Tatizo la Tanzania sio Katiba Mpya bali utii wa Katiba iliyopo

Mkuu 'Menuka jr', imenilazimu nirudi haraka baada ya kubandika niliyobandika mwanzo...a?
Na Dhani ndio msingi mkuu wa bandiko tajwa hapo juu mkuu. Ni wakati wakugundishwa UTII WA SHERIA kwa kuwa uwepo wa sheria ni jambo moja na utekelezaji wake ni jambo tofauti kabisa...

Sent from my itel W5001P using JamiiForums mobile app
 
... kwa namna moja uko sahihi; utii wa katiba imekuwa tatizo sugu kwa viongozi. Nini kifanyike? Au Katiba yenyewe inasemaje kwa wasiotaka kuitii? Ok, unaweza kusema asiyeridhika "aende mahakamani" kauli pendwa ya viongozi...
Kwema mkuu?

Loop holes hazikosekani katika sheria yoyote duniani na ndio maana mawakili wapo na wanamtetea mtu aliyeua na anashinda kesi.

Brother sheria sio kama hesabu au sayansi ambayo ni factual based na sio theory. 1+1=2 hii iwe kichina, kikorea, Japan hata Kifipa lugha ya baba na mama.

Low of motion, quantum physics, rasperatory system haijalishi lugha gani unatumia content ni ile ile.

Sent from my itel W5001P using JamiiForums mobile app
 
South Africa ANC ndio yenye Rais wake na sio serikali.

Hivyo chama ndicho kinamuweka au kumuondoa

Sent from my itel W5001P using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kalamu. South Africa wameweza kumuondoa Zuma na sasa wanampwleka Jela . wao wanawezaje? Haya mambo yanawezekan ili mradi katiba iseme hivyo
Amesikia tu fatilia kama Zuma kaenda Jela. Watu wanataka katiba mpya ili wagawane madaraka lakini kwao hoja za wananchi hamna.
 
Na Dhani ndio msingi mkuu wa bandiko tajwa hapo juu mkuu. Ni wakati wakugundishwa UTII WA SHERIA kwa kuwa uwepo wa sheria ni jambo moja na utekelezaji wake ni jambo tofauti kabisa...

Sent from my itel W5001P using JamiiForums mobile app
Sawa, ninakubali uliyoandika.

Katiba iliyopo sasa inampa madaraka makubwa sana huyo kiongozi mmoja kiasi kwamba hata "ukigundisha utii wa sheria" madaraka aliyonayo mkubwa huyo ni kama yanamuweka juu ya sheria zenyewe unazotaka 'zigundishiwe utii'.

Na kwa madaraka hayo makubwa aliyonayo, hata katiba hiyo hiyo inaonyesha ina upungufu juu ya kuhoji matendo yake, na hakuna wa kumwajibisha anapokiuka matakwa ya katiba yenyewe.

Sasa hapo sijui wewe unaoje kuhusu huo "ugandishi wa utii wa sheria." Una maana hawa viongozi wa chini ndio 'wagandishiwe utii? Itawezekana vipi huku mteuzi wao ndiye anayewahimiza watende matakwa yake.

WaTanzania wakati mwingine tunajidanganya na kudhani sisi ni wajanja kumbe hatuna lolote! Tunatetea jambo ambalo tunajuwa wazi kwamba utekelezaji wake hauwezekani, lakini tunakomaa kweli kweli na upotosha ulio wazi.
 
South Africa ANC ndio yenye Rais wake na sio serikali.

Hivyo chama ndicho kinamuweka au kumuondoa

Sent from my itel W5001P using JamiiForums mobile app
Una maana wananchi wa Afrika Kusini hawamchagui rais wao, au siyo? Hawampigii kura?

Vipi, mbona kama ni sawa tu na sisi hapa. CCM ndio wanaoteua mtu wao, lakini sisi wananchi tunajihadaa tu kwamba tunakwenda kumpigia kura rais ambaye tayari amekwisha teuliwa na CCM?

Tatizo la CCM ambalo pengine ni tofauti na ANC, wakishamteua mtu wao kuwa Rais na mwenyekiti wa chama, wanapoteza uwezo wao wa kumwondoa, kwa sababu tayari anayo mabunduki, mabomu na mahela ya kuwanyamazisha wanaofanya fyokofyoko huko ndani ya chama.

Huenda ANC wao bado wanyo nafuu juu ya hili. Mteule wao wanabaki na madaraka ya kumwadabisha akikiuka masharti ya chama. Hapa kwetu hilo haliwezekani.
 

Bro, popote pale ulipo kunywa chochote (lkn siyo kilevi, ili uendelee kutoa madini maridhawa) nitapita kulipa.
 
Tatizo la wanasiasa wa Tanzania ni kuifanya siasa ni ajira na jiko la kujikimu, badala ya kuichukulia kuwa ni sehemu ya kujitolea muda na uwezo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na taifa kwa ujumla.

Ndio maana wanaoshindwa katika chaguzi wanapenda kila siku kupiga siasa za kuwawezesha kutawala ili wakidhi matakwa binafsi, na hawana muda wa kukipa muda chama kilichoshinda uchaguzi kitekeleze ilani yao waliyoinadi na kukubalika kwa wananchi.

Kwa sababu hiyo wapo radhikuihujumu nchi yao na kuiweka reheani maslahi ya taifa, kwa kushirikiana na maadui wa Tanzania, ili mradi mabeberu hao wawe tayari kuwapa ruzuku za kujikimu na kuendesha vyama vyao.
 
Sote kwa umoja wetu TUHUBIRI KUTII TARATIBU BILA SHURUTI. TUJENGE JAMII AU NCHI ILIYO NA WATU WENYE MLENGO NA MTAZAMO WA KUTII SHERIA, MIONGOZO NA TARATIBU BILA SHIRUTI.
Licha ya kuwa mkazo mkubwa uko katika katiba mpya, lkn pia kuwe na nguvu hiyo hiyo katika kuhamasisha jamii kutii miongozo, taratibu, sheria na katiba bila shuruti.
Kama upande wa kujenga jamii yenye kutii sheria halitiliwi mkazo, basi hata ikija katiba mpya itakuwa ni bure, kwa maana jamii yetu itakuwa imejengwa katika misingi ya kutotii sheria. Hata katiba iwe nzuri kiasi gani, kama wananchi hawaitii na wana mtazamo na muelekeo wa kuipuuza, itakuwa haina faida.
Lkn hata mkiwa na katiba mbovu kiasi gani, lkn inaheshimiwa, hiyo itakuwa ni bora mara mia kwa mamia, kuliko kuwa na katiba nzuri isiyofuatwa.
 
Katiba Mpya ni muhimu, hii ya sasa ina udhaifu mkubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…