Binafsi, huwa siamini mwanasiasa yeyote na ndo maana posts zangu ni nadra sana ukute natoa reference kutoka kwa wanasiasa!!
Kinyume chake, naifahamu Power Master Plan, na kuna siku hapa niliweka sehemu yake!
Kwa mfano, baada ya kujenga bomba, ilitakiwa pajengwe vituo 4 vya kuzalisha umeme pale Kinyerezi kwa sababu gesi ilishavutwa!!
Katika vituo 4 hivyo, JK alijenga kituo kimoja, na kingine kikawa kwenye mchakato! Ilitarajiwa Magu akiingia amalizie vituo 3 vilivyobaki!! Hadi umauti unamkuta, alijenga kimoja TU ambacho tayari mchakato wake ulishaanza, vingine vyote akapiga chini na kuhamia kwenye Bwawa la Nyerere ambalo tulitakiwa KUANZA MWANZO!!
What do you expect?
Na ingawaje watu mnaleta masihara sana, hadi sasa umeme wa gesi ni 57% ya umeme WOTE uliopo kwenye grid ya taifa!! Ulishawahi kujiuliza endapo Magu angejenga vituo vyote, hivi sasa kungekuwa na umeme kiasi gani kwenye grid ya taifa?!
Huku mkishangilia umeme wa maji, huku mkidanganywa kwamba mgao wa wakati wa JK ulitokana na watu kuziba maji, lakini ukweli ni kwamba umeme wa maji ni 36.6% TU!
Hapa chini ni Ripoti ya Wizara ya Nishati zama za JPM....
View attachment 2015891
Kumbe, ingawaje nchi ilikuwa inategemea zaidi umeme wa gesi, lakini bado tukatelekeza mradi wa ujenzi wa vituo vipya vya kuzalisha umeme pale Kinyerezi!!
Sasa unatarajia nini ile 36.6% tunayotegemea kutoka kwenye chanzo cha maji, inapokumbwa na changamoto ya ukame?! Au unakataa kwamba hakuna ukame?! Au unakataa kwamba vyanzo vya maji vimepungua?!
Na huyo aliyewahi kusema "tuna umeme mwingi" alizingatia kwamba kila siku wateja wapya wa umeme wanazaliwa, na matumizi ya umeme yanaongezeka?!