Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume: Chanzo cha tatizo na ushauri wa jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo

hizi mada zimezidi sasa apa.........meza Erectomia hahahaaaaaaaaaaaaaa
 
.........kwa wanaume wenzangu, nashangaa , kila mganga wa kienyeji (kama ataandika tangazo, ama atakua anatangaza) hiyo ndio kauli mbiu yao, je hivi ni tatizo sugu tulonalo au ninini........?
 
ni kutokujiamini tu mkuu.... hakuna tatizo hapo
 
hakuna jipya nguvu zinzongezwa kwa kula chakula bora, nakufanya mazoezi ilikuwa napumzi na sio chipsi
 
ni tatizo kweli lipo hasa kwa wale wapenda kujichua..si unanajua tena bwana hii habari ya kujipa self service imezidi sana siku hizi kwa vijana
 
Wala sio tatizo, bali tunatafuta nguvu za ziada bana ..................... Fikiria mtu ana mke, ana nyumba ndogo, bado kuna House girl na kuna wale wa chap chap a.k.a one night stand kwenye semina au warsha au workshop .........
Wewe unatarajia nguvu za asili zitatosha ...................................!?
 

We manyema si unywe supu ya konokono?
 
.........kwa wanaume wenzangu, nashangaa , kila mganga wa kienyeji (kama ataandika tangazo, ama atakua anatangaza) hiyo ndio kauli mbiu yao, je hivi ni tatizo sugu tulonalo au ninini........?

Ni tatizo sugu hasa kwa wasio wazoefu wa majambozi! Fikria unaburudika na mpenzi wako, .......n.k unamaliza mzunguko uko hoi, mara unaambiwa " haaa haaa jamaniii jamanii haraka ya nini mbona hunifikishiiiii....Hapo utaanza kuumiza kichwa! Inamaana huwa kuna mijamaa inamfikisha huko mawinguni? Then huyooo kwa mganga wa miti shamba. Ila unaweza usiende huko. Tulia, googles utapata majibu na utakuwa kama simba dumeeeeeee!
 
.........kwa wanaume wenzangu, nashangaa , kila mganga wa kienyeji (kama ataandika tangazo, ama atakua anatangaza) hiyo ndio kauli mbiu yao, je hivi ni tatizo sugu tulonalo au ninini........?

Mambo yanayochangia upungufu wa nguvu za kiume




LEO ninataka tuangalie kwa kina mambo yanayochangia tatizo hilo upungufu wa nguvu za kiume. Ningependa tulio katika ndoa, ukishaisoma makala hii tuwahusisishe wenza wetu nyumbani au mpigie rafiki yako na kumueleza kuwa ana nafasi ya kujilinda kupoteza


nguvu za kiume na hivyo kuwa na uhakika wa amani nyumbani.
Nasema amani kwa sababu tatizo hili huingilia amani nyumbani kwani kuna kuhisiwa kuwa mwanaume anajihusisha na nyumba ndogo maarufu. Uzoefu katika vituo vyetu vya Marie


Stopes kina mama ndio huja kutafuta ushauri kwa nini mzee kabadilika na wafanye nini ili kumrudisha nyumbani. Zifuatazo ni sababu amabazo kitaalamu zinatajwa kuchangia kupungua kwa nguvu za kiume na nyingi kama si zote zinaepukika.


Msongo wa mawazo: Ni dhahiri kuwa akili na tendo la ngono vinategemeana sana. Inajitokeza mara nyingi sana kwa watu wenye matatizo katika biashara, kazini na sehemu nyingine hujikuta hawako katika hali ya kuwa na hamu ya tendo la ndoa mpaka pale


watakapotulia. Hii inaweza kuwapata watu wa rika zote na tatizo hili linaweza kuisha haraka kutegemeana na shughuli zao zinavyorudi katika hali ya kawaida


Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu. Mzunguko wa damu mwilini una maana sana kwani kama damu haizunguki vizuri itachangia uume kutosimama vizuri kwa sababu usimamaji hutegemea kiasi na kasi ya damu inayoingia kwenye mishipa ya sehemu hiyo. Dawa zinazotumika kutibu shinikizo la damu huchangia pia kupungua kwa nguvu za kiume.


1. Unywaji pombe kupita kiasi: Pombe inaweza kuathiri mishipa ya damu na mishipa ya fahamu kwa wakati mmoja. Wakati mwingine mtu akilewa sana huathiri ubongo na kukata mawasiliano kisaikologia na hivyo kushindwa kuwa katika hali ya kuwa na hamu ya ngono na hivyo kutosimamisha.


2. Unene. Unene huwa unaambatana na mafuta mengi mwilini. Mafuta hayo wakati mwengine huzidi kwenye kuta za ndani za mishipa ya damu na hivyo kupunguza ukubwa wa mrija kiasi kwamba damu inipita kidogo na kwa shida. Hii huchangia kupungua kwa nguvu za kiume kwa sababu kiasi cha damu kinachotakiwa kisimamisha uume kitakuwa kidogo sana. Wakati mwingi uume unaweza kusimama kidogo na kulala kabla shughuli haijakamilika.


3. Kutokufanya mazoezi: Tusipofanya mazoiezi pia mzonguko wa damu kutokuwa mzuri na hivyo kutoparuhusu damu ya kutosha kusimamisha uume. Kwa watu wanaotembelea magari na shughuli za kukuaa maofisini mda mrefu na hasa kama hawafanyi mazoezi asubuhi au jioni wako kwenye hatari zaidi kuliko watu wanotembea kwa miguu mwendo mrefu na kufanya kazi ngumu za kuuchosha mwili.


5. Matatizo ya kisukari: Kisukari ni ugonjwa unaoathiri mishipa ya fahamu na kufanya mishipa ya damu kutofanya kazi yake viuri ili kuruhusu damu kujaa kwenye uume. Hii himfanya mgonjwa wa kisukari kushindwa kusimamisha hata kama ana hamu ya kufaya tendo hilo.


5. Umri: Inaelezwa kuwa kadri umri unavyopanda ndio uwezo wa nguvu za kiume utaendelea kupungua. Baadhi ya watu huanza kuona tatizo hili wanapofikia umri wa miaka 40 na kuendelea na hasa kama maisha yao hayakuwa na mazoezi ya mwili. Sababu


nyingine ni kama utumiaji madawa ya kulevya, kuumia katika uti wa mgogongo, uvutaji sigara nk. Sababu nyingi zinachangia kupungua kwa nguvu za kiume zinaepukika kwa hiyo tunashauriwa kuwasiliana na wataalamu ili kujifunza jinsi ya kujikinga au kutibu matatizo



Chanzo: Mambo yanayochangia upungufu wa nguvu za kiume.

Mkuu sinafungu Dawa ya Kuongeza nguvu ya Kiume Bonyeza hapa https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/196934-dawa-za-nguvu-za-kiume-kwa-anaye-taka.html

MziziMkavu kwa ushauri zaidi nitumie email (fewgoodman@hotmail.com)
 
Last edited by a moderator:

Kama upo maeneo ya miji ya pwani, pata supu ya pweza.
 
Kwa heshima kubwa naomba tupeane maarifa ya tiba mbadala ya kuongeza nguvu za kiume kwa juice ya tende.
Mahitaji.
1. Robo kilo ya tende
2. Maziwa nusu lita
3. Blenda ya kusagia
4. Bakuli
5. Birauli

Hatua
i. Ondoa kokwa za tende na tia kwenye blenda
ii. Changanya tende na maziwa.
iii. Blendi maziwa na tende kwa muda wa dakika 5 mpaka upate juice laini.

Matumizi.
Kunywa birauli 1 hadi mbili mara 3 kwa siku kwa kiasi cha siku utakazo weza.

Sharti.
Usichanganye wala kuongeza sukari kwenye juice hiyo.

Faida.
i. Hutibu chango la kiume na kike (tumbo kunguruma na kujaa gesi)
ii. Hutibu tatizo la choo ikiwa ni pamoja na wale wenye kutoa choo
mithili ya mnyama mbuzi.
iii. Inaweza kutumiwa na mtu yoyote wa jinsia yoyote.
 
Tende!Inabidi niamie zanzibar sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…