Habarini za asubuhi wakuu, natumaini mmeamka salama kabisa, Mungu aendelee kuwaongoza.
Jamani mimi kijana wenu nimekuja hapa nina changamoto kubwa sana ya upungufu wa nguvu za kiume.
Halii hii inanitesa sana, yaaani nikiangalia umri wangu na tatizo ambalo ninalo roho inaniuma najiona mwanaume nisie na faida😞
Imefikia hatua sasa mpenzi wangu anataka kuniacha, maana kasema tutaishi vipi mimi nikiwa na hali hii.
Maana hapo mwanzo nilimuomba anipe muda kumuhaidi kuwa nitatatua hii changamoto inayonisumbua lakini wapi imeshindikana
Na kinachoniuma zaidi nimeshatumia pesa nyingi, kwa upande wangu nasema ni nyingi kutokana sina shughuli rasmi, so shughuli zangu ni za kuunga unga tu.
Jaman naandika huu uzi wakati moyo wangu ukiwa na masononeko kweli
Hata nilijaribu kutembelea baadhi ya hizi taasisi za tiba mbadala tena zenye majina makubwa na ndio huko pesa zangu ziliisha kabisa, hadi sasa nimebaki mtupu hapa na bado tatizo linaendeleaa (sijapona bado hii changamoto)
Jaman mwenye kujua jinsi ya kutibu hili tatizo anisaidie wakuu, maana imefikia hatua hata nikikutana na wadada siwezi tongoza maana hizo nguvu sina kabisa
Daah, Roho inaniuma sana