Tatizo la Uke Kuwa Mkavu: Chanzo, Suluhisho na Ushauri

Tatizo la Uke Kuwa Mkavu: Chanzo, Suluhisho na Ushauri

Duuu yaan tatzo hli hata wife analo. Uke kuwa mkavu, hisia hanazo nyingi, wakati wa hedhi shida tupu tatizo kubwa zaidi anadaka mimba zinatoka to. Sometimes anaweza jikuta na dalili zote za kuwa mama kijacho lkn ghafla hali hyo hutoweka.

Hormone imbalance ni tatizo sana. Hizo mimba kutoka zikiwa changa sana mara nyingi ni kushuka kwa Progesterone hormone ambayo ndio hushikilia mimba. Nendeni hospitali mapema, akishika mimba tuu hivi aanze kupewa extra Progesterone.
 
Nafikiri ni hormone imbalance. Nilikuaga naumwa sana tumbo la hedhi then hapo nyuma a few years ago nikawa na experience dryness hatakama mwanaume ameniandaa.

Nakushauri awe anakunywa Fennel tea, nunua mbegu za Fennel zenyewe na achemshe maji aweke hizo mbegu kijiko cha chai asubuhi na jioni, achuje then aweke asali kidogo anywe. Fennel sijui zinaitwaje Kiswahili. Ni moja ya viungo vya kupikia. Tafuta najua huko home ziko.

Au supu ya pweza. Inongeza Eostrogen pia. All the best. Jaribu kuangualia kama hio hali pia inatokea akiwa kwenye zile siku za hatari za kushika mimba. Hizo siku estogen inakuaga juu hivyo hamu ya kufanya mapenzi inakua juu na utelezi unazidi pia. Kama hapati hii, basi she def has hormone imbalance.
Ni kweli unachosema mkuu siku za hatari nakauaga na ute kimtindo na sexual desire inakuaga juu sana.
 
MAUNGIO.jpg

Kwa kawaida kwa kila mwanamke,uke wake unapaswa kuwa na hali ya unyevunyevu kutokana na ute mwepesi unaozalishwa ili kusaidia kuuweka uke katika hali hii.

Hormone inayojulikana kama estrogen ndo inayofanya kazi ya kufanya ute ute huu kuzalishwa ili kufanya uke kuwa na unyevunyevu na kuta za uke kuwa zinavutika(elastic). Pia ute huu husaidia kuweka sawa mazingira rafiki kwa mbegu za kiume,ili zinapokuwa zimeingia zisiweze kufa hadi zinapolifikia yai.

Kushuka kwa kiwango cha hormone ya estrogeni ni chanzo kikubwa cha kupungua kwa ute huu na kufanya uke kuwa mkavu.Kiwango cha hormone kinaweza kushuka kutokana na sababu mbali mbali kama tutavyoona katika makala hii.

Inaweza kuonekana ni jambo dogo,lakini kutokua na unyevunyevu wa kutosha inaweza kuathiri maisha ya muhusika haswa katika swala la kujamiiana.Ikiwemo kusababisha tatizo la maumivu wakati wa tendo la ndoa, na kupata tatizo la fangasi za ukeni mara kwa mara

CHANZO CHA TATIZO
Tatizo la uke kuwa mkavu linawakumba sana watu waliofikia ukomo wa hedhi (Menopause) Kutokana na sababu kwamba mwanamke anapofikia kipindi hiki mwili unapunguza au kuacha kutengeneza hormone hii ya estrogen. Hali hii hupelekea kuta za uke kuwa nyembamba na hazivutiki tena hali ambayo kitaalamu inajulikana kama Vaginal Atrophy.

Kiwango cha estrogen kinaweza pia kushuka kutokana na vitu vifatavyo:

1.Kuzaa na kunyonyesha. Kipindi hiki mwili unazalisha hormone ya maziwa (prolactin hormone) ambayo pia inazuia kuzalishwa kwa hormone ya estrogen.
2.Matibabu ya saratani. (Tiba ya mionzi na dawa za saratani)
3.Kutolewa mifuko ya mayai( ovaries)
4.Dawa zinazozuia uzalishwaji wa hormone ya estrogen kwa watu wenye tatizo la Uvimbe kwenye kizazi, (fibroids na endometriosis)

SABABU NYINGINE ZA UKE KUWA MKAVU NI:
SJOGREN SYNDROME ,Huu ni ugonjwa ambao kinga ya mwili inaharibu cell zinazotengeneza huu unyevunyevu
Dawa kutibu mzio( allergy) na mafua
Kusafisha uke hadi kwa ndani (douching)
Kusafisha uke kwa kutumia sabuni zenye kemikali
Kutoandaana kabla ya kufanya ngono.

UCHUNGUZI
Unapopata muwasho,au maumivu wakati wa tendo la ndoa na kuona uke wako ni mkavu vyema ukafika hospitali au ukawasiliana na daktari.Daktari atakuuliza maswali muhimu ili kubaini chanzo cha tatizo na atakufanyia vipimo na uchunguzi na atajua dawa gani inafaa.

MATIBABU
Matibabu yaliyozoeleka katika hili tatizo la ukavu ukeni ni kwa kutumia Estrogeni za kupaka au kupachika ukeni (topical estrogen),
Pia estrogen inaweza kuwa kaitka miundo mbali mbali kama ifatavyo:

Ring (estring) Hii inakua ni kitu cha duara kama pete ambacho mtu anawekewa ukeni,kinakua kinazalisha hormone ya estrogen,na kinabadilishwa kila baada ya miezi mitatu

Vidonge (Vagifem),Vidonge hivi ni bya kupachika ukeni vinakua na kifaa chake maalumu cha kusaidia kuviingiza ukeni.Unapachika kidonge kimoja kwa siku ndani ya muda wa week mbili.

Dawa za kupaka /cream (Estrace na Prematin)
Dawa hizi unapaka ukeni kila siku kwa muda wa wiki mbili.

MUHIMU: Dawa zenye Estrogen zinakuwa na maudhi madogo madogo (side effects) kama matiti kuvimba na kuuma na dawa za estrogen hazipaswi kutumiwa na watu wenye matatizo yafuatayo:

Saratani ya matiti
Saratani ya shingo ya kizazi
Wajawazito na wanonyonyesha
 
Kama sio tatizo la homoni laweza kuwa tatizo la PID.
 
Hakuna mwanamke aliyemkavu sehemu hizo. Labda awe ana hisia tofauti na hali halis au hakupendi kabisa. Vinginevyo maumbile yako pia yamekaa vibaya yanamtisha mwenzio.
Wako mkuu wengi tu mbona huwa wana lalamika sana, sema sio mfuatiliaji wa mada, so lazima uwe unabisha.
 
Nahisi atumia njia ya uzazi wa mpango kama kijiti au dawa zingine zinazobadili homoni ktk mwili wake.

Muoji na kama anatumia hizo dawa nendeni kwa daktari mkapate ushauri namna ya kuepuka hilo tatizo.

Njia ya asili ya kalenda au withdrawal method zimkwepesha natumizi ya dawa na kuondoa tatizo linalomkabili.
 
Wako wengine unamsikia amekojoa kabisa kwa jinsi anavyojikaza misuli lakini bado anakojoa hewa tu.
 
Ale vyakula kama mihogo mibichi, karanga mbichi na ndizi bukoba kwa wingi.
 
Habari wanajamvi.

Naomba msaada wa kitabibu juu ya girlfriend wangu ambaye huwa ni mkavu sana sehemu za siri wakati wa kujamiana.

Huwa natumia muda mwingi kumwandaa kabla ya tendo hilo na pindi tunapoanza kujamiana huwa ni mkavu sana ingawa yeye huwa anafurahia na huwa hahisi maumivu.

Ninachotaka kujua ni kwamba hali hiyo ya ukavu sehemu za ndani ya uke ni tatizo la kiafya au ni kawaida na kama ndivyo nini kifanyike ili awe na hali ya kawaida.

Naomba msaada.
Kiongozi sina uhakika kama unaelewa unachosema " Huwa natumia muda mwingi kumwandaa kabla ya tendo hilo na pindi tunapoanza kujamiana huwa ni mkavu sana ingawa yeye huwa anafurahia na huwa hahisi maumivu". anagalia hapo kwenye red na usirudie kusema uongo hususani hapa JF ila kwingine unaruhusiwa. Kabla hatujachukua hatua nyingine za kinidhamu nipatie majibu ya haya maswali:-

Itakuwaje awe mkavu halafu afurahie?

Kingine zakari inapitaje? na mwisho kwa mazingira hayo mchubuko ni nje nje. Hivyo mjiandae kwa UKIMWI na magonjwa mangine ambayo ni rafiki yake UZINZI.

Ila huyo mupenzi wako unaweza kumleta kanisani kwangu kwa ajili ya maombi maalum na kanisa linaitwa BREAST AND HONEY FELLOSHIP INATERNATIONAL. Maombi yanafanyika kila Alhamisi kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa sita usiku. Ukija nae wewe huruhusiwi kuingia Kanisani. Sasawa?
 
Na hapa lazima mtu apapaswe kuangalia kama ni mkavu kweli.
 
Hahahahahah! Na hapa lazima mtu apapaswe kuangalia kama ni mkavu kweli.
Kweli maana wengi wanadanganya, 😀😀😀 ushuhuda utakuja baada ya kuangalia na kama hajapona anabaki kwa maombi zaidi.
 
NSWECKY,
Hahahahahah. Hata ile Dimond "weka mate niteleze kama nyoka pangoni" imekushinda?
 
Back
Top Bottom