Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu umemaliza kila kitu. umepita mule mule. Hata hivyo, niliwahi kuandika kwa urefu kuhusu suala la ufaulu duni wa wanafunzi wa kizazi hiki kwenye uzi huu hapa chini.Sababu zinazochangia ufaulu duni ni pamoja na,
1. IQ ndogo za wanafunzi
2. Wanafunzi kutumia muda wao mwingi kwenye mambo ya ngono, bangi, vigodoro, tamthilia, muziki na mpira
3. Usimamizi mbovu wa wazazi/walezi kwa watoto wao.
4. Jamii kuyachukulia masomo hayo kama masomo ya "Wateule" kitu kinachoathiri kisaikolojia mitazamo ya wanafunzi.
5. Mazingira duni ya kujifunzia.
6. Upungufu wa walimu wa masomo hayo, mfano utakuta shule ina wanafunzi 800 ila ina mwalimu mmoja au wawili wa hisabati, kwa mazingira hayo hakuna muujiza wa walimu kumudu kufundisha vema idadi hiyo.
7. Ualimu imebaki ni kazi kama kazi zingine na sio wito tena, hivyo walimu wako busy na maisha kuliko kazi.
8. Siasa.
.Acha niishie hapo kwa sasa.