1) Mheshimiwa Waziri wa Nishati January Makambaanadai kwamba:
a) Tatizo la Mgao wa Umeme limesababishwa na Uchakavu wa Miundombinu ambayo haijafanyiwa Matengenezo kwa miaka 5!!
b) Tanesco hawajafanya Matengenezo katika kipindi kilichopita cha miaka 5 (soma: Awamu ya 5) kwa sababu eti kila aliyejaribu kukata Umeme ili afanye Matengenezo alifukuzwa kazi!
c) Hakuna Tatizo la Maji!
2) Mheshimiwa Waziri Mkuu Majaliwa Majaliwa yeye amewahimiza Wawekezaji waje kwa wingi kuwekeza Tanzania maana tuna Umeme mwingi wa kutosha!
3) Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan yeye anadai kwamba Tatizo la Mgao wa Umeme limetokana na mambo 2 makubwa:
a) Ubishi wa Binadamu kuchepusha maji na shughuli nyingine kwenye vyanzo vya maji!
b) Kudra za Mwenyezi Mungu!
4) Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wao wametoa Taarifa Maalum wakidai kwamba Tatizo la Mgao wa Umeme Nchini limetokana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa yaliyosababisha Kiwango cha Maji katika Mito na Mabwawa kupungua sana!
5) Tanesco wanasema athari kubwa imetokea kwenye vituo vyetu vya kuzalisha Umeme vya Kihansi, Kidatu na Pangani. Wanasema hii imesababisha Upungufu wa Uzalishaji wa Umeme wa taklibani 345MW ambayo ni 21%. Eti ghafla wamekumbuka pia kwamba wanaweza pia kuzalisha Umeme kwa kutumia Gesi Asilia...!
6) Kwa kifupi:
a) Mheshimiwa Rais Samia anamlaumu Mungu!
b) Mheshimiwa Waziri Makamba analaumu Uchakavu wa Miundombinu!
c) Tanesco wanalaumu Mabadiliko ya Hali ya Hewa!
d) Mheshimiwa Waziri Mkuu yeye anamshangaa kila Mtu... maana anadai Umeme upo mwingi wa kutosha!
7) Nimepigwa na butwaa maana, kwa maoni yangu, hii ni aibu kubwa sana kwa Serikali (na kwa Taifa zima)! Na uthibitisho kwamba kweli (we are not serious!)
8) Nimebaki najiuliza:
a) Kwa nini Serikali inajichanganya kiasi hiki?!
b) Sasa sisi Wananchi tuelewe nini hapo?!
c) Hivi tukisema hizi ni dalili kwamba Serikali ni Dhaifu tutakuwa tunakosea nini?!
9) Nashangaa kwamba Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Tanesco, wote wanashindwa kukiri kwamba sababu kuu ya Mgao wa Umeme ni Serikali kutokua na Mipango mizuri, madhubuti na endelevu. Tunafanya mambo kama Zimamoto!
10) Aidha, tuwe makini sana na Ufisadi wa Mafisadi maana wana Nguvu kubwa, Mtandao mkubwa (ndani na nje ya Nchi) na Mbinu nyingi. Ni Wacheza Chess wazuri sana hawa.
11) Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli aliwabania sana Mafisadi kwa miaka zaidi ya 5. Nadhani sasa wanahaha kwa Hasira wakitafuta namna ya kuiba hadi kulipia "Hasara" waliyoipata.
12) Naamini kuwaomba radhi Wananchi wako pale unapoteleza ni moja ya misingi ya Utawala Bora. Ndio ustaarabu.
13) Ni matumaini yangu Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan atatafakari kwa makini hili Tukio la Aibu na kulipatia Ufumbuzi wa haraka! Asiyachukulie kirahisi Matatizo ya Watanzania... kuanzia Umeme, Maji, Mafuta, Mbolea na mengine! Wanapolalamika ajue kweli wanaumia!
14) Chochonde Mama Samia usiwaruhusu tena Mafisadi wakainajisi Nchi yetu! Ashakum si matusi!