Tatizo la Simba ya sasa ni kocha mzuri au wachezaji wazuri?

Tatizo la Simba ya sasa ni kocha mzuri au wachezaji wazuri?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Sioni namna Pablo kocha mgeni Simba atakavyoweza kupata matokeo mazuri kwa wachezaji waliopo Simba. Kocha ni wa kawaida na wachezaji ni wa kawaida pia.

Pablo angekuwa kocha mzuri sana angeshanyakuliwaa na timu za Barcelona, Man U, au Tottenham zilizokuwa zinatafuta makocha wazuri. Ni kocha wa kawaida sawa na makocha wengine wa kibongo bongo ambae anahitaji kupata wachezaji wazuri ili apate matokeo mazuri.

Cedric kaze alikuwa Barcelona lakini Yanga alikuwa hapati matokeo kutokana na aina ya wachezaji aliowakuta Yanga wakati ule.

Wachezaji wa Simba hawana vipaji vikubwa sana kuwazidi wengine, wanatumia bahati zaidi, janjajanja, nguvu na mbinu za nje ya uwanja kupata matokeo kuliko ufundi. Wachezaji aina ya Chama, Mayele, Aucho, Bangala, Fei Toto na Dube hawana Sasa hivi.

Kagere, Wawa, Bocco, nyoni, Ajibu, kapombe, Mugalu, muzamiru, mkude, Kibu wote ni WA kuanikizaanikiza juani ili kupata matokeo. Ni wachezaji sawa na wachezaji wa timu nyingine kwenye ligi.

Waandishi na mashabiki wa Simba huu ndio wakati wenu wa kuweka akiba ya maneno kuhusu Pablo na Simba.
 
Haya mliyasema msimu uliopita na matokeo mliyaona.. kuweni wapole hao mnaowaita mababu ndo wanaoipa Simba heshima mwisho wa siku
Unapata matokeo kwa timu pinzani kuwa na wachezaji pungufu, huko ni kujidanganya. Timu zote zinazocheza na Simba zinagoma kuingia vyumba vya kubadilishia nguo viwanjani, hakuna anayejiukiza Kwanini, hata CAF wanalifahamu hili isipokuwa TFF.

Timu ziko tayari kutozwa 500,000 adhabu kuliko kuingia vyumbani. Baada ya janjajanja hii ya pulizapuliza kugundulika Sasa hivi wamekuja na mbinu mpya ya red cards.
 
Unapata matokeo kwa timu pinzani kuwa na wachezaji pungufu, huko ni kujidanganya. Timu zote zinazocheza na Simba zinagoma kuingia vyumba vya kubadilishia nguo viwanjani, hakuna anayejiukiza Kwanini, hata CAF wanalifahamu hili isipokuwa TFF. Timu ziko tayari kutozwa 500,000 adhabu kuliko kuingia vyumbani. Baada ya janjajanja hii ya pulizapuliza kugundulika Sasa hivi wamekuja na mbinu mpya ya red cards.
Hayo ndo matokeo na kawaida ya kucheza na mtu aliekuzidi uwezo ukijifanya kumkamia unakula kadi hahahaha

Hayo ya kugoma kuingia kwenye vyumba vya kubadilisha nguo ni masharti ya kichawi kama ilivyo kwa yanga kugomea rangi nyekundu
 
Hayo ndo matokeo na kawaida ya kucheza na mtu aliekuzidi uwezo ukijifanya kumkamia unakula kadi hahahaha

Hayo ya kugoma kuingia kwenye vyumba vya kubadilisha nguo ni masharti ya kichawi kama ilivyo kwa yanga kugomea rangi nyekundu
Hiyo sio kweli, huko Ulaya Kuna timu kubwa na ndogo pia, lakini timu kubwa hazipati matokeo kwa timu ndogo kupewa kadi nyekundu wachezaji wao.
 
"..angekuwa kocha mzuri sana angeshanyakuliwa na timu za Barcelona, Man u au Tottenham..."
Kwa hoja hii ya kipoyoyo hakika wewe ni utopolo haswaa.
 
Ila Utopolo buana[emoji2]

Eti " Pablo angekua kucha mzuri angechukuliwa na Barcelona or Man United sababu wanatafuta kocha bro" [emoji2]

Kwahiyo unataka kusema Simba "Mnyama" Levels zake ni zile za Barca na Man U?[emoji2]

Simba akichukua kitu ambacho hakipo kwenye radar/malengo ya Barca na Man U ni kibaya?[emoji2]

Naona mmeanza kujitioa wenyewe in term of Levels. UTO......UTO.......UTO...POLOOO[emoji2][emoji706]
 
Paragraph ya pili andiko lako ndilo limebeba maudhui ya uzi na kadri nilivyosoma inaonekana una ufinyu wa kufikiri, siyo bure.

Yaani Simba iwe sawa na Barcelona, Madrid nk ni ufinyu, kwani siyo kwa Tanzania tu bali kwa bara zima la Afrika kuna team unaweza kufananisha na Barcelona nk kwa kila nyanja yaani viwango vya ubora, utajiri nk?

Ungetafuta team zingine za bara la Afrika kisha ungefanya hiyo comparison
 
Ila Utopolo buana[emoji2]

Eti " Pablo angekua kucha mzuri angechukuliwa na Barcelona or Man United sababu wanatafuta kocha bro...
Kwanini haya? Kuna watu wanavumisha na ku justify ubora wa Pablo kwakuwa alikuwa msaidizi Madrid.
 
Sioni namna Pablo kocha mgeni Simba atakavyoweza kupata matokeo mazuri kwa wachezaji waliopo Simba. Kocha ni wa kawaida na wachezaji ni wa kawaida pia....

Sasa mbona umchagua wachezaji wa kutolea mfano?

Bwalya, Sakho, Inonga, Wawa, Mohammedi Hussein, Manula, Kanoute, Kibu, Dancun hawa hukuwaona? Hivi Bangala ana kipi kikubwa cha kumzidi Tadeo Lwanga? Huyo hata kwa Mkude hafikii bali kinachowapa upofu ni hayo matokeo muliokwisha kupata.

Halafu utafautishe Academy na Senior Timu! Usione haya kusema Kaze alikuwa Academy analea Watoto wa Chekechea Tofauti na Pablo aliyekuwa Senior Team na kina Ramos.
 
Sasa mbona umchagua wachezaji wa kutolea mfano?...
Sijui nikwambie nini kuhusu kanoute, Banda, sakho, na Kibu, hawa ni wachezaji ambao level na vipaji vya havipishani na vya akina Ambundo, muhilu, nchimbi, shemtembo, ndemla, Rashid Juma, nk.

Kule Africa ya magharibi Kuna mawakala wengi sana na wazuri wanaosaka vipaji. Kama kanoute na sakho wangekuwa na vipaji vya hali ya juu wangeshanyakuliwa na timu za Ulaya na Africa Kaskazini vya waarabu. Luhanga na Kibu wanategemea nguvu zao zaidi kuliko kipaji.

Mourihno ni kocha mzuri sana lakini wachezaji ndio wanaomuangusha. Unaweza kuwa kocha mzuri lakini huna wachezaji.

Mafanikio ya Simba ya kufika robo finali yaamechagizwa na vitu vingi sana hasa vya nje ya uwanja kama vile viporo vingi kwenye ligi, ujanja wa kwenye nyumba vua kubadilishia nguo, marefa.

Ndio maana Simba haina consistency kwenye CAF champions league. Kwakuwa wanategemea mambo ya nje ya uwanja zaidi kuliko mpira.
 
Sijui nikwambie nini kuhusu kanoute, Banda, sakho, na Kibu, hawa ni wachezaji ambao level na vipaji vya havipishani na vya akina Ambundo, muhilu, nchimbi, shemtembo...

Kwahiyo na hao kina Aucho, Bangala na Mayele ni level za kina Mzamiru Yasini kwani wangekuwa na vipaji vya hali ya juu wangeonekana na hao mawakala wa West Afrika si ndiyo?
 
Kwahiyo na hao kina Aucho, Bangala na Mayele ni level za kina Mzamiru Yasini kwani wangekuwa na vipaji vya hali ya juu wangeonekana na hao mawakala wa West Afrika si ndiyo?
Kweli kabisa, wangekuwa wako PSG ufaransa, SEMA Wana afadhali, yaani ni kama Bocco na Waziri Junior, Bocco ana afadhali kidogo ya Waziri Junior kwenye kufunga mabao ingawa wote wameahindwa kupenya soko la Ulaya na Afrika Kaskazini.
 
Back
Top Bottom