Tatizo la Tanzania sio Katiba Mpya bali utii wa Katiba iliyopo

Tatizo la Tanzania sio Katiba Mpya bali utii wa Katiba iliyopo

Mjadala wa madai ya Katiba mpya unaendelea kushika hatamu. Baadhi yetu wanadai kuwa nchi inahitaji Katiba mpya, wanatoa sababu zao. Madai yao ni ya kuheshimiwa kwa sababu ni haki yao lakini ni yenye kustahili kusahihishwa kwa sababu si ya kweli. Ni uongo...
Kwanza mfano wako wa Rais na Baba ni fallacious

Uhusiano wa baba na familia yake ni wa blood relationship ambao kimsingi baba anakuwa na Moral obligation tu ya kuweza kutekeleza majukumu as a father.

Uhusiano wa rais na wananchi ni Contractual ule wa social contract na kutoka katika uhusiano huo rais anakuwa na Both Legal obligation ya kwanza kutekeleza matakwa ya social contract na wananchi wake.
Pili kutokutenda yale ambayo siyo matakwa ya social contract.

Rais anapochaguliwa haongozi kwa utashi wake binafsi anaongoza kwa kuzingatia social contract aliyoingia na wananchi hivyo lazima katiba iweke misingi Bora ya rais kuweza kuongoza ikiwemo safeguard za protection ya wananchi waliomchagua.

Hebu nikuulize kwa kuzingatia huo mfano wako.
Baba anaweza akakimbia familia yake, au akawa mlevi kupindukia hivyo kutekeleza wajibu wake je rais naye akiwa mlevi au kuwakimbia wananchi aachwe tu kwa sababu hata ushauri wenyewe atakaopewa siyo lazima afuate?

Utii wa katiba na sheria za nchi ni wajibu wa lazima siyo hulka ya kiongozi na hakipaswi kufundishwa sheria ni enforceable lakini ili sheria iwe enforceable lazima ziwepo taasisi za kutekeleza hiyo enforceability ya hizo sheria.

Katika katiba yetu
Rais ana kinga ya kushitakiwa mahakamani hata kama atakuua wewe hadharani barabarani hatashitakiwa.

Chombo pekee cha kuweza kumwajibisha rais ni bunge lakini rais huyo huyo ana mamlaka ya kuvunja bunge likikataa bajeti au kutaka kumwajibisha yeye kwa impeachment wewe huoni kuwa huo ni udhaifu mkubwa wa katiba ya nchi ?

Niishie hapa kwanza
 
Mjadala wa madai ya Katiba mpya unaendelea kushika hatamu. Baadhi yetu wanadai kuwa nchi inahitaji Katiba mpya, wanatoa sababu zao. Madai yao ni ya kuheshimiwa kwa sababu ni haki yao lakini ni yenye kustahili kusahihishwa kwa sababu si ya kweli. Ni uongo...
2020 Bunge la katiba ya Jamhuri ya Muungano lilipitisha sheria iliyofanya marekebisho katika The Basic Rights and Duties Enforcement Act kuzuia watu binafsi kufungua constitutional petitions mpaka upeleke kiapo kinachoonyesha umeathiri personally na huo uvunjifu wa katiba hii maana yake ilifuta rasmi Public Interest litigations kwa watu binafsi na mashirika yanayopigania haki za binadamu.

Wakati huo huo ilipitisha sheria ya kuweka kinga kwa kinga kwa rais, spika , naibu spika na Jaji mkuu kutoshitakiwa mahakamani kinga hii moja kwa moja inaondoa uwajibikaji wa watumishi hao kwa umma.

Yote hayo yanaweza kufanyika kwa sababu katiba mbovu iliwezesha yafanyike.
 
Tatizo la watanzania sasa ni huu umasikini. Watanzania wengi wanawaza kuwa na maisha bora angalau pesa itembee mikononi mwao. Kuwaletea Katiba Mpya kwa sasa hata hawakuelewi zaidi wataona ni mpango wenu nyie wanasiasa kujinufaisha..
Umaskini wenyewe unaletwa na katiba mbovu viongozi haiwajibishi kutekeleza matakwa ya wananchi badala yake wanatekeleza utashi wao binafsi.

Kama tatizo la wananchi ni hospitali au chuo cha Veta na utashi wa rais anaona ni barabara ya flyover kwa sababu rais hawajibiki kisheria kutekeleza matakwa yenu akinunua ndege wakati mahitaji yenu ni hospitali na VETA huo umaskini wenu utaondoka vipi ?

Kama rais anaweza kudictate bunge lifanye vipi kazi na muwe mmewachagua hao wabunge au hamjawachagua wakipitisha bajeti kandamizi kwenu huo umaskini wenu utaishaje ?
 
Andiko lako, naliunga mkono, pamoja na kwamba sijasoma uliyoandika humo ndani, mbali ya Kichwa cha habari na 'subtitles' zake...
Katiba ya nchi ni roho ya nchi katiba mbovu ni sawa na mtu mwenye roho mbaya haiwezi kuleta viongozi wenye matendo mema wakati yenyewe ni mbovu.
 
Rais anaemiliki hazina na majeshi, kama hakuna hulka ya kuheshimu taratibu zilizopo hata kama mkiwa na katiba nzuri vipi atawayumbisha tu.

Vinginevyo mtajikuta mnataka kuandika katiba nyingine kila mwaka.
Hayo ndiyo mapungufu ya kikatiba tuliyonayo yanapaswa kutatuliwa kwa kuweka mustakabali mpya wa katiba yetu.
 
Nakubaliana na wewe pale mwanzoni kwamba tatizo ni kutii Katiba ingawa kwa hakika ukitaka kulipatia tatizo kwa ujumla wake ingefaa isemwe tarizo ni Kukuwepo au kutotekeleza utawala wa sheria. Hao wanaotawala kwa niaba yetu na kwa ruhusa yetu wanatakiwa wafuate Katiba na sheria, wasichaguliwe kisha baada ya hapo wanajigeuza kuwa masultani! Ufafanuzi wako baada ya utii wa Katiba sikubaliani nao. Utawala mzuri wa sheria "Good governance" ni zaidi mno ya maoni yako.
Kwani hao wanaowaongoza ndiyo mliowachagua ?

Katiba yetu imewapokonya wananchi mamlaka katika nchi yao.

Rais anapokuwa madarakani wananchi wote wanageuka kuwa ombaomba kwa rais na ana hiari ya kuwapa wanachokiomba au lah na hawana cha kumfanya

An imperial president
 
katiba ndio msingi ambao sheria zote zinazoendeshwa nchi zimejengwa juu yake mkuu, sheria za uwekezaji au umiliki ardhi na zinginezo zote zinatungwa kwa kuzingatia misingi ya katiba, maisha bora hayawezi kuletwa na katiba mbovu au sheria zitokanazo na katiba mbovu, ila naunga mkono hoja kuwa issue si katiba mpya issue ni kuanza kuheshimu hii iliopo kwanza
Katiba mbovu haiwezi kuzalisha sheria nzuri vile vile haiwezi kuzalisha viongozi wazuri kwa sababu viongozi hawatapatikana kwa njia halali
 
Mjadala wa madai ya Katiba mpya unaendelea kushika hatamu. Baadhi yetu wanadai kuwa nchi inahitaji Katiba mpya, wanatoa sababu zao. Madai yao ni ya kuheshimiwa kwa sababu ni haki yao lakini ni yenye kustahili kusahihishwa kwa sababu si ya kweli. Ni uongo..
MenukaJr Asante kwa mada nzuri sana na namna ulivyowasilisha. Nakubaliana na wewe kwa 100% kuwa tatizo liko kwa elimu ya Katiba na mwenendo wa viongozi wa Kiafrika dhidi ya Katiba. Kama hatuna utamaduni wa kuheshimu Katiba hata hiyo mpya haitatusaidia.

Kwa umri wangu nilikuwa conscious na utawala wa JK Nyerere kwa miaka 17 na nimewashuhudia maRais wote waliofuata.

Nahakikisha kuwa pamoja na mapungufu yake hii Katiba ya JMT ya mwaka 1977 toleo la 2000 maRais wote kasoro Magufuli walijitahidi kuheshimu kwa kiwango cha juu. Nyerere na Mwinyi waliiheshimu kwa 99% wakati Mkapa na Kikwette waliiheshimu kwa 90%. Pale kwenye Tume ya Uchaguzi ndipo palilalamikiwa sana enzi za Mkapa na JK. Ila Magufuli hakuiheshimu Katiba hii kwa kiasi kikubwa. Kama ali observe Katiba labda ni 25%.

Takwa la Katiba mpya liko toka miaka ya 1980s ingawa likikuwa officially documented na Tume ya Nyalali mwaka 1991.

jK alianziaha mchakato wa Katiba lakini kwa sababu anazojuwa mwenyewe hakuweza kumalizia pamoja na kutumia Mabilioni ya fedha za walipa Kodi.

Kwenye utawala wa Mgufuli ndipo Katiba ilionekana so chochote si lolote kwa vile Magufuli alikuwa anasema Mhimili wa Serikali ndiyo umejichimbia zaidi kuliko mingine. Akatishia Mahakama, akaka na Acting Chief Justice, akachagua AG ambaye haja qualify vigezo.

Akalidhibiti Bunge, akawa anamarisha Spika namna ya kuwaadhibu wabunge, kuwafuta nk. Akamfukuza CAG, akaiba uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2019 na Uhaguzi Mkuu wa 2020.

Kimsingi Magufuli ndiye aliyeweka mafuta kwenye moto wa kutaka Katiba mpya. Sasa inatafutwa kutoka kila upande, iwe CCM, Upinzani na Asasi za kiraia.

Mimi binafsi napeleka lawama zote kwa chombo cha TISS pale mwaka 2015. Wao kama wanafanya vetting za kazi ndogo kama za ma DC, ma RC na ma DED, je kufanya vetting ya Wagombea Urais siyo kazi yao?

Ilikuwaje jina la MAGUFULI mwenye rekodi mbaya ya kufuata Sheria na taratibu likapita na kuonekana ni bora kuliko wale wengine 42?
 
Ukiwa na katiba ya kueleweka watu wanasimami viapo vyao. Hakuna polisi utamtuma akauwe watu atakubali eti kwa sababu tu wewe ni mkuu wa nchi.
Mimi nadhani tuanzie hapo, penye "watu kusimamia viapo vyao."

Hali ilivyo sasa hivi, si huyo tu mkubwa wao wa juu kabisa anayekiuka kiapo chake, bali wote hawa walio chini yake kuapa siku hizi ni kama mtindo tu, kwenda kujionyesha mbele za watu na kushika misahafu, bila ya kuwa na dhamira juu ya viapo hivyo wanavyokula.

Pengine, inabidi pawepo na utaratibu wa watu hawa kuwajibishwa kila mara wanapokiuka waliyoapa kuyafuata. Hii itakuwa ni hatua moja katika kurekebisha ukiukwaji mwingi, katika kila ngazi.

Wakati huo huo nikirudi kwenye hoja yako unayosema:
"Ukiwa na katiba ya kueleweka watu wanasimamia viapo vyao" - Inawezekana pia kukawepo na Kiongozi asiyejali hiyo "Katiba inayoeleweka"; yeye akaamua kujifanyia yake. Tumeuona mfano mahsusi kwa Magufuli. Hata hiyo iliyopo, pamoja na mapungufu yake, makatazo iliyokuwa inayakataza katiba hiyo, yeye kayapiga mateke.

Kwa hiyo swali linabaki palepale, hiyo "Katiba inayoeleweka" akitokea kiongozi mwingine wa aina ya Magufuli, na akikiuka na haya mambo yake "yanayoeleweka" ni kipi kifanyike ili kumzuia asikiuke? Nani atasimama na kumzuia asiikiuke hiyo katiba?
 
Ilikuwaje jina la MAGUFULI mwenye rekodi mbaya ya kufuata Sheria na taratibu likapita na kuonekana ni bora kuliko wale wengine 42?
Nimekusoma andiko lako toka huko juu mkuu 'Huihui', na ninakubaliana na maoni yako kwa kirefu, ingawaje ufumbuzi wa tatizo tulilonalo bado sote hatujui litakuwa ni lipi.

Katiba iliyopo sasa ubovu wake mkubwa ni wa kumpa madaraka yasiyokuwa na kikomo mtu anayepewa uongozi wa nchi. Hili moja kwa moja ni udhaifu mkubwa wa katiba hii, ambao nadhani wengi wetu tungependa sehemu hii hasa ishughulikiwe.

Huyu mtu, anakuwa kama ndiye mungu wa nchi hii! Analotamka yeye mara moja inakuwa kama ni sheria hapo kwa hapo, hata kama tamko lake linapingana na sheria zilizopo.

Udhaifu huu wa katiba yetu ndio chanzo cha watu kama Magufuli kuwa na ujasiri wa kukanyaga hata yale mengine yaliyomo kwenye katiba, kwa sababu anajua hakuna mtu mwingine tena juu yake wa kuhoji matendo yake

Magufuli angejua kuna chombo kinachoweza kumhoji matendo yake, asingekuwa na ujasiri wowote wa kuanza kuvuruga kama alivyovuruga.

Tabia ya Magufuli ilieleweka, pamoja na kukengeuka kwake kwa mara kwa mara, alipokuwa waziri, lakini mara tu alipokuwa anakanywa, hukumsikia tena akiendelea na ukichaa wake. Jengo la Tanesco, na hata uvunjaji wa nyumba za wananchi ni matukio aliyoshindwa kuyatekeleza kwa sababu palikuwepo na watu juu yake wa kumfunga breki.
Na hakuthubutu kulalamika wala kutishia kujiuzuru, hapo ndipo ujue hakuwa na kisirani cha ziada.

Lakini alipoukwaa uRais, na akajikuta Katiba inampa madaraka makubwa sana, na hapakuwepo na mtu wala chombo chochote cha kumhoji, jamaa akajichukulia kila kitu; yeye ndiye akawa ni mwongozo wa matakwa ya nchi.

Alijikuta kwenye chama chake hakuna wa kumzima, na huku kwenye mfumo wa nchi hakuna kitu chochote cha kumzuia.

Hao watangulizi wake walikuwa ni watu wenye kutegemea busara; tukimpata kiongozi mwingine asiye na busara chini ya katiba iliyopo sasa mambo yataendelea vilevile kama yalivyokuwa chini ya Magufuli.

Kama kiongozi hana busara, lakini kuna mwongozo unaomwonyesha kwa uwazi kabisa, kwamba hana madaraka ya kufanya mambo kadhaa; hali hiyo inaweza kuwa ni msaada kwake na kwa raia wote.
 
Mimi nadhani tuanzie hapo, penye "watu kusimamia viapo vyao."

Hali ilivyo sasa hivi, si huyo tu mkubwa wao wa juu kabisa anayekiuka kiapo chake, bali wote hawa walio chini yake kuapa siku hizi ni kama mtindo tu, kwenda kujionyesha mbele za watu na kushika misahafu, bila ya kuwa na dhamira juu ya viapo hivyo wanavyokula...
Mahakama ndio kwa sehemu kubwa huwa inawajibisha viongozi.

Katika hali ya sasa ambayo majaji wanachaguliwa na raisi na anawabadili akijisikia inakuwa ni ngumu kumzuia mtu wa aina ya magufuli.
 
Mahakama ndio kwa sehemu kubwa huwa inawajibisha viongozi.

Katika hali ya sasa ambayo majaji wanachaguliwa na raisi na anawabadili akijisikia inakuwa ni ngumu kumzuia mtu wa aina ya magufuli.
Swadakta.
Madaraka makubwa kupita kiasi kwa mtu mmoja, ni tatizo kubwa sana la katiba iliyopo sasa. Ndiyo maana ni muhimu katiba mpya yenye kuzuia madaraka hayo itengenezwe.

Soma mchango wangu hapo juu nilivyoandika kuhusu hili jambo.
 
1. (a) Kwa maoni yako, wanaotaka KATIBA mpya wanaharakisha. JE WAJUA YA KUWA MJADALA WA KUTAKA KATIBA MPYA ULIANZA TANGU MIAKA YA 1980??? Je wajua?, tuanzie kwanza hapo.

(b) Unadhani inahitajika miaka mingapi ya kufanya maandalizi kabla ya kuanza mchakato?

2. Je, wewe mleta mada unafahamu vyema maana sahihi ya KATIBA YA NCHI YA KIDEMOKRASIA?

Watu wanakiuka KATIBA waziwazi, na KATIBA haina uwezo wa kuwaonya.

NB: Hujafanya kumlinganisha Mungu na madhaifu ya Tanzania
 
Mjadala wa madai ya Katiba mpya unaendelea kushika hatamu. Baadhi yetu wanadai kuwa nchi inahitaji Katiba mpya, wanatoa sababu zao. Madai yao ni ya kuheshimiwa kwa sababu ni haki yao lakini ni yenye kustahili kusahihishwa kwa sababu si ya kweli. Ni uongo..
Agiza wine bili kwangu mleta hoja.
 
Hayo yanafanyika kutokana na katiba tuliyonayo kutokuwepo na sheria yakumshtaki kiongozi mkuu wa nchi pindi anapoivunja hiyo katiba hata kama akitoka madarakani
 
Kwa namna moja uko sahihi; utii wa katiba imekuwa tatizo sugu kwa viongozi. Nini kifanyike? Au Katiba yenyewe inasemaje kwa wasiotaka kuitii? Ok, unaweza kusema asiyeridhika "aende mahakamani" kauli pendwa ya viongozi...
napinga hoja hii kwa asilimia 999 kabisa haiwezekani katiba yenye miaka 50+ isiwe tatizo dunia imebadilika sana na hata watu wanaotarajiwa kuongozwa kwa katiba hiyo kikongwe hawaongizeki tena huwezi endesha kwa katiba iliyoundwa na raisi aliyekua hana mpinzani eti itusaidie na kutuongoza kipindi pana wapinzani tena wenye uzoefu wa miaka 20 kwenye medani za kisaiasa mkuu nawasilisha tu.
 
Mleta mada, kama unakubali kuwa utii wa katiba ndio tatizo - ingefaa ukatuonesha ni mamlaka gani inayoweza kumshurutisha Rais kuitii. Bila shaka utasema ni kura ya kutokuwa na imani Bungeni. Je hujui pia kuwa Rais huyohuyo wanaeweza kumwondoa madarakani yeye pia anaweza kulivunja hilo Bunge?

Rais si ndio huteua majaji na hata jaji mkuu na hata Msajiri wa vyama vya siasa, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, wakuu wa Polisi, Majeshi, Wakuu wa mikoa na wilaya na wakurugenzi ambayo ni wasimamizi wa uchaguzi ngazi za majimbo?? Je unatambua wote hao wanawajibika katika mamlaka yake iliyo huru?

Kila siku unasikia Uwazi na Ukweli, kidogo Kilimo Kwanza, sijui Big Results Now, Kidogo Maisha Bora kwa Kila Mtanzania. Kabla maisha hayajawa bora inakuwa Hapa Kazi tu na sijui Uchumi wa Viwanda. Kidogo Miradi ya Kimkakati na sasa Kazi Iendelee (ipi?)

Katiba hukusudia kuratibu na kuongoza matendo ya wananchi na mamlaka yao!! Umesema wazi kuwa matendo ndio shida kuu, je yanaratibiwa? Jibu ni HAPANA!

Tuna rasilimali za kuwa matajiri lakini tu masikini - tatizo ni kutoratibu shughuli zetu! Katiba hujenga taratibu hizo!!!
 
Back
Top Bottom