Akili 09 Nguvu 01
JF-Expert Member
- Jun 23, 2015
- 695
- 1,377
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Nimekua nikisikia kutoka kwa baadhi ya watu(wateja wa benki ya CRDB) kuwa wameomba Mikopo kutoka katika benki hiyo lakini kwa muda mrefu hawajapatiwa fedha/mkopo huo lakini wameshaanza kukatwa fedha kwa ajili ya mkopo huo
Hivi karibuni nimekua mhanga wa jambo hilo(mkopo wa CRDB). Mimi ni mteja wa benki hiyo niliomba mkopo kutoka katika benki tangu tarehe 10 ya mwezi Machi hadi leo tarehe 30 Aprili sijapatiwa fedha?mkopo huo na wameshaanza kunikata,
Kila nikienda kwa Afsa mikopo wa branch hii ananiambia kua yeye ameshamaliza kila kitu shida ipo Makao makuu, yaani kwa sasa ukiomba mkopo benki ya CRDB mahali popote pale Tanzania hii basi Makao makuu ya CRDB ndo watalazimika kupitia Maombi yako na wao ndo wataamua kukupa au kutokupa. Baada ya kumsumbua sana Afsa mikopo akalazimika kunionesha list ya wateja walioomba mkopo tangu mwezi Machi lakini bado hawajapata
Nina rafiki yangu yupo mikoa ya Kaskazini nae aliomba mkopo CRDB tangu mwezi Machi naye hadi leo hajapata(tunawasiliana kila siku ili kujua maendeleo)
Benki ya CRDB kama hamna fedha za kutoa mikopo basi sitisheni tu kuliko kusumbuana na kutiana hasara namna hii(ninapoomba mkopo nakua na shida na fedha kwa wakati huo kwahiyo toeni mikopo kwa wakati,
Huu utaratibu wa mikopo yote Tanzania hii kuwekwa kutoka Makao makuu umeanza lini, mbona kipindi cha Mkurugenzi yule kulikua hakuna mambo haya? mjitafakari kama hamna fedha semeni
Kama una mpango wa kuombs Mkopo CRDB utachelewa sana, ikiwa aliyeomba mwezi machi hadi leo hajapata, je wewe ukiomba Mwezi huu utapata lini?' TAFAKARI, CHUKUA HATUA'
Nina hasira sana