View attachment 1471846
Habari zenu?
Jamani ningependa kufahamishwa nini kinachopelekea ukavu sehemu za uke wakat wa tendo. Je, ni vyakula duni, uchache wa maandalizi au upungufu wa nguvu za kike?
Nawasilisha
WADAU WENGINE WANAOHITAJI KUFAHAMU UNDANI WA TATIZO HILI
MICHANGO YA WADAU
SABABU YA UKAVU WA UKE WAKATI WA KUJAMIIANA (TENDO LA NDOA)
Via vya uzazi vya mwanamke vimeundwa kwa hali ambayo inaweza kukabiliana na aina kama tatu za vitendo ikiwemo kujifungua, tendo la ndoa (kujamiiana) na kutolea uchafu (mkojo na damu ya hedhi). Kila kitendo kina mazingira au hali tofauti kukamilisha kitu husika, maandalizi ya mwili kujifungua ni tofauti na maandalizi ya mwili kwa tendo la ndoa. Wakati wa kushiriki tendo la ndoa ni muhimu kwa mwili wa mwanamke kupitia homoni zake kutengeneza na kutiririsha
ute ambao hurahisisha upenyaji wa maumbile ya mume na kuepusha michubuko kutokana na msuguano.
Sababu zinazopelekea ukavu wa uke
Maandalizi hafifu au mabaya. Mwanamke ili aweze kushiriki kikamilifu katika tendo la ndoa inahitaji aandaliwe kwanza kabla ya kuanza tendo lenyewe.Yapo makosa ambayo kwa kusudi au bila kujua wanaume hufanya kwa wenza wao kipindi cha kushiriki tendo la ndoa ikiwemo la kutokumwaandaa vyema mke au mwenza wake.
Bila kujiandaa. Kwa hali ya kawaida tu uwezo wa kusisimka mwili hutofautiana kutoka mtu mmoja na mwingine. Wapo watu ambao wakishaona tu maumbile ya mwanaume wakiwa eneo husika hupata msisimko haraka na kuwa tayari kuingiliwa bila shida yoyote, lakini wengi ni muhimu kutumia muda kidogo kuuandaa mwili wake (zipo homoni zinazalisha maji/uterezi/ubichi ukeni) ili kumweka katika njia ya tendo la ndoa.
Maambukizi. Baadhi ya magonjwa kama vile fangasi na mengineyo huathiri mfumo wa utendaji kazi kwa mwanamke na kupelekea homoni zinazohusika kutengeneza ute kushindwa kufanya kazi.
Msongo wa mawazo. Mawazo yanpo kuwa makali huleta mambo mengi mwilini ikiwemo kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.Kwa wanandoa mara nyingi hubaki kuwa kama kutimiza wajibu tu.
Upungufu wa nguvu za kike. Kwa matatizo mbalimbali ya kiafya hasa magonjwa ya kudumu kama kisukari na TB pia unywaji wa pombe kali au ulevi wa kupindukia huchangia kupotea kwa utendaji kazi mzuri wa homoni hivyo kuleta ukavu wa uke
Kasoro za mfumo wa uzazi. Mabadiliko ya hali ya hewa,vyakula vipya,madawa ya magonjwa na vipodozi hasa vile vinavyokutana na ngozi moja kwa moja huweza kuleta mabadiliko mazuri au mabaya katika mfumo wa uzazi kwa njia ya kuchochea au kupoteza baadhi ya homoni.
Angalizo: Endapo tatizo hili linaonekana, ni vema kuonana na wataalamu wa tiba kwa ushauri wa kitabibu na badala yake kuacha kubashiri ni tatizo dogo au kubwa.