini kambini, wanalipwaje, wanalalaje, maisha yai nje ya mpira wa miguu.
Simba na timu nyingi za Tanzania zipo kienyeji.
Yani leo bado tuna mfumo wa MWEKA HAZINA. Mfumo wa kizamani kabisa.
Ishu kwa Mo Dewji kuitaka Simba, kwanza yeye ni simba damu, pia ni mfanyabiashara anayeona fursa za kupata faida, pili ni kuwa simba na yanga zina FANBASE kubwa sana! Viongozi wa hizi timu wangekuwa smart, kuna hela nyingi sana!
Azam itaendelea kuwa timu inayoendeshwa kisasa, ila kamwe upande wa fanbase hawataifunika simba au yanga! Hata miaka mingi ijayo, hizi timu mbili zitaendelea kuwa na fanbase kubwa! Timu zingine kama Azam zitaendelea kuwa na fans wa mkopo, Azam wakicheza na simba, watawapata fans wa yanga na yanga wakicheza na azam watapata fans wa simba, simple!
Sio kila jambo baya linalofanywa na timu ya simba linafananishwe na yanga, Kuna mchezaji wa yanga anaelalamikia sehemu ya kulala!! Mishahara je!!!?
Tumia akili unapocomment
Simba & yanga majupu
Majabvi mi maskini ubishi wangu umeniponza, Ngoma na Kamusoko washiba Jangwani, nakufa hapa kwa nini?
Hans Poppe ajitazame upya, inajidhihirsha kuwa tatizo la Simba ni Hans Poppe kwa sababu anajenga na kubomoa yeye mwenyewe. Ubabe haujawahi kuwa suluhu ya kudumu ya matatizo. Apunguze ubabe na jazba ajenge timu
Najua Simba wengi hawatanielewa lkn Hans Poppe ndio kikwazo kikubwa
Mzee inaonesha hunaifahamu simba lakimi siyo deep, kuna kiumbe hai anaitwa Kaburu acha kabisa!!
Kaburu namsikia kila mara akilalamikiwa lkn Hans Poppe ni mbabe hakuna na wachezaji wanamuogopa kama nini. Kila bifu analitolea ufafanuiz wa ubabe. Haiwezekani ndani ya muda mfupi wachezaji zaidi ya wanne walalamikie suala la nyumba halafu Poppe anakuja na majibu ya kibri na mkato. Simba kuna tatizo
Mkuu kukosa hela si umasikini, bali umasikini ni kukosa mawazo ya namna ya kupata pesa.Klabu kukosa hela sio aibu, ni umaskini tu. Hata wewe au ndugu yako akikosa hela sio jambo la aibu, ni umaskini tu. Yanga na Azam zinaonekana zina hela, si ujanja wa viongozi wake, bali kuna mtu amekuwa anatoa tu hela zake binafsi kuendesha klabu, na wala si mapato ya klabu. Leo mfadhili akitaka kujitoa, watu wazima wenye familia zao wamampigia magoti, hiyo ndiyo aibu!
Akisikia atakushangaa wewe zaidi. Mwenzio hanunui timu, ananunua mashabiki!!Nilimshangaa sana Mohamed Dewji kutaka kuwekeza pesa zake Simba. Ni mara mia akaanzisha timu yake binafsi, akaikuza baada ya miaka minne itakuwa ligi kuu, ikiwa na viwanja vyake, Jezi zake, Wachezaji wake, nk na kuwa Big brand ya Soka hapa Tanzania na Ukanda wa Afrika.
Azam wameweza na wataweza zaidi na zaidi. Kwa nini MO Dewji asiige mfano huo?