Nimechelewa kukujibu sababu ya majukumu mengine.
Upungufu wa nguvu za kiume "erectile dysfonction" husababishwa na vitu vingi.
Utanisamehe kwa Kiswanglish.
1. Magonjwa kama Kisukari na Shindikizo la damu.
2. Unene kupita kiasi na ugonjwa wa usingizi "Sleep Apnea".
3. Matumizi ya tumbaku.
4. Baadhi ya tiba kama Mionzi kwa ajili ya Saratani, opareshi ya Tezi dume nk.
5. Tiba kama za msongo wa mawazo "antidepressants", Tiba za shindikizo la damu nk
6. Magonjwa kama magonjwa ya saikolojia "Depressions, Antiety and Stress".
7. Kunywa pombe kupita kiasi.
8. Kuumizwa kwenye sehemu za nyonga kwenye michezo nk "Physical injuries on pelvic region".
9. Upungufu wa homoni za kiume "Low testosterone".
10. Baadhi ya magonjwa ya mishipa ya fahamu "Some neurological diseases".
11. Matatizo ya kimahusihano kati ya mgonjwa na mwenza wake. (Relationship problems due to stress, poor communication or other concerns).
Hizo ni baadhi ya sababu "Risk Factors" zinazopelekea mtu kukumbwa na tatizo la nguvu za kiume.
Tiba yake inategemea na sababu yake, kwahiyo tiba inatofautiana mtu.
1. Tiba bora ya Shindikizo la damu na Kisukari
2. Kupunguza unene kwa kufanya mazoezi na lishe bora.
3. Kuacha matumizi ya tumbaku.
4. Kupunguza kunywa pombe kupita kiasi au kuacha kabisa.
5. Pata tiba bora ya saikolojia.
6 Uwe maelewano mazuri na mwenza wako.
7. Viagra hutumika kutibu kwa sababu imethibitishwa kwa matumizi ya "erectile dysfonction"
Hizi ni baadhi vitu unawezakufanya ili kukisaidia kuondokana na tatizo hilo.
Hiyo Kidaktari, tofauti na kiswahili swahili mtaani zile tiba za asili ALKASUSU, MCHUZI WA PWEZA, VUMBI LA KONGO na zingine nyingi, hazina uthibitisho kisayansi lakini zinasaidia kiasi fulani kuongeza kujiamini kitaalamu inaitwa "Placebo effect" . Au inawezekana kuwa zinatibu kweli.