TANESCO
Habari za kazi?
Eneo letu la MARANGU MAUO Karibu na kanisa la KKKT BETHANIA kwa mwenyekiti Estomihi Mongi ambaye namba zake za simu ni
0753716202 Tunaomba msaada wa haraka.
Ninaijulisha ofisi yako kuwa tangu mwaka 2018 au kabla tumekuwa tukiripoti katika ofisi ya Tanesco HIMO-Moshi tatizo la nguzo kuoza, kuliwa na mchwa na kuinama kisha waya zake kuwa chini kwenye migomba na nyingine kushikiliwa kwa vijiti. Wakati wote ripoti zilipopelekwa tumeahidiwa mafundi kuja kufanya matengenezo haraka jambo ambalo halijawahi kutokea.
Kutokana na hali ya hatari inayoweza kutokea wakati wowote imenilazimu kuandika waraka huu na kuweka viambatanisho vya picha kwaajili ya ofisi yako ya Tanesco kuchukua hatua,
Tafadhali angalia viambatanisho.
Tunatarajia kusikia toka kwenu kuokoa janga linaloweza kutokea na ninatanguliza shukrani zetu.
View attachment 2087596
View attachment 2087600
View attachment 2087601
View attachment 2087602
View attachment 2087603