Tatizo la Uke Kuwa Mkavu: Chanzo, Suluhisho na Ushauri

stable woman

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2013
Posts
3,884
Reaction score
4,479


Habari zenu?

Jamani ningependa kufahamishwa nini kinachopelekea ukavu sehemu za uke wakat wa tendo. Je, ni vyakula duni, uchache wa maandalizi au upungufu wa nguvu za kike?

Nawasilisha


WADAU WENGINE WANAOHITAJI KUFAHAMU UNDANI WA TATIZO HILI
Ushawahi kukutana na mwanamke ana uke mkavu sana yani hana ute, tatizo linasababishwa na nini? Tiba yake ni ipi? Maana unatumia mate weeee kulainisha njia mpaka yanakauka mdomoni.


MICHANGO YA WADAU


SABABU YA UKAVU WA UKE WAKATI WA KUJAMIIANA (TENDO LA NDOA)

Via vya uzazi vya mwanamke vimeundwa kwa hali ambayo inaweza kukabiliana na aina kama tatu za vitendo ikiwemo kujifungua, tendo la ndoa (kujamiiana) na kutolea uchafu (mkojo na damu ya hedhi). Kila kitendo kina mazingira au hali tofauti kukamilisha kitu husika, maandalizi ya mwili kujifungua ni tofauti na maandalizi ya mwili kwa tendo la ndoa. Wakati wa kushiriki tendo la ndoa ni muhimu kwa mwili wa mwanamke kupitia homoni zake kutengeneza na kutiririsha ute ambao hurahisisha upenyaji wa maumbile ya mume na kuepusha michubuko kutokana na msuguano.

Sababu zinazopelekea ukavu wa uke

Maandalizi hafifu au mabaya. Mwanamke ili aweze kushiriki kikamilifu katika tendo la ndoa inahitaji aandaliwe kwanza kabla ya kuanza tendo lenyewe.Yapo makosa ambayo kwa kusudi au bila kujua wanaume hufanya kwa wenza wao kipindi cha kushiriki tendo la ndoa ikiwemo la kutokumwaandaa vyema mke au mwenza wake.

Bila kujiandaa. Kwa hali ya kawaida tu uwezo wa kusisimka mwili hutofautiana kutoka mtu mmoja na mwingine. Wapo watu ambao wakishaona tu maumbile ya mwanaume wakiwa eneo husika hupata msisimko haraka na kuwa tayari kuingiliwa bila shida yoyote, lakini wengi ni muhimu kutumia muda kidogo kuuandaa mwili wake (zipo homoni zinazalisha maji/uterezi/ubichi ukeni) ili kumweka katika njia ya tendo la ndoa.

Maambukizi. Baadhi ya magonjwa kama vile fangasi na mengineyo huathiri mfumo wa utendaji kazi kwa mwanamke na kupelekea homoni zinazohusika kutengeneza ute kushindwa kufanya kazi.

Msongo wa mawazo. Mawazo yanpo kuwa makali huleta mambo mengi mwilini ikiwemo kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.Kwa wanandoa mara nyingi hubaki kuwa kama kutimiza wajibu tu.

Upungufu wa nguvu za kike. Kwa matatizo mbalimbali ya kiafya hasa magonjwa ya kudumu kama kisukari na TB pia unywaji wa pombe kali au ulevi wa kupindukia huchangia kupotea kwa utendaji kazi mzuri wa homoni hivyo kuleta ukavu wa uke

Kasoro za mfumo wa uzazi. Mabadiliko ya hali ya hewa,vyakula vipya,madawa ya magonjwa na vipodozi hasa vile vinavyokutana na ngozi moja kwa moja huweza kuleta mabadiliko mazuri au mabaya katika mfumo wa uzazi kwa njia ya kuchochea au kupoteza baadhi ya homoni.

Angalizo: Endapo tatizo hili linaonekana, ni vema kuonana na wataalamu wa tiba kwa ushauri wa kitabibu na badala yake kuacha kubashiri ni tatizo dogo au kubwa.

 
mchicha Mbogq,

Hapo palipokolezewa rangi panahusika. Epuka kumpiga mtama mwezio. Tulieni muongee maneno matamu ya mapenzi ili kuondoa/kupunguza msongo wa mawazo, kupumzika muda wa kutosha pamoja na kula vizuri. Ongeza kasi ya ULAJI WA BAMIA.
 
Kama mwanamke hajaandaliwa vizuri au hayupo tayari kusex .pia inachangia mzongamano wa mawazo na ugumu wa maisha ya kila .inatakiwa mwanamke alilax na awe tayari kwa tendo. Pia kuna baadhi ya magonjwa yanachangia hali hiyo .kwa ujumla zipo sababu nyingi sana.inabidii kumhona doctor kwanza.
 
Kutokula mlenda au bamia kwa wingi....teh teh!
 
Majibu unayo ndugu kitu ni maandalizi, andaa msosi wako vizuri kisha upalilie ndo upakue, tena hapo unamuumiza sana yani. ivisha msosi wako vizuri utaona raha wakati wa kula.
 
Msongo wa mawazo
Lishe duni
Maandalizi hafifu na wengine hua ni maumbile tu.

Na mi naomba kuelezwa, nguvu za kike ni zipi?
 
Kama huyo mkeo kakeketwa (Kaondolewa Kisimi) basi analo tatizo kubwa la kutopata hisia za tendo la ndoa. Fanya utafiti wa kumgusa sehemu nyingi za mwili wake utagundua ni wapi panamletea hisia kali. Ukisha pagundua basi kabla ya tendo la ndoa pashike, papapase mara nyingi iwezekanavyo hadi umuone amesisimka ndiyo uende huko mahalaelkubra na siyo kabla kwani utamletea maumivu makali na atachukia tendo lenyewe na wewe pia.
 
Acha kumbaka mke mkuu. Husifanye mapenzi ya jogoo, muandaye mke kabla ya kumuhingilia
 
Msongo wa mawazo
Lishe duni
Maandalizi hafifu, na wengine hua ni maumbile tu..

Na mi naomba kuelezwa..nguvu za kike ni zipi?

Swali zuri sana hilo.

NGUVU ZA KIKE: = Be yourself. Usijifanye kuwa mtu mwengine. Utapata tu mwenzi wako.

Trust me: mimi ni mwamme na nisingependa kujihusisha na mwanamke anaye-ACT.
 
Nguvu za kike ni kutoku act?
:A S-confused1::A S-confused1:..
Swali zuri sana hilo.

NGUVU ZA KIKE: = Be yourself. Usijifanye kuwa mtu mwengine. Utapata tu mwenzi wako.

Trust me: mimi ni mwamme na nisingependa kujihusisha na mwanamke anaye-ACT.
 
Nini kinasababisha mwanamke ambae hakua na uke mkavu kuwa na uke mkavu wakati wa kusex? Tiba yake ni nini?
 
Afanyiwe maandalizi ya kutosha kabla ya tendo. Pia awe anapakaa mafuta ya ubuyu huko kwenye nanihii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…