Tatizo la Uoga wa kujumuika (Social Phobia)

Tatizo la Uoga wa kujumuika (Social Phobia)

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Ngoja tuongelee hili swala kidogo.

Huu ni uoga wa kujumuika na watu kwa sababu ya kuogopa kwamba unaweza kufanya jambo la kukuabisha au kuogopa kwamba watu wengine watakuonaje. Hapa haihusu watu wenye magonjwa au kasoro yeyote ambao wanaweza kuogopa kujumuika na watu kutokana na kasoro zao.

Watu wenye shida hii huwa waoga bila kuwa na sababu ya msingi. Watu hawa wanaweza kuogopa kutumia vyoo vya jumuiya au vyumba vya kubadilishia nguo (vya jumuiya).

Watu wengine wenye shida hii hali huwa mbaya sana kiasi hujikuta wanashindwa kuoa. Wengine huacha shule na wengine hushindwa kufanya kazi. Pia hutumia kila mbinu kuepuka kujumuika na iwapo watavumilia basi huwa kwa shida na huonyesha dalili za kupaniki kama moyo kwenda mbio, kutoka jasho, kuvurugika tumbo na wasiwasi (anxiety).

Pia watu hawa wako tayari wakae kimya waonekane wajinga kuliko ''kuaibika''. Mara nyingi shuleni au kazini huwa hawafanyi vizuri kulingana na uwezo wao halisi.

AINA ZAKE

Kuna aina mbili za Social Phobia

1. Wale ambao huogopa mijumuiko yoyote ile ya watu

2. Wale ambao huogopa baadhi tu ya mijumuiko.
Aina hii ya pili huogopa sana mijumuiko ambao wao ndio wanakuwa wahusika wakuu kama vile kuongea mbele za watu au siku ya harusi zao.

CHANZO CHA TATIZO:

Matatizo yote yahusishayo akili huwa na sababu tatu

1. Tatizo la Kijamii
Unaweza kuta wazazi wengine huwalinda sana watoto wao na hawataki wasahihishwe hivyo watoto wanakuwa wakubwa na kuwa waoga wa kukosea kwa sababu wanaogopa kusahihishwa (kitu ambacho hawajakizoea).

2. Tatizo la Kisaikolojia
Matatizo ya kisaikolojia huhusisha zaidi mtu anavyojiona na anavyowaona watu wengine. Watu wenye tatizo hili hupenda kuwaona wengine katika mtazamo hasi(huwaona wengine kama ni wasutaji au wenye kufurahia kuaibika kwao). Pia watu hawa huona kama dunia imejaa wasutaji hivyo hata kitendo kidogo hukichukulia kwa mtazamo hasi.

Mfano mtu anaweza akatabasamu kwa njia ya kawaida lakini mtu mwenye tatizo anaweza kuona tabasamu hilo kama ni la dhihaka. Watu hawa hufikiria sana jinsi walivyoonekana mbele za watu au jinsi walivyoongea kwa muda mrefu baada ya tukio kupita na hukazia fikra jinsi walivyokosea(kwa mtazamo wao).


3. Tatizo kwenye mfumo wa fahamu
Inaonekana kwamba watu wenye tatizo hili wana tatizo kwenye sehemu ya ubongo inayojihusiha na uoga. Tatizo hilo huwafanya waogope sana kuabika kuliko watu wengine na hali hii inaweza kurithiwa.

MATIBABU YAKE:

Kama tulivyosema, tatizo hili linasababishwa na mambo matatu hivyo matibabu nayo yamegawanyika katika sehemu hizo kuu tatu. Kumbuka kwamba hayo mambo matatu yanategemeana sana hivyo mtu jambo moja likitibiwa mengine nayo yanaanza kuboreka. Mfano kama ana tatizo kwenye mfumo wa fahamu akipewa dawa unakuta hata tatizo lake upande wa jamii linaanza kuboreka na anaanza kujumuika na wengine kirahisi na uoga unapungua na baada ya kuanza kujumuika unakuta na tatizo lake la kisaikolojia linaanza kuboreka anaanza kuwafikiria watu wengine katika njia chanya zaidi.

1. Tiba ya tatizo kwenye mfumo wa fahamu
Kwa wale ambao hushindwa kujumuika kwenye matukio yanayowahusu kama vile siku zao za harusi au kuongea mbele za watu dawa iwafaayo ni Propranolol. Dawa hii kwa kawaida hutumika kushusha presha.

Tumeona mtu mwenye tatizo hili anaweza kuwa na moyo unaoenda mbio, kutoka jasho, wasiwasi. Dawa hii ikitumika muda kidogo kabla mtu hajaenda kwenye jambo analoliogopa basi atalivumilia jambo hilo kirahisi na wasiwasi na moyo kumwenda mbio vitamuisha.

kwa wale ambao huogopa kujumuika kwenye mjumuiko wowote hupewa dawa za kuongeza kichocheo cha ubongo kiitwacho Serotonin, Mfano wa dawa hizo ni Paroxetine. Dawa hizi hutumika kwa muda mrefu na mara nyingi tatizo hujirudia baada ya kuacha hivyo dawa hizi huambatana na aina nyingine za matibabu.

2. Tiba ya tatizo la saikolojia
Lengo la tiba ya saikolojia ni kumfanya mtu awaone watu wengine kwa njia chanya na kumfanya aone kukosea na kujajiwa/kusutwa na mambo ya kawaida. Mfano vinaweza kuandaliwa vipindi ambavyo mtu mwenye tatizo atatakiwa kuongea mbele ya kundi dogo la watu au mbele ya mtoa tiba na kisha kuulizwa vitu ambavyo vimemuogopesha na vikafanyiwa kazi kwa pamoja. Kidogo kidogo anaanza kuona kwamba vitu alivyokuwa anaviogopa sio vitu vya kuogopa. Pia kwa kuona waongeaji wengine anakuwa anazidi kupata uzoefu kwamba kukosea ni jambo la kawaida na anaanza kuwa na mtazamo chanya kwamba kujajiwa ni kwa ajili ya kumjenga na sio kumuaibisha.

3. Tiba ya tatizo la kijamii
Lengo la tiba hii ni kumfanya mtu mwenye tatizo ajichanganye zaidi na wengine. Hapa mtu huyu huweka katika kundi la watu wenye matatizo kama yake (group therapy) na hufanya mambo mbalimbali kama kuandaa mada, kuiwasilisha mbele za wenzake na kufanya majadiliano katika vikundi na mambo mengine.

Nafikiria JamiiForums inaweza kuwa njia nzuri ya kujitibu tatizo hili. Jaribu kuanzisha post au kuchangia post na pia kusoma post mbalimbali. Utaona kuwa wachangiaji wengi sio kwamba wana uwezo mkubwa sana kuliko wewe, pia utaona kwamba kukosolewa ni jambo la kawaida na utajisikia vizuri zaidi watu wanapofurahia post zako.

Kwa ujumla tiba hizi zote husaidia sana kuondoa tatizo hili la uoga wa kujumuika (social phobia) na hata kama tatizo lipo kwenye mfumo wa fahamu kupitia tiba hizi hupungua au kuisha kabisa.

Wenu katika kujumuika Red Giant
 
yaani my eyes are stuck on your avatar, nimeshndwa hata kusoma
 
Nafurahi sana kukutana na uzi huu Mkuu Red Giant

Mimi ni mhanga wa Social Phobia. Kwanza nikiwa sehemu yenye watu wengi naishiwa nguvu kabisa achilia mbali kuongea mbele yao.

Nilitaka kuacha chuo nikiwa mwaka wa mwisho kutokana na kuaibishwa na ticha mmoja siku ya presentation ya awali. Nikafanya project yangu vizuri nikamaliza ila siku ya presentation ya mwisho sikuweza kwakweli nikajifungia ndani.

Nimeimprove over the years though huwa inanitesa sometimes kwenye event mbalimbali hasa za kazi. Nitazifanyia kazi mbinu za tiba hapo juu.
 
Nafurahi sana kukutana na uzi huu Mkuu Red Giant

Mimi ni mhanga wa Social Phobia. Kwanza nikiwa sehemu yenye watu wengi naishiwa nguvu kabisa achilia mbali kuongea mbele yao.

Nilitaka kuacha chuo nikiwa mwaka wa mwisho kutokana na kuaibishwa na ticha mmoja siku ya presentation ya awali. Nikafanya project yangu vizuri nikamaliza ila siku ya presentation ya mwisho sikuweza kwakweli nikajifungia ndani.

Nimeimprove over the years though huwa inanitesa sometimes kwenye event mbalimbali hasa za kazi. Nitazifanyia kazi mbinu za tiba hapo juu.

pole sana. i hope umepata nafuu kwa sasa
 
Elimu nzuri sana mkuu mi mi muathirika mkubwa sana wa hilo jambo na zaidi sana ni kusimama mbele za watu.
 
Back
Top Bottom