Tatizo la tumbo

Tatizo la tumbo

Kafiti

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
537
Reaction score
220
nimekuwa nikisumbuliwa na tatizo la tumbo kujaa gesi kwa takribani kila siku kwa wiki mbili hizi, nimejaribu kupiga utrasound hamna kitu..........nimekunywa dawa ya minyoo likaacha kama siku 3, na leo naona limerudia.....linauma maeneo ya kitovuni.....please help
 
Unasumbuliwa na hewa nyingi katika tumbo Njia Mbadala za kupunguza hio tatizo ni:
1. Kula/Kunywa taratibu ili kuepuka kumeza hewa nyingi
2.Punguza/Epuka Kunywa vvyakula/vinywaji vinavyoongeza hewa katika tumbo mfano vyakula vyenye fiber nyingi au maziwa au product za maziwa kwasababu inawezekana una upungufu wa enzyme inayoitwa lactase ambyo inaivunja lactose(sukari iliyomo kwenye maziwa)kwahio kusababisha kuongezeka kwa hewa kwenye tumbo
3.Tumia dawa inayoitwa SIMETHICONE AU DIMETHICONE
 
DAWA YA TUMBO KUJAA GESI (COLIC): Ikiwa mtu atakula kwa wingi vyakula vinavyoleta gesi halafu vyakula hivyo visisagike vizuri tumboni, hukusanyagesi tumboni na kufanya mingurumo humo na kumsababishia maumivu,

humkosesha mtu utulivu na kumfanya kutoka jasho na machovu bila ya kufanya kazi.
Mtu hujisikia mara kwa mara aende haja kubwa na akienda hapati choo. Pia humsababishia mtu kuumwa kwa mgongo au kiuno. Ikiwa gesi hii

itakosa kutoka kwa njia ya haja kubwa, basi yaweza kupanda juu na kufanya presha sehemu au karibu ya moyo na kusababisha maumivu ya moyo.


TIBA: Chukua asali robo lita , unga wa arki susi vijiko vitatu vikubwa na unga wa habat soda vijiko viwili vikubwa. Koroga zote pamoja kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vya mchanganyiko huu ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto halafu yakishapoa unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili asubuhi na jioni.@
Kafiti14
 
hizi haswaa ndo dalili zangu ila nimeshindwa kuelewa.....unga wa arki suki na habat soda ndo kwanza nazisikia, naweza pata maduka ya gani hizo unga....dar es salaam
 
Tiba ya bure na rahisi tumbo kuuma/gesi/kuharisha tafuna majani ya mpera
 
Back
Top Bottom