Tatizo la Uke Kuwa Mkavu: Chanzo, Suluhisho na Ushauri

Tatizo la Uke Kuwa Mkavu: Chanzo, Suluhisho na Ushauri

Hata Mimi mchepuko wangu ni mkavu sana hua tunatumia KY jelly na tunaenjoy tu
 
Wasalaam,

Mpenzi wangu uke wake mkavu, afanye nini ili kuwa na ute?
 
Kuosha kwa sabuni

Nini kinasababisha mwanamke ambae hakua na uke mkavu kuwa na uke mkavu wakati wa kusex? Tiba yake ni nini?


WADAU WENGINE WANAOHITAJI KUFAHAMU UNDANI WA TATIZO HILI




MICHANGO YA WADAU






SABABU YA UKAVU WA UKE WAKATI WA KUJAMIIANA (TENDO LA NDOA)

Via vya uzazi vya mwanamke vimeundwa kwa hali ambayo inaweza kukabiliana na aina kama tatu za vitendo ikiwemo kujifungua, tendo la ndoa (kujamiiana) na kutolea uchafu (mkojo na damu ya hedhi). Kila kitendo kina mazingira au hali tofauti kukamilisha kitu husika, maandalizi ya mwili kujifungua ni tofauti na maandalizi ya mwili kwa tendo la ndoa. Wakati wa kushiriki tendo la ndoa ni muhimu kwa mwili wa mwanamke kupitia homoni zake kutengeneza na kutiririsha ute ambao hurahisisha upenyaji wa maumbile ya mume na kuepusha michubuko kutokana na msuguano.

Sababu zinazopelekea ukavu wa uke

Maandalizi hafifu au mabaya. Mwanamke ili aweze kushiriki kikamilifu katika tendo la ndoa inahitaji aandaliwe kwanza kabla ya kuanza tendo lenyewe.Yapo makosa ambayo kwa kusudi au bila kujua wanaume hufanya kwa wenza wao kipindi cha kushiriki tendo la ndoa ikiwemo la kutokumwaandaa vyema mke au mwenza wake.

Bila kujiandaa. Kwa hali ya kawaida tu uwezo wa kusisimka mwili hutofautiana kutoka mtu mmoja na mwingine. Wapo watu ambao wakishaona tu maumbile ya mwanaume wakiwa eneo husika hupata msisimko haraka na kuwa tayari kuingiliwa bila shida yoyote, lakini wengi ni muhimu kutumia muda kidogo kuuandaa mwili wake (zipo homoni zinazalisha maji/uterezi/ubichi ukeni) ili kumweka katika njia ya tendo la ndoa.

Maambukizi. Baadhi ya magonjwa kama vile fangasi na mengineyo huathiri mfumo wa utendaji kazi kwa mwanamke na kupelekea homoni zinazohusika kutengeneza ute kushindwa kufanya kazi.

Msongo wa mawazo. Mawazo yanpo kuwa makali huleta mambo mengi mwilini ikiwemo kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.Kwa wanandoa mara nyingi hubaki kuwa kama kutimiza wajibu tu.

Upungufu wa nguvu za kike. Kwa matatizo mbalimbali ya kiafya hasa magonjwa ya kudumu kama kisukari na TB pia unywaji wa pombe kali au ulevi wa kupindukia huchangia kupotea kwa utendaji kazi mzuri wa homoni hivyo kuleta ukavu wa uke

Kasoro za mfumo wa uzazi. Mabadiliko ya hali ya hewa,vyakula vipya,madawa ya magonjwa na vipodozi hasa vile vinavyokutana na ngozi moja kwa moja huweza kuleta mabadiliko mazuri au mabaya katika mfumo wa uzazi kwa njia ya kuchochea au kupoteza baadhi ya homoni.

Angalizo: Endapo tatizo hili linaonekana, ni vema kuonana na wataalamu wa tiba kwa ushauri wa kitabibu na badala yake kuacha kubashiri ni tatizo dogo au kubwa.

 
Habari wanajamvi,

Naomba msaada wa kitabibu juu ya girlfriend wangu ambaye huwa ni mkavu sana sehemu za siri wakati wa kujamiana.

Huwa natumia muda mwingi kumwandaa kabla ya tendo hilo na pindi tunapoanza kujamiana huwa ni mkavu sana ingawa yeye huwa anafurahia na huwa hahisi maumivu.

Ninachotaka kujua ni kwamba hali hiyo ya ukavu sehemu za ndani ya uke ni tatizo la kiafya au ni kawaida na kama ndivyo nini kifanyike ili awe na hali ya kawaida.

Naomba msaada.
Mi naona hana hisia na wewe kuna kitu tu unacho labda elimu au ela ila hisia na ww za mapenzi hana utapatanae shida sana uyo wanawake wengi wanaolew na wanaume wasiowapenda kwajil ya masilahi tu ndo shida kama mwanaum unampenda ukimwangalia usoni tu wakati wa time ushaloa kabla hata hajakugusa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom