Tatizo la umeme kukatika; Waziri Makamba jipime kama unatosha au kung'atuka

Tafadhali onesha unalalamikia eneo gani na namba yako ya simu kwa huduma na taarifa zaidi

Huduma kwa Wateja
kuhitaji uwekewe namba ya simu kwa mtu anaetumia jina bandia humu Jf kunapelekea kutokuwepo na umuhimu wa yeye kutumia jina bandia.Namba za simu zimesajiliwa na watu hawahitaji kufahamika humu.

Urahisi ni wewe kuweka namba za simu za huduma kwa wateja akakupigia.
 
TANESCO
Habari za kazi?
Eneo letu la MARANGU MAUO Karibu na kanisa la KKKT BETHANIA kwa mwenyekiti Estomihi Mongi ambaye namba zake za simu ni 0753716202 Tunaomba msaada wa haraka.

Ninaijulisha ofisi yako kuwa tangu mwaka 2018 au kabla tumekuwa tukiripoti katika ofisi ya Tanesco HIMO-Moshi tatizo la nguzo kuoza, kuliwa na mchwa na kuinama kisha waya zake kuwa chini kwenye migomba na nyingine kushikiliwa kwa vijiti. Wakati wote ripoti zilipopelekwa tumeahidiwa mafundi kuja kufanya matengenezo haraka jambo ambalo halijawahi kutokea.

Kutokana na hali ya hatari inayoweza kutokea wakati wowote imenilazimu kuandika waraka huu na kuweka viambatanisho vya picha kwaajili ya ofisi yako ya Tanesco kuchukua hatua,
Tafadhali angalia viambatanisho.

Tunatarajia kusikia toka kwenu kuokoa janga linaloweza kutokea na ninatanguliza shukrani zetu.









 
Kwa kweli hii ni aibu kama Taifa tuko karne ya 21 haya mambo Duniani hakuna tena umeme kukatika katika huu ni ujinga wa mwisho sasa munataka maendeleo munataka waekezaji waje wakati hamuna ENERGY Vipi investors aje kuwekezaaa .Nishati zipo nyingi tu munashindwa kuzitumia .Jengeni Nuk ya Umeme hiyo ndio kiboko yao mutamaliza kila kitu na mutawauzia East na West africa .Dah Aibu sana sana ikifika usiku tu utajua hii nchi bla bla blaa nyingi sana vitendo Zeroooooooooo.
 
Tunashukuru kwa taarifa tunaifanyia kazi tafadhali
 
Unaweza kutuma taarifa hata Pm
 
Tunashukuru kwa taarifa

Tafadhali tujulishe

Eneo gani

Simu

Tatizo

Toka saa ngapi

Wengi au mwenyewe

Ahsante sana
 
Niko hapa Mbezi beach umeme umekuwa ukikatika unakaa kidogo unawaka then unakatika tena toka saa kumi usiku, umeshafanya hivyo kama mara 20 hivi naona hataru ya kuunguliwa na vifaa vya umeme. Hapa ninapoandika umekatika na hatujui utarudi saa ngapi, shughuli za kiuchumi zimesimama. Kweli nchi imefunguliwa kila mmojaanapambana ula kwa urefu wa kamba yake. RIP chuma
 
Tunashukuru kwa taarifa

Tafadhali tujulishe

Eneo gani

Simu

Tatizo

Toka saa ngapi

Wengi au mwenyewe

Ahsante sana
 
TAARIFA YA KUREJEA KWA HUDUMA YA UMEME LAINI YA JANGWANI 1

Wapendwa wateja huduma ya umeme imesharejea katika hali yake mara baada ya mafundi kugundua tawi la mti uliokuwa unagusa laini ya umeme maeneo ya mbezi beach Kidimbwi .

Kwa ambae bado anakosa huduma ya umeme muda huu tunaomba atupatie taarifa.

Endelea kufurahia huduma zetu.

Tanesco tunayaangaza maisha yako
 
huyu akitosha basi ,tunaweza kwenda hata sober house tukamteua teja yeyote ,na akaisimia wizara vyema tu!!
 
Hakuna atakayeweka namba za simuu au majina yake apa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…